Friday, December 18, 2015


Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays Tanzania, Valence Luteganya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua kampeni ya matumizi ya Kadi za VISA za benki ya Barclays kwaajili ya wateja wake. Pia Lutenganya amesema kuwa kampeni hii itadumu kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Desemba 17 mwaka huu hadi Februari 28, 2016. Kampeni hii itamwezesha mteja kunufaika na mafao mbalimbali yanayohusiana na malipo kabla na baada ya kutumia kadi zao za Visa. Wateja wenye kazi hizo wanaweza kunywa na kula kwa bei ya punguzo kwenye toteli zilizopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera.
Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwamfwagasi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua kampeni ya matumizi ya Kadi zake za VISA kwaajili ya wateja wa benki hiyo. Pia amesema kuwa punguzo la bei itakuwa katika hoteli ya Southen Sun na Double Tree by Hilton, ambapo huduma za kadi za VISA za benki hiyo, wateja wenye kazi hizo watapata ofa kwa huduma yeyote kwa punguzo la 10% katika huduma za maeneo tofauti tofauti kama hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam, Double Tree by Hilton Zanzibar Nungwi, Double Tree by Hilton Stone Town- Zanzibar, Bayt El Salaam-Ston Town Zanzibar na Hoteli ya Southern Sun- Dar es Salaam kwa punguzo la 20% mpaka 30%.

Wateja wanaweza kazi zao za Barclays kwaajili ya malipo ya huduma malimbali katika maduka ya ndani ya nchi na Nje ya nchi na kutoa pesa kwenye ATM za ndani na nje ya nchi.Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera, Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays Tanzania, Valence Luteganya na Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays, Erica Mwaipopo.

Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera, Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays Tanzania, Valence Luteganya, Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwamfwagasi na Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays, Erica Mwaipopo wakionyesha kadi za VISA za benki ya Barclays mara baada ya kuzindua kaDi hizo jijini Dar es Salaam leo.


Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa na kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya Halmashauri tano za Mkoa wa Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka huu.

   

Taarifa ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10 vilivyoshindanishwa, kuwa ni pamoja na miradi yenye maslahi kwa umma iliyozinduliwa wakati wa mbio za mwenge wa uhuru, uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na vijana.


Vigezo vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa za kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya mwenge wenyewe ulipowasili wilayani Mufindi


Akizungumzia ushindi huo, Mkuu wa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao na akatoa rai ya kundelea kuuenzi mewenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.


Aidha, taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza kimkoa, ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36 pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.



Wanamuziki nyota wa bongo fleva nchini, Estelina Peter Sanga maarufu kwa jina la Linah Sanga na Feza Kessy  ijumaa watapanda jukwaa moja na nyota kibao wa Nigeria katika tamasha kubwa la mwaka la muziki lijulikanalo kwa jina la Soundcity Urban Festival.

Tamasha hilo pia litawashirikisha wasanii nyota wa Nigeria kama, Davido, Kiss Daniel, Iyanya na  Olamide. Katika orodha hiyo wapo wasanii nyota wengine kama  Victoria Kimani, Runtown, Sound Sultan, Lil Kesh, Ycee, Sean Tizzle na Phyno.

Wanamuziki hao waliondoka nchini Jumatano usiku chini ya Doreen Noni ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni mpya ya kusimamia wanamuziki nchini, Panamusiq Limited.



Doreen alisema kuwa kampuni yao ndiyo iliyowawezesha wanamuziki hao kuweka historia kwa kuwa wanamuziki wa kwanza nchini kushiriki katika tamasha hilo kubwa la muziki litakalofanyika mjini Lagos.

 Alisema kuwa Panamusiq Limited imepanua wigo wa shughuli zake na kwa sasa inafanya kazi na kampuni nyingi maarufu duniani zinazojishughulisha na masuala ya muziki.

“Tumejiandaa kufanya kweli katika tamasha hilo, Linah na Feza walikuwa katika mazoezi makali ya kuimba, kucheza hasa kwa kutawala jukwaa, lengo ni kuacha historia katika tamasha hilo,” alisema Doreen.

 Doreen alisema kuwa  kampuni yao yenye maskani yake Kinondoni jijini, imepania kuwatambulisha wasanii kimataifa pamoja na kuwaongezea kipato kutokana na kazi zao.

“Linah na Feza ni miongoni tu mwa wasanii ambao wapo chini ya kampuni yetu ambayo lengo lake kubwa ni kuwaendeleza na kufaidika kupitia kazi zao, najua kuna wanamuziki wengi sana hapa nchini, wachache sana ndiyo wapo kimataifa zaidi, sisi tunataka wafikie mamia na kupanua soko lao,” alisema Doreen.


Diamond akipiga kinanda huku akimuimbia mpenzi wake Zari.
  Nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kasimama mbele ya magari aliyoyatumia katika video yake mpya ya Utanipenda.Staa wa Bongo, Jacqueline Wolper, akiongea jambo na Diamond.
Gari ya Wolper katika video hiyo ikimmwagia maji Diamond.

Diamond akiangalia vipande vya video hivyo kabla ya kuendelea kushuti.Diamond akiangalia Magazeti Pendwa baada ya kupata matatizo, nayo hayakuwa nyuma kuandika.
Mama yake Diamond, Sanura Kasim (kushoto) akifukuzwa na mlinzi baada ya kwenda kuomba msaada kwa JK.
Diamond akiongea jambo.Diamond akiwa kapozi na mpenzi wake Zari.

Sasa hivi kwenye ulimwengu wa muziki, gumzo ni ngoma aliyoitoa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la Utanipenda. Ni ngoma kali ambayo itatambulishwa kwa mara ya kwanza ndani ya Ukumbi wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar.

Mbali na utambulisho wa ngoma hii ambayo itapigwa live kwa kutumia vyombo, nyimbo nyingine ambazo Diamond atazipiga siku hiyo ni pamoja na Mdogomdogo, Nasema Nawe, Nana na nyinginezo zinazobamba huku akiwa na madansa wake kutoka Wasafi Classic Baby (WCB). Itakuwa ni siku ya Krismasi (Ijumaaa ijayo) ambayo msanii huyo ameahidi kufanya mambo makubwa akisindikizwa na mkali wa nyimbo za Singeli, Msaga Sumu pamoja na wacheza dansi hatari Afrika Mashariki, Wakali Dancers na wasanii wengine kibao. 

Burudani yote hiyo ambayo imedhaminiwa na huduma kutoka kampuni ya simu Tanzania, Airtel Money utaipata kwa kiingilio cha shilingi 15,000 tu getini na wale watakaohitaji huduma ya VIP watalipia shilingi 30,000. Katika kuelekea kwenye shoo hiyo, Showbiz ilifanikiwa kunasa baadhi ya picha za nyuma ya pazia ‘behind the scene’ wakati kichupa cha wimbo huo kikiandaliwa. 

Video hiyo ni mkono wa yuleyule mkali wa vichupa kutoa Sauzi anayekwenda kwa jina la God Father. Hajakosea! Amefanya bonge la kazi na hata mashabiki ni mashahidi kwamba wimbo ni mkali na kideo chenyewe ni ‘kitamu’. Maneno mengi siyo ishu, kwenye hili picha zinaongea zaidi hivyo pitisha macho kwenye baadhi ya picha hizo ili upate uhondo! Kwani kuna mtu kaibiwa?

waliotembelea blog