*Msafiri Diouf, Amigolas wa Bendi ya Ruvu Stars kupamba shindano
Na Mwandishi Wetu
Wakati
warembo 14 wanaowania taji la Kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern
Zone 2014) (kesho Jumanne) watashindana kwenye taji la vipaji (talent
award), bendi mpya inayokuja juu kwa kasi, Ruvu Stars chini ya nyota
Msafiri Diouf na Hamis Amigolas watapamba shindano hilo lililopangwa
kufanyika kwenye ukumbi wa Maisha Plus, Kibaha, Mkoa wa Pwani.
Akizungumza
jijini jana, mratibu wa mashindano hayo, Alex Nikitas alisema kuwa
awali walipanga kufanya shindano hilo siku ya Idd Pili, lakini kutokana
na muda wameamua kulifanya leo ili kuwapa muda zaidi warembo kwa ajili
ya mazoezi ya kuwania taji la mrembo wa Kanda ya Mashariki Agosti 8
kwenye hotel ya Nashera mkoani Morogoro.
Nikitas
alisema maandalizi ya shindano hilo yamekamilika na onyesho litaanza
saa 2.00 usiku huku warembo wakichuano katika vipaji mbalimbali kama
kuimba, kucheza muziki wa kisasa, wa asili na ya nje ya nchi. Alisema
kuwa mgeni rasmi katika shindano hilo ni Mbunge wa Kibaha mjini,
Silvester Koka.
“Warembo
wapo katika maandalizi makali tayari kuchuana katika mashindano hayo,
mbali ya vipaji, pia warembo hao watatoa misaada mbalimbali kwa vituo
vya watoto yatima katika mkoa huo,” alisema Nikitas.
Alisema
kuwa warembo hao wataondoka mkoa wa Pwani Julai 31 tayari kwa kambi ya
mwisho kwenye hotel ya Usambara Safari Lodge chini ya Miss Kanda ya
mashariki wa mwaka jana, Diana Laizer.
0 maoni:
Post a Comment