Halmashauri
ya Wilaya ya Mufindi ya Mkoani Iringa imeibuka mshindi wa kwanza kimkoa na
kushika nafasi za juu kikanda na kitaifa, kati ya Halmashauri tano za Mkoa wa
Iringa, baada ya kufanya vizuri zaidi wakati wa mbio za mwenge wa uhuru
ulipokimbishwa Mkoani Iringa mnamo mwezi Juni mwaka huu.
Taarifa
ya kitengo cha habari na mawasiliano cha Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
imevitaja baadhi ya vigezo kati ya vigezo 10 vilivyoshindanishwa, kuwa
ni pamoja na miradi yenye maslahi kwa umma iliyozinduliwa wakati wa mbio za
mwenge wa uhuru, uimarishaji wa vikundi vya uzalishaji mali kwa wanawake na
vijana.
Vigezo
vingine vinavyozingatiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya Malaria, dawa za
kulevya, michango ya Mwenge wa uhuru sanjari na mapokezi ya mwenge wenyewe
ulipowasili wilayani Mufindi
Akizungumzia
ushindi huo, Mkuu wa wilaya ya Mufindi JOWIKA KASUNGA amewashukuru wakazi
wa Mufindi na wadau wa maendeleo kwa michango yao na akatoa rai ya kundelea
kuuenzi mewenge wa uhuru kama alama na utambulisho wa taifa.
Aidha,
taarifa hiyo imezitaja nafasi ilizoshika kuwa ni ushindi wa kwanza kimkoa,
ushindi wa 05 kwa kanda ya kiuchumi yenye zaidi Halmashauri 36
pamoja na nafasi ya 22 kitaifa ikijumuisha zaidi ya Halmashauri 140.
0 maoni:
Post a Comment