Watangazaji
wa Clouds FM kupitia kipindi cha Powerbreakfast Gerald Hando pamoja na
Hudson Kamoga wa Clouds TV kupitia kipindi cha Clouds 360 wakifanya
mahojiano na Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini na
kwingineko Diamond Platnum akiwa na mchumba wake Zari the
bosslady,kuhusiana na mambo mbalimbali yakiwemo ya maisha yao na pia
kuhusu onesho lao la Zari White Party wanalotarajia kulifanya usiku wa leo pale Mliman City,Jijini Dar.
Onesho
hilo ambalo lilizua gumzo kila kona ya jiji la Dar likijulikana kwa
jina la The White Party leo ndio kilele chake,kiingilio chake ukikisikia
lazima usisimke,Kiingilio cha Onesho hilo kimevunja rekodi,haijawahi
kutokea,kwa maana ya kwamba kiingilio kimepangwa kwa madaraja kuanzia
Elfu hamsini,laki moja,milioni moja na milioni tatu,na huwezi amini
tiketi sold out kitambo,imagine.
Katika
mahojiano hayo Zari alieleza kuwa amefurahi kuonana na mtu kama
Diamond,kijana anaejiamini,anaejituma na ni msanii anaefanya kazi zake
kwa kujituma na juhudi kubwa,mwenye upendo na mapenzi ya kweli kutoka
moyoni,alisema Zari huku akitoa tabasamu laini na kuongeza kuwa hajutii
kumpata Diamond katika maisha yake.
Kwa
upande wake Diamond nae alikiri wazi kumpenda Zari katika nyanja
zote,amesema kwa sasa amekuwa na furaha kila wakati, kwa kuwa hivi
karibuni anatarajia kupata mtoto wa kike kutoka kwa mchumba wake Zari.
Mtangazaji
wa Clouds 360 Hudson Kamoga akimuuliza swali Bi.Zari ambae ni
Mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki na kwingineko.
Diamond akirekebisha jambo kwa mpenzi wake
Ooh..relax baby.
Ooh
Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa
Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha
Zari The Bosslady kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia
Clouds FM na Clouds TV.
Ooh
Shemejiiii......karibu..karibu Clouds FM/Clouds TV...! Mtangazaji wa
Clouds FM kupitia kipindi cha Power breakfast,Gerald Hando akimkaribisha
Zari The Ladyboss kabla ya kuanza mahojiano ya moja kwa moja kupitia
Clouds FM na Clouds TV.
Diamond akifafanua jambo.
Kicheko kwa mbaaali
Zari the bosslady katika ubora wake wa pozi.
0 maoni:
Post a Comment