Monday, July 28, 2014

Liverpool imemsaini Beki wa Southampton Dejan Lovren kwa Dili inayoaminika ni Pauni Milioni 20 na huyo ni Mchezaji wao wa 5 kumnunua kwa ajili ya Msimu mpya.
Lovren, mwenye Miaka 25, ni Sentahafu kutoka Croatia na amesaini Mkataba wa Miaka Minne.
Lovren anaungana na Wachezaji wengine wawili waliotoka Southampton na kuhamia Liverpool katika kipindi hiki ambao ni Rickie Lambert na Adam Lallana.

Meneja Brendan Rodgers amesema usajili huu wa Mchezaji huyo ni muhimu mno kwao na Lovren atasafiri moja kwa moja kwenda Marekani kujiunga na Liverpool ambayo inashiriki Mashindano ya International Champions Cup.
Lovren alijiunga na Southampton kutoka Lyon Mwaka Jana kwa Dau la Pauni Milioni 8.5 na anaondoka Klabu hiyo akiwa amebakisha Miaka Mitatu kwenye Mkataba wake.

Hadi sasa Southampton, kwenye Kipindi hiki cha Uhamisho, imeshawauza Wachezaji Watano kwa Jumla ya Pauni Milioni 92.Wachezaji wengine walioondoka Klabu hiyo ni Luke Shaw aliekwenda Man United, Calum Chambers anaekwenda Arsenal, na wawili waliohamia Liverpool, Rickie Lambert na Adam Lallana.


Dejan Loven amesaini kwenda Liverpool kwa pauni £20m kutoka  Southampton

 Lovren sasa ni Beki wao mpya na hatari

Lovren anatarajiwa kujiunga na Wachezaji wa Liverpool kwenye Ziara kujiandaa na Msimu mpya wa 2014/15 unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Watano walionunuliwa na Liverpool:
-Straika: Rickie Lambert, Miaka 32, Pauni Milioni 4 kutoka Southampton
-Kiungo: Adam Lallana, Miaka 25, Pauni Milioni 25 kutoka Southampton
-Kiungo: Emre Can, Miaka 20, Pauni Milioni10 kutoka Bayer Leverkusen
-Winga: Lazar Markovic, Miaka 20, Pauni Milioni 20 kutoka Benfica
-Beki: Dejan Lovren, Miaka 25, Pauni Milioni 20 kutoka Southampton

 
index
*Msafiri Diouf, Amigolas wa Bendi ya Ruvu Stars kupamba shindano
Na Mwandishi Wetu
Wakati warembo 14 wanaowania taji la Kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014)  (kesho Jumanne)  watashindana kwenye taji la vipaji (talent award), bendi mpya inayokuja juu kwa kasi, Ruvu Stars chini ya nyota Msafiri Diouf na Hamis Amigolas watapamba shindano hilo lililopangwa kufanyika  kwenye ukumbi wa Maisha Plus, Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Akizungumza jijini jana, mratibu wa mashindano hayo, Alex Nikitas alisema kuwa awali walipanga kufanya shindano hilo siku ya Idd Pili, lakini kutokana na muda wameamua kulifanya leo ili kuwapa muda zaidi warembo kwa ajili ya mazoezi ya kuwania taji la mrembo wa Kanda ya Mashariki Agosti 8 kwenye hotel ya Nashera mkoani  Morogoro.
Nikitas alisema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na onyesho litaanza saa 2.00 usiku huku warembo wakichuano katika vipaji mbalimbali kama kuimba, kucheza muziki wa kisasa, wa asili na ya nje ya nchi. Alisema kuwa mgeni rasmi katika shindano hilo ni Mbunge wa Kibaha mjini, Silvester Koka.
“Warembo wapo katika maandalizi makali  tayari kuchuana katika mashindano hayo, mbali ya vipaji, pia warembo hao watatoa misaada mbalimbali kwa vituo vya watoto yatima katika mkoa huo,” alisema Nikitas.
Alisema kuwa warembo hao wataondoka mkoa wa Pwani Julai 31 tayari kwa kambi ya mwisho kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya mashariki wa mwaka jana,  Diana Laizer.

waliotembelea blog