Friday, July 18, 2014

Leo hii Stamina ametengeneza gumzo kwa mashairi yaliyo katika wimbo wake mpya na Nay wa Mitego "Huko Kwenu Vipi" ambao wamejibizana kuhusu mziki wa kuimba na mziki wa hiphop (Ngumu)
Lengo kubwa katika ngoma hii ni kutuweka pamoja wasani, kusiwe na tabaka la bongo fleva hivi hiphop hivi wote tuwe kitu kimoja amesema Stamina.
huu ni mmoja kati ya mashairi yaliyoko katika wimbo huo .
 
Stamina " kwa kupost picha insta, hilo mnaongoza, utaskia mjengo wangu mpya kumbe umepanga mnajiongeza. naskia daily mpo gym eti mnatanua vifua, wakati mkirudi makweni wengi wenu mnajichubua
 
Nay wamitego: " Nyie mnajifanya mnakaza huku mnakufa na njaa, hakuna mnachopata zaidi ya sifa kwenye mitaa, kwanza mnatudhalilish akutwa mnatupiga vizinga, umerekani mwingi mpaka mnakula unga"

 Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso akifuatiwa na  Meneja Masoko wa Airtel bi, Prisca Tembo ,na Mwenyekiti wa shirikisho la  wadau wa Utalii Tanzania Bwana Gaudence Temu , wakionyesha vifurushi vya bidhaa mpya ya Airtel Tourist Pack , wakati wa uzinduzi wa kifurushi hicho kitakacho wawezesha watalii kuwasiliana na familia zao mara wawapo nchi katika utalii, uzinduzi hu umefanyika leo katika makao makuu ya Airtel Daressalaam
 Mkurgenzi mtendaji wa Airtel Tanzania bw, Sunil Colaso akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kifurishi chenye vocha maalum na laini ya Airtel kwaajili ya watalii wanaoingia nchini kitakachojulikana kama Airtel Tourist pack, uzinduzi huo umefanyika leo  ambapo Watalii watakaofaidika ni wale wanaotoka Amerika, India, Italia na Uingereza kufaidika na 'Airtel Tourist pack'


*        Watalii toka Amerika, India, Italia na Uingereeza kufaidika na 'Airtel Tourist pack'
*        Airtel yapunguza gharama za kupiga simu na intaneti kwa watalii  toka Amerika, India, Italia na Uingereeza

Dar es Saalam, Juni 17, 2014, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekuja na ubunifu mpya wa bidhaa itakayojulikana kama AIRTEL TOURIST PACK maalum kwa wageni/watalii wanaotembelea nchini toka mataifa mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora ya mawasiliano nafuu kwa kuwaweza kuwasiliana na ndugu na familia zao wawapo kwenye utalii wao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema" Huduma hii mpya ya "Vifurushi vya watalii" itapunguza usumbufu kwa mtalii/mgeni kukosa mawaliano bora ya simu au Intaneti awapo katika sehemu mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini.

Ni imani yangu kuwa wageni watafurahia huduma hii kutokana na ubora wa mawasilano ya Airtel hasa katika maeneo ya pembezoni mwa miji ambako ndiko vivutio vingi vya utalii vinakopatika.

"Kifurushi hiki cha watalii kitakuwa na muda wa maongezi  wa dakika 30 za kupiga simu za nje, dakika 10 za kupiga simu za ndani ya nchi, SMS 10 kwenda mtandao wowote ndani na nje ya nchi pamoja na kifurushi cha intaneti cha 1GB vitakavyodumu kwa muda wa siku 30" alieleza Bw, Colaso

Kifurushi cha watalii Airtel Tourist Pack pia kinakuja na Laini ya simu na vocha ambapo, hii ni kwa yule mteja ambae hana laini ya Airtel au anataka kujiunga na kufaindika na huduma

Mtumiaji wa "Kifurushi cha watalii" Airtel Tourist pack atatakiwa kusajili namba yake pale tu anapofanya manunuzi kwa kutoa kitambulisho au pasi ya kusafiria.  Usaliji huo utakuwa wa muda kwa siku 30 na baada ya hapo mtalii atatakiwa kutoa kopi ya kitambulisho au pasi ya kusafiria kwaajili ya usajili wa kudumu.

Huduma hii ya vifurushi kwa wageni wakutoka nje ya nchi kwa simu ni ya kwanza kutoka Airtel na inampatia mteja uhuru wa kuwasilina  na ndugu jamaa na marafiki nyumbani kwa gharama nafuu zaidi kuliko ilivyokuwa awali, wateja watafurahia huduma za internet kwa kujiunga na mitandao ya kijamii, kutuma picha na video kwa gharama nafuu wakati wote . Aliongeza Colaso

Kwa upande wake mgeni rasmi, Mwenyekiti wa wadau wa Utalii nchini Bw, Gaudence Temu alisema "kwa niaba ya wadau wote wa utalii, ninaipongeza sana Airtel kwa kuanzisha huduma hii ya vifurushi vya mawasiliano kwa watalii wanaoingi nchini. Huduma hii inaendana na mahitaji ya wageni wetu na inakwenda sambamba na dhamira yetu sisi wadau ya kuendelea kutoa huduma bora katika soko.

"kwa kupitia mtandao wa Airtel ulioenea zaidi maeneo ya vijijini wageni wetu sasa watakuwa na uhakika wa mawasiliano bora na kwa gharama nafuu wakati wote" alieleza Bw, Temu

Mwenyekiti huyo pia alitoa ushauri kwa wadau wote wa biashara ya utalii kuchangamkia fulsa hiyo kwa kuwajulisha wageni wanaoingia nchini ili waweze kufaidika na punguzo hilo ambalo kwa msimu huu wa utalii hutumia gharama kubwa katika mawasiliano.

"Migahawa na Hoteli, wadau wa usafirishaji, watembezaji watalii na wadau wote hii ni fulsa kwetu kuwapa habari njema wateja wetu wanapoingia nchini kwamba kuna Tourist pak yenye faida zote hizi" alimaliza kwa kusema Bw, Temu

Vifurushi vya watalii zitapatikana katika maeneo yote ya biashara katika maeneo ya kuingia nchini kama zile viwanja vya ndege vya Dar es saalam(JKIA), Zanzibar, Arusha na KIA. Pia zinapatikana katika hoteli na migahawa ya kitalii.

Nchi zitakazofaidika na huduma hii kwa sasa ni pamoja na Amerika, India, Italia na Uingereeza

Van Gaal was all smiles as he took his fist press conference as Manchester United manager
Van Gaal alikuwa na tabasamu kubwa wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari katika klabu ya Manchester United manager.

LOUIS van Gaal hataleta kombe la ligi kuu Manchester United katika msimu wake kwa kwanza, kwa mujibu wa kocha wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp.
Redknapp, aliyekamilisha usajili wa beki wa zamani wa United, Rio Ferdinand jana alhamisi, haoni kama Mholanzi huyo atapata kombe bila kuwa na wachezaji wanne wa kiwango cha juu, achalia mbali  Luke Shaw na Ander Herrera waliosajiliwa.
'Van Gaal ana rekodi nzuri, lakini wanahitaji wachezaji," .Redknapp aliwaambia  talkSPORT.
The new United boss got to know his new surroundings with club legend Sir Bobby Charlton
Bosi mpya wa United alipata nafasi ya kujua mazingira ya klabu akiwa na gwiji wa klabu hiyo Sir Bobby Charlton.
"Anahitaji kuleta wachezaji angalau wanne au watano ili kurudi pale alipokuwa Alex (Ferguson), ambapo walishinda makombe".
"Kwa hatua hii kama ingekuwa ni kucheza kamari ya wao kushinda  ubingwa msimu ujao, nisingewapa nafasi ya kushinda, vinginevyo wanasajili wachezaji watatu au wanne wa kiwango cha juu".
Redknapp alitaja washindani wa ubingwa msimu ujao kuwa ni  Chelsea, Manchester City na Arsenal na kusema Man United watahangaika kufika juu baada ya kushuka wakati wa David Moyes.
Opinionated: The QPR manager spoke to the media on Friday morning
 Kocha wa QPR alizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi.
New signing: Rio Ferdinand (left) took part in his first training session with QPR on Friday morning
Jembe jipya: Rio Ferdinand (kushoto)  akishiriki mazoezi yake kwa mara ya kwanza leo asubuhi katika klabu ya  QPR 
"Sioni kama watakuwa imara kama Chelsea au Man City," aliongeza. "Nadhani Asernal wamefanya usajili mkubwa kwa kumleta Alexis Sanchez, kwahiyo msimu ujao wanaweza kuukaribia ubingwa zaidi".
"Bado ni wazi. Ningependa kuwaona Liverpool wanakuwa na msimu mzuri tena, lakini wamempoteza mchezaji wa ajabu (Luis Suarez). Hana mbadala kwakweli".
Catching up: Arsenal could play a big part in this season's title race after signing Chilean striker Alexis Sanchez from Barcelona
 Alexis Sanchez amesajiliwa na Asernal kutokea klabu ya Barcelona


Moving on: Luis Suarez, signs Uruguay shirts and flags and throws them back to fans outside his house
 Luis Suarez, alitia muhuri katika jezi na bendera ya Uruguay na kuwatupia mashabiki nje ya nyumba yake.

Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 11:07 jioni

BARCELONA inatarajia kumpa majukumu mpya nyota wake Lionel Messi ambapo sasa atacheza nyuma ya washambuliaji wawili, Luis Suarez na Neymar, kwa mujibu wa ripoti za Hispania.
Kuelekea msimu ujao, Kocha Luis Enrique anataka kuwatumia washambuliaji wote watatu kwa wakati mmoja ndani ya kikosi chake.
Enrique anaamini kumhamisha Messi katika nafasi aliyozoeleka kucheza na kumchezesha nyuma upande wa kulia, kutawafanya Suarezi na Neymar wang`are zaidi. 
Lionel Messi is set for a new role at Barcelona
Lionel Messi is set for a new role at Barcelona
Mabadiliko: Lionel Messi anatarajiwa kupewa majukumu mapya katika klabu yake ya Barcelona, sasa atacheza nyuma ya Suarez na Neymar.

Main man: Neymar will join Suarez in attack after the Brazil star recovers from his fractured vertebra
Mtu muhimu: Neymar ataungana na Suarez kuongoza safu ya ushambuliaji ya Barcelona baada ya kupona majeruhi yake ya kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Suarez amefungiwa mpaka mwezi oktoba mwaka huu kwa kitendo cha kumng`ata beki wa Italia , Giorgio Chiellini  kwenye mechi ya makundi ya kombe la dunia nchini Brazil.
Baada ya kitedo hicho aliamua kuondoka Liverpool na kujiunga na Barca kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 75.
Wakatalunya wanasemekana kuanza harakati za kukata rufani juu ya adhabu hiyo.
Barcelona pia wanamsubiri Neymar apone majeruhi yake aliyoyapata kombe la dunia  hatua ya robo fainali.
Taifa mwenyeji bila Neymar lilipigwa mabao 7-1 kwenye mechi ya nusu fainali dhidi ya Ujerumani.
Wakati huo huo, Messi alitajwa kuwa mchezaji bora wa mashindano licha ya Argentina kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ujerumani katika mechi ya kfainali.



Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 8:32 mchana

Semina elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars kwa mikoa sita inafanyika kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.


Washiriki wa semina hiyo ni kutoka mikoa ya Mbeya (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Mwanza (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Morogoro (Katibu), Ilala (Katibu na mwakilishi wa wanawake).


Temeke (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Kinondoni (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Dar es Salaam (Mwenyekiti na Katibu), na Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) kitakachowakilishwa na mwakilishi wa wanawake.


Washiriki wengine katika semina hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ni wajumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana ya TFF.


BONIFACE WAMBURA

OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


Na Boniface Wambura, Dar es salaam

Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 8:00 mchana

Viingilio kwa mechi ya Taifa Stars na Msumbiji itakayochezwa keshokutwa (Jumapili) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni sh. 7,000 na sh. 30,000 kwa viti maalumu 4,500 tu. 
Kuanzia kesho asubuhi (Jumamosi) tiketi za kielektroniki zitauzwa pia katika magari maalumu kwenye vituo vya Buguruni Shell, Dar Live Mbagala, Ferry Magogoni, Kigamboni, OilCom Chang’ombe, OilCom Ubungo, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa (Kariakoo), TCC Club Chang’ombe na Uwanja wa Taifa. 
Aidha tiketi zinapatikana kupitia M-PESA kwa kupiga *150*00# kisha bonyeza 4, bonyeza tena 4 kisha weka namba ya kampuni 173399 kisha ingiza 7000 kama namba ya kumbukumbu ya malipo, kisha andika tena 7000 kwenye weka kiasi, kasha weka namba ya siri na baadaye bonyeza  1 kukubali.
Utapokea ujumbe wenye orodha ya vituo vya MaxMalipo vya kuchukua tiketi ukiwa na namba ya uhakiki wa malipo yako.
Vituo vya MaxMalipo vya kuchukulia tiketi ni mgahawa wa Steers uliopo mtaa wa Samora/Ohio, maduka makubwa ya Uchumi Supermarket (Quality Centre, Tabata Segerea na kituo cha daladala Makumbusho), Sheer Illussions (Millennium Tower na Mlimani City), maduka makubwa ya TSN Supermarket (City Centre, Kibo Tegeta na Upanga). 

Vodashop (Ubungo na Mill Pamba), Shop Mwenge (Born to Shine), Puma Petrol Station (Mwenge na Uwanja wa Ndege), Engen Petrol Station (Mbezi Beach), Big Bon Petrol Station (Kariakoo, Sinza Mori, Mbagala na Temeke), YMCA (Posta Mpya), City Sports Lounge (Posta), Uwanja wa Taifa) na Uwanja wa Karume.


Straika wa Chelsea Demba Ba amefuzu upimwaji afya huko Besiktas na Ijumaa anatarajiwa kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 8.
Ba, mwenye Miaka 29, alianza Mechi 23 kati ya 50 alizochezea Chelsea Msimu uliopita na kufunga Bao 14.
Kwenye Msimu huo, Ba alikuwa nyuma kwa namba akiwa chaguo la mwisho baada ya Samuel Eto'o na Fernando Torres.
Lakini Eto’o hivi sasa amemaliza Mkataba na Chelsea wamemsaini Diego Costa na hivyo Ba kuonekana hahitaji tena.
*********

Beki mkongwe Rio Ferdinand anatarajiwa kukamilisha Uhamisho wake kwenda QPR kama Mchezaji Huru baada ya kufuzu upimwaji Afya yake.
Rio, mwenye Miaka 35, ni Mchezaji Huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Manchester United alikodumu kwa Miaka 12.
Huko QPR, Rio ataungana tena na Meneja Harry Redknapp ambae ndie alimwibua na kumpa namba kwa mara ya kwanza kama Mchezaji wa Kulipwa walipokuwa wote huko West Ham Mwaka 1996.

Rio anatarajiwa kuwa ndie Mchezaji wa Kwanza kusainiwa na QPR kwa ajili ya Msimu mpya.
Signed, sealed, delivered: Rio Ferdinand is officially a Queens Park Rangers playerRio akiwa amebeba jezi ya QPROn the dotted line: Ferdinand puts pen to paper with QPR on ThursdayRio akimwaga winoHoopla: The former England international puts his autograph on a QPR home strip


TONI Kroos amekamilisha uhamisho wa paundi milioni 24 kujiunga na Real Madrid kutokea kwa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.
Bayern walitangaza jana usubuhi kwamba klabu hizo mbili zimefikia makubaliano na uhamisho utafanyika mara moja.
Mkataba wa Kroos ilikuwa unamalizika majira ya kiangazi mwakani na mshindi huyo wa kombe la dunia amesaini mkataba wa miaka sita katika dimba la Santiago Bernabeu.
Kroos alitambulishwa rasmi jana na hapa chini ni baadhi ya picha zilizopigwa katika utambulisho wake ndani ya dimba la Bernabeu.
Delighted: Real Madrid president Florentino Perez unveils Toni Kroos following his move

Furaha: Rais wa Real Madrid,  Florentino Perez akimtambulisha Toni Kroos baada ya kukamilisha uhamisho.
Eye on the ball: Kroos does some kick-ups at the Santiago Bernabeu
Done deal: Kroos holds up his No 8 shirt at his unveiling in Madrid
Kroos atakayekuwa anavaa jezi namba 8 akionesha maujanja ta kuchezea gozi la ng`ombe ndani ya dimba la Bernabeu.
Dream move: Kroos was unveiled in glorious sunshine in Madrid
Golden boy: The former Bayern Munich man was integral during Germany's World Cup triumph
Wamepigwa chini: Manchester United walikuwa wakihusishwa kumsajili Kroos, lakini mwisho wa siku ni Real Madrid wamefanya yao.
Wanted: The German applauds the Madrid fans that attended his unveiling at the Santiago Bernabeu
Kroos akiwashukuru mashabiki wa Real Madrid waliohudhuria katika utambulisho wake ndani ya dimba la Santiago Bernabeu
Superstar: The World Cup-winning midfielder enjoys the adulation of Real Madrid's fans
Nyota: Mshindi wa kombe la dunia akifurahia na mashabiki wa timu yake mpya ya Real Madrid.
Great shakes: Toni Kroos (left) meets Real Madrid boss Carlo Ancelotti as he signs for the Spanish giamts
Karibu kijana: Toni Kroos (kushoto) akisalimiana na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti baada ya kusaini mkataba wake
Welcome aboard: Kroos is greeted by  Assistant coach Fernando Hierro
Karibu: Kroos akisalimiana na kocha msaidizi Fernando Hierro.


Mbwana Samatta akishangilia moja ya goli aliloifungia Taifa Stars mechi za nyuma
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 9:00 asubuhi
TAIFA Stars chini ya kocha, Mholanzi, Mart Nooij, inakabiliwa na mechi muhimu dhidi ya Msumbiji `Black Mambas` , kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kwenda kushiriki fainali za mataifa ya Afrika, AFCON , mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo ya kwanza itapigwa jumapili (julai 20 mwaka huu) ndani ya uwanja wa Taifa,  jijini Dar es salaam , ambapo Stars watalazimika kupata  ushindi wa mabao angalau 3-0 ili kujiweka mazingira mazuri ya kusonga mbele katika mechi ya marudiano itakayochezwa wiki mbili baadaye mjini Maputo nchini Msumbiji.
Kuelekea katika mechi hiyo ya jumapili, unaweza kusema kikosi cha Taifa Stars kipo kamili gado kwasababu nyota wake wote wa ndani na nje wapo tayari kwa kazi.
Mwinyi Kazimoto Mwitula alitua jana asubuhi akitokea nchini Qatar anakocheza soka la kulipwa tayari kwa kuongeza nguvu katika kikosi cha Stars.
Uzoefu wa Mwinyi katika soka la kimataifa utasaidia sana kuimarisha safu ya kiungo itakayomkosa Frank Domayo  `Chumvi` kwasababu ni majeruhi.
`Majembe` mawili ya Stars yanayokipiga TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu yapo nchini tangu juzi.
Kuelekea katika mechi hiyo, Mart Nooij ana wigo mpana wa kuamua nani aanze katika safu ya ushambuliaji.
Samatta amesema kwa upande wake, maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na amefurahi kwasababu ni mzima wa afya tofauti ni ilivyokuwa kwa mechi iliyopita mjini Harare nchini Zimbabwe.
“Maandilizi  kwa mimi kama mimi yako vizuri , kwasababu tulikuwa katika maandalizi ya ligi ya mabingwa, tulikuwa tunafanya mazoezi magumu. Kwahiyo maandalizi yako vizuri kwangu na kwa Thomas pia”. Alisema Samatta.
Thomas Emmanuel Ulimwengu
Ulimwengu kwa upande wake, kauli aliyoitoa jana jioni ni kwamba mechi ya jumapili itakuwa ngumu, lakini watajitahidi kupambana ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
“Maandilizi ni mazuri, tumefanya mazoezi, tunaamini tutafanya kazi nzuri. Mechi itakuwa ngumu, lakini tutafanikiwa kwa umoja”.
“Tutafanya kazi, tuwaombe watanzania waje kwa wingi uwanjani, ushindi wa pili ni kwa upande wao”. Alisema Ulimwengu.
Mshindi wa jumla kati ya Tanzania na Msumbiji atakata tiketi ya kupangwa katika hatua ya mwisho ya makundu kutafuta safari ya Morocco.
Tanzania iliitoa Zimbabwe kwa kuifunga bao 1-0 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kulazimisha sare ya mabao 2-2 mjini Harare.
Msumbiji wao waliifunga Sudan Kusini mabao 5-0 mjini Maputo na walipoenda ugenini walilazimisha suluhu ya bila kufungana.

Kila la kheri timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars kuelekea mechi muhimu na `Black Mambas`.

waliotembelea blog