Meneja
wa bidhaa wa benki ya Barclays Tanzania, Valence Luteganya akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kuzindua
kampeni ya matumizi ya Kadi za VISA za benki ya Barclays kwaajili ya
wateja wake. Pia Lutenganya amesema kuwa kampeni hii itadumu kwa muda wa
miezi mitatu kuanzia Desemba 17 mwaka huu hadi Februari 28, 2016.
Kampeni hii itamwezesha mteja kunufaika na mafao mbalimbali
yanayohusiana na malipo kabla na baada ya kutumia kadi zao za Visa.
Wateja wenye kazi hizo wanaweza kunywa na kula kwa bei ya punguzo kwenye
toteli zilizopo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa kitengo
cha Masoko wa benki ya Barclays, Joe Bendera.
Mkuu
wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar Mwamfwagasi
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa
kuzindua kampeni ya matumizi ya Kadi zake za VISA kwaajili ya wateja wa
benki hiyo. Pia amesema kuwa punguzo la bei itakuwa katika hoteli ya
Southen Sun na Double Tree by Hilton, ambapo huduma za kadi za VISA za
benki hiyo, wateja wenye kazi hizo watapata ofa kwa
huduma yeyote kwa punguzo la 10% katika huduma za maeneo tofauti
tofauti kama hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam,
Double Tree by Hilton Zanzibar Nungwi, Double Tree by Hilton Stone Town-
Zanzibar, Bayt El Salaam-Ston Town Zanzibar na Hoteli ya Southern Sun-
Dar es Salaam kwa punguzo la 20% mpaka 30%.
Wateja
wanaweza kazi zao za Barclays kwaajili ya malipo ya huduma malimbali
katika maduka ya ndani ya nchi na Nje ya nchi na kutoa pesa kwenye ATM
za ndani na nje ya nchi.Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko
wa benki ya Barclays, Joe Bendera, Meneja wa bidhaa wa benki ya
Barclays Tanzania, Valence Luteganya na Meneja wa bidhaa wa benki ya
Barclays, Erica Mwaipopo.
Kutoka
kulia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Masoko wa benki ya Barclays, Joe
Bendera, Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays Tanzania, Valence
Luteganya, Mkuu wa kitengo cha Bidhaa katika benki ya Barclays, Oscar
Mwamfwagasi na Meneja wa bidhaa wa benki ya Barclays, Erica Mwaipopo
wakionyesha kadi za VISA za benki ya Barclays mara baada ya kuzindua
kaDi hizo jijini Dar es Salaam leo.
0 maoni:
Post a Comment