Saturday, May 2, 2015


Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mheshimiwa Diodorus Kamala[l] akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wageni waalikwa kutoka mataifa mbalimbali katika uzinduzi wa filamu za kitanzania ambazo sasa zitakuwa zikiuzwa online.sherehe hizo za uzinduzi ambazo zilifanyika jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Proin Group Tanzania ndugu Johson Lukaza akizungumza machache na kuwashukuru watu wote waliohudhuria uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online hapo jana katika ukumbi wa ACP House jijini Brussel nchini Ubelgiji na kuudhuriwa na watu wa mataifa mbalimbali.Uzinduzi huo ulifanywa na balozi wa Tanzania Mheshimiwa Diodorus Kamala.
Dr.Pendo akifanya mahojiano machache na Mheshimiwa Emmanuel kuhusiana na Filamu za kitanzania ambazo zitakuwa ziliuzwa mitandaoni pipote duniani.
Mwenyekiti wa Proin Promotion Tanzania ndugu Johson Lukaza [r] akiwa na viongozi wa Kitanzania nchi Ubelgiji katika sherehe za uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania onlione.
Kiongozi wa watanzania nchini Ubelgiji bwana Macha[r] akiwa na kiongozi wa watanzania jijini Antwerpen kwenye uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online popote duniani
Mwenyekiti wa Proin Promotion bwana Johnson Lukaza [l] akiwa na mmoja wa wageni waalikwa katika uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online jijini Brussel nchini Ubelgiji hapo jana.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji,Mheshimiwa Dr.Kamala akibadilishana mawazo na wageni wake mara tu baada ya uzinduzi wa manunuzi ya filamu za kitanzania online duniani kote.Balozi ni mmoja wa washiriki waliofanikisha shughuli nzima ya uzinduzi huo.
Warembo kutoka mataifa mbalimbali walikuwepo kwenye uzinduzi huo hapo jana.kwa manunuzi ya filamu zote za kitanzania sasa waweza kununua popote pale duniani kwa kutembelea website hii ya www.proinpromotions.co.tz 
Pendelea vya kwenu kwa kununua vyenu,sheme  Watanzania,Warundi,Wanyarwanda,Wakongo,Wazambia,Waganda,Wakenya na waafrika woote tunaomba ushirikiano wenu kwa kununua filamu zetu sasa.

Wafanyakazi wa Shirika la Umeme(TANESCO) mkoa wa Kilimanjaro wakipita na gari lao mbele ya mgeni rasmi katika sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu chaUshirika  mjini Moshi. 
Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCLwakipita katikamaonesho ya Mei Mosi

 Watangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Powerbreakfast Gerald Hando pamoja na Hudson Kamoga wa Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wakifanya mahojiano na Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na kwingineko Diamond Platnum akiwa na mchumba wake Zari the bosslady,kuhusiana na mambo mbalimbali yakiwemo ya maisha yao na pia kuhusu onesho lao la Zari White Party wanalotarajia kulifanya usiku wa leo pale Mliman City,Jijini Dar.

Onesho hilo ambalo lilizua gumzo kila kona ya jiji la Dar likijulikana kwa jina la The White Party leo ndio kilele chake,kiingilio chake ukikisikia lazima usisimke,Kiingilio cha Onesho hilo kimevunja rekodi,haijawahi kutokea,kwa maana ya kwamba kiingilio kimepangwa kwa madaraja kuanzia Elfu hamsini,laki moja,milioni moja na milioni tatu,na huwezi amini tiketi sold out kitambo,imagine.

Katika mahojiano hayo Zari alieleza kuwa amefurahi kuonana na mtu kama Diamond,kijana anaejiamini,anaejituma na ni msanii anaefanya kazi zake kwa kujituma na juhudi kubwa,mwenye upendo na mapenzi ya kweli kutoka moyoni,alisema Zari huku akitoa tabasamu laini na kuongeza kuwa hajutii kumpata Diamond katika maisha yake.
Kwa upande wake Diamond nae alikiri wazi kumpenda Zari katika nyanja zote,amesema kwa sasa amekuwa na furaha kila wakati, kwa kuwa hivi karibuni anatarajia kupata mtoto wa kike kutoka kwa mchumba wake Zari. 
 Mtangazaji wa Clouds 360 Hudson Kamoga akimuuliza swali Bi.Zari ambae ni Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na kwingineko. 
 Diamond akirekebisha jambo kwa mpenzi wake
 Ooh..relax baby.
 Ooh Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha Zari The Bosslady kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia Clouds FM na Clouds TV.
 Ooh Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha Zari The Ladyboss kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia Clouds FM na Clouds TV.
 Diamond akifafanua jambo.
 Kicheko kwa mbaaali
 Zari the bosslady katika ubora wake wa pozi.

waliotembelea blog