Friday, July 18, 2014


Straika wa Chelsea Demba Ba amefuzu upimwaji afya huko Besiktas na Ijumaa anatarajiwa kukamilisha Uhamisho wa Pauni Milioni 8.
Ba, mwenye Miaka 29, alianza Mechi 23 kati ya 50 alizochezea Chelsea Msimu uliopita na kufunga Bao 14.
Kwenye Msimu huo, Ba alikuwa nyuma kwa namba akiwa chaguo la mwisho baada ya Samuel Eto'o na Fernando Torres.
Lakini Eto’o hivi sasa amemaliza Mkataba na Chelsea wamemsaini Diego Costa na hivyo Ba kuonekana hahitaji tena.
*********

Beki mkongwe Rio Ferdinand anatarajiwa kukamilisha Uhamisho wake kwenda QPR kama Mchezaji Huru baada ya kufuzu upimwaji Afya yake.
Rio, mwenye Miaka 35, ni Mchezaji Huru baada ya kumaliza Mkataba wake na Manchester United alikodumu kwa Miaka 12.
Huko QPR, Rio ataungana tena na Meneja Harry Redknapp ambae ndie alimwibua na kumpa namba kwa mara ya kwanza kama Mchezaji wa Kulipwa walipokuwa wote huko West Ham Mwaka 1996.

Rio anatarajiwa kuwa ndie Mchezaji wa Kwanza kusainiwa na QPR kwa ajili ya Msimu mpya.
Signed, sealed, delivered: Rio Ferdinand is officially a Queens Park Rangers playerRio akiwa amebeba jezi ya QPROn the dotted line: Ferdinand puts pen to paper with QPR on ThursdayRio akimwaga winoHoopla: The former England international puts his autograph on a QPR home strip

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog