Imechapishwa Julai 18, 2014, saa 8:32 mchana
Semina
elekezi ya michuano ya Airtel Rising Stars kwa mikoa sita inafanyika
kesho (Julai 19 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Washiriki
wa semina hiyo ni kutoka mikoa ya Mbeya (Katibu na mwakilishi wa
wanawake), Mwanza (Katibu na mwakilishi wa wanawake), Morogoro (Katibu),
Ilala (Katibu na mwakilishi wa wanawake).
Temeke
(Katibu na mwakilishi wa wanawake), Kinondoni (Katibu na mwakilishi wa
wanawake), Dar es Salaam (Mwenyekiti na Katibu), na Chama cha Mpira wa
Miguu Zanzibar (ZFA) kitakachowakilishwa na mwakilishi wa wanawake.
Washiriki
wengine katika semina hiyo ambayo mgeni rasmi atakuwa Katibu Mkuu wa
TFF, Mwesigwa Selestine ni wajumbe wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Vijana
ya TFF.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
0 maoni:
Post a Comment