Friday, July 18, 2014

 Wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso akifuatiwa na  Meneja Masoko wa Airtel bi, Prisca Tembo ,na Mwenyekiti wa shirikisho la  wadau wa Utalii Tanzania Bwana Gaudence Temu , wakionyesha vifurushi vya bidhaa mpya ya Airtel Tourist Pack , wakati wa uzinduzi wa kifurushi hicho kitakacho wawezesha watalii kuwasiliana na familia zao mara wawapo nchi katika utalii, uzinduzi hu umefanyika leo katika makao makuu ya Airtel Daressalaam
 Mkurgenzi mtendaji wa Airtel Tanzania bw, Sunil Colaso akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kifurishi chenye vocha maalum na laini ya Airtel kwaajili ya watalii wanaoingia nchini kitakachojulikana kama Airtel Tourist pack, uzinduzi huo umefanyika leo  ambapo Watalii watakaofaidika ni wale wanaotoka Amerika, India, Italia na Uingereza kufaidika na 'Airtel Tourist pack'


*        Watalii toka Amerika, India, Italia na Uingereeza kufaidika na 'Airtel Tourist pack'
*        Airtel yapunguza gharama za kupiga simu na intaneti kwa watalii  toka Amerika, India, Italia na Uingereeza

Dar es Saalam, Juni 17, 2014, Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imekuja na ubunifu mpya wa bidhaa itakayojulikana kama AIRTEL TOURIST PACK maalum kwa wageni/watalii wanaotembelea nchini toka mataifa mbalimbali ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuendelea kutoa huduma bora ya mawasiliano nafuu kwa kuwaweza kuwasiliana na ndugu na familia zao wawapo kwenye utalii wao.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema" Huduma hii mpya ya "Vifurushi vya watalii" itapunguza usumbufu kwa mtalii/mgeni kukosa mawaliano bora ya simu au Intaneti awapo katika sehemu mbalimbali ya vivutio vya utalii nchini.

Ni imani yangu kuwa wageni watafurahia huduma hii kutokana na ubora wa mawasilano ya Airtel hasa katika maeneo ya pembezoni mwa miji ambako ndiko vivutio vingi vya utalii vinakopatika.

"Kifurushi hiki cha watalii kitakuwa na muda wa maongezi  wa dakika 30 za kupiga simu za nje, dakika 10 za kupiga simu za ndani ya nchi, SMS 10 kwenda mtandao wowote ndani na nje ya nchi pamoja na kifurushi cha intaneti cha 1GB vitakavyodumu kwa muda wa siku 30" alieleza Bw, Colaso

Kifurushi cha watalii Airtel Tourist Pack pia kinakuja na Laini ya simu na vocha ambapo, hii ni kwa yule mteja ambae hana laini ya Airtel au anataka kujiunga na kufaindika na huduma

Mtumiaji wa "Kifurushi cha watalii" Airtel Tourist pack atatakiwa kusajili namba yake pale tu anapofanya manunuzi kwa kutoa kitambulisho au pasi ya kusafiria.  Usaliji huo utakuwa wa muda kwa siku 30 na baada ya hapo mtalii atatakiwa kutoa kopi ya kitambulisho au pasi ya kusafiria kwaajili ya usajili wa kudumu.

Huduma hii ya vifurushi kwa wageni wakutoka nje ya nchi kwa simu ni ya kwanza kutoka Airtel na inampatia mteja uhuru wa kuwasilina  na ndugu jamaa na marafiki nyumbani kwa gharama nafuu zaidi kuliko ilivyokuwa awali, wateja watafurahia huduma za internet kwa kujiunga na mitandao ya kijamii, kutuma picha na video kwa gharama nafuu wakati wote . Aliongeza Colaso

Kwa upande wake mgeni rasmi, Mwenyekiti wa wadau wa Utalii nchini Bw, Gaudence Temu alisema "kwa niaba ya wadau wote wa utalii, ninaipongeza sana Airtel kwa kuanzisha huduma hii ya vifurushi vya mawasiliano kwa watalii wanaoingi nchini. Huduma hii inaendana na mahitaji ya wageni wetu na inakwenda sambamba na dhamira yetu sisi wadau ya kuendelea kutoa huduma bora katika soko.

"kwa kupitia mtandao wa Airtel ulioenea zaidi maeneo ya vijijini wageni wetu sasa watakuwa na uhakika wa mawasiliano bora na kwa gharama nafuu wakati wote" alieleza Bw, Temu

Mwenyekiti huyo pia alitoa ushauri kwa wadau wote wa biashara ya utalii kuchangamkia fulsa hiyo kwa kuwajulisha wageni wanaoingia nchini ili waweze kufaidika na punguzo hilo ambalo kwa msimu huu wa utalii hutumia gharama kubwa katika mawasiliano.

"Migahawa na Hoteli, wadau wa usafirishaji, watembezaji watalii na wadau wote hii ni fulsa kwetu kuwapa habari njema wateja wetu wanapoingia nchini kwamba kuna Tourist pak yenye faida zote hizi" alimaliza kwa kusema Bw, Temu

Vifurushi vya watalii zitapatikana katika maeneo yote ya biashara katika maeneo ya kuingia nchini kama zile viwanja vya ndege vya Dar es saalam(JKIA), Zanzibar, Arusha na KIA. Pia zinapatikana katika hoteli na migahawa ya kitalii.

Nchi zitakazofaidika na huduma hii kwa sasa ni pamoja na Amerika, India, Italia na Uingereeza

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog