TONI Kroos amekamilisha uhamisho wa paundi milioni 24 kujiunga na Real Madrid kutokea kwa mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich.
Bayern walitangaza jana usubuhi kwamba klabu hizo mbili zimefikia makubaliano na uhamisho utafanyika mara moja.
Mkataba wa Kroos ilikuwa unamalizika
majira ya kiangazi mwakani na mshindi huyo wa kombe la dunia amesaini
mkataba wa miaka sita katika dimba la Santiago Bernabeu.
Kroos alitambulishwa rasmi jana na hapa chini ni baadhi ya picha zilizopigwa katika utambulisho wake ndani ya dimba la Bernabeu.
Furaha: Rais wa Real Madrid, Florentino Perez akimtambulisha Toni Kroos baada ya kukamilisha uhamisho.
Kroos atakayekuwa anavaa jezi namba 8 akionesha maujanja ta kuchezea gozi la ng`ombe ndani ya dimba la Bernabeu.
Wamepigwa chini: Manchester United walikuwa wakihusishwa kumsajili Kroos, lakini mwisho wa siku ni Real Madrid wamefanya yao.
Kroos akiwashukuru mashabiki wa Real Madrid waliohudhuria katika utambulisho wake ndani ya dimba la Santiago Bernabeu
Nyota: Mshindi wa kombe la dunia akifurahia na mashabiki wa timu yake mpya ya Real Madrid.
Karibu kijana: Toni Kroos (kushoto) akisalimiana na kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti baada ya kusaini mkataba wake
Karibu: Kroos akisalimiana na kocha msaidizi Fernando Hierro.
0 maoni:
Post a Comment