Zinaitwa
African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014 zimetolewa huko
Eisemann Center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa mbalimbali
akiwemo Diamond wa Tanzania ambaye pia alikua mmoja wa wanaowania tuzo
hizo
Habari njema za ushindi wote huu
ni kwa mujibu wa meneja wake Babu Tale ambaye nae kahudhuria tuzo hizi
Marekani ala ametuma ujumbe mfupi wa simu akisema Diamond ameshinda
tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo
bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa
Nigeria.
Kolabo bora ni tuzo iliyokua
inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na
Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya
Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj
Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume
Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol
kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na
Jackie Gosee wa Ethiopia.
lady
Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua
anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya,
Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka tuzo yake
imechukuliwa na Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana na Don Jazzy
wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South
Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo ya Mtayarishaji bora wa video
imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya
‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
0 maoni:
Post a Comment