Friday, July 18, 2014


Van Gaal was all smiles as he took his fist press conference as Manchester United manager
Van Gaal alikuwa na tabasamu kubwa wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari katika klabu ya Manchester United manager.

LOUIS van Gaal hataleta kombe la ligi kuu Manchester United katika msimu wake kwa kwanza, kwa mujibu wa kocha wa Queens Park Rangers, Harry Redknapp.
Redknapp, aliyekamilisha usajili wa beki wa zamani wa United, Rio Ferdinand jana alhamisi, haoni kama Mholanzi huyo atapata kombe bila kuwa na wachezaji wanne wa kiwango cha juu, achalia mbali  Luke Shaw na Ander Herrera waliosajiliwa.
'Van Gaal ana rekodi nzuri, lakini wanahitaji wachezaji," .Redknapp aliwaambia  talkSPORT.
The new United boss got to know his new surroundings with club legend Sir Bobby Charlton
Bosi mpya wa United alipata nafasi ya kujua mazingira ya klabu akiwa na gwiji wa klabu hiyo Sir Bobby Charlton.
"Anahitaji kuleta wachezaji angalau wanne au watano ili kurudi pale alipokuwa Alex (Ferguson), ambapo walishinda makombe".
"Kwa hatua hii kama ingekuwa ni kucheza kamari ya wao kushinda  ubingwa msimu ujao, nisingewapa nafasi ya kushinda, vinginevyo wanasajili wachezaji watatu au wanne wa kiwango cha juu".
Redknapp alitaja washindani wa ubingwa msimu ujao kuwa ni  Chelsea, Manchester City na Arsenal na kusema Man United watahangaika kufika juu baada ya kushuka wakati wa David Moyes.
Opinionated: The QPR manager spoke to the media on Friday morning
 Kocha wa QPR alizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi.
New signing: Rio Ferdinand (left) took part in his first training session with QPR on Friday morning
Jembe jipya: Rio Ferdinand (kushoto)  akishiriki mazoezi yake kwa mara ya kwanza leo asubuhi katika klabu ya  QPR 
"Sioni kama watakuwa imara kama Chelsea au Man City," aliongeza. "Nadhani Asernal wamefanya usajili mkubwa kwa kumleta Alexis Sanchez, kwahiyo msimu ujao wanaweza kuukaribia ubingwa zaidi".
"Bado ni wazi. Ningependa kuwaona Liverpool wanakuwa na msimu mzuri tena, lakini wamempoteza mchezaji wa ajabu (Luis Suarez). Hana mbadala kwakweli".
Catching up: Arsenal could play a big part in this season's title race after signing Chilean striker Alexis Sanchez from Barcelona
 Alexis Sanchez amesajiliwa na Asernal kutokea klabu ya Barcelona

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog