Afisa Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba akitoka
kukagua jukwaa lenye hadhi ya kimataifa la Ebony FM kwenye uzinduzi wa
kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika jana kwenye viunga vya Samora mkoani
Iringa.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Baadhi
ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Tosamaganga wakiwasili kwenye
viwanja vya Samora mjini Iringa kushuhudia uzinduzi wa kampeni ya SHUGA
Redio inayowalenga vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 iliyozinduliwa
rasmi jana mkoani humo.
Wanafunzi
kutoka shule mbalimbali za Sekondari wakiwemo Shule ya wasichana Iringa
wakiendelea kumiminika kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
Stella
Shubi kutoka Clouds Media (kulia) akibadilishana mawazo na Afisa
Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumba kabla ya kuanza kwa
sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika kwenye viwanja
Samora mjini Iringa.
MC
wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio B 12 kutoka Clouds FM Redio ambao
ndio waratibu wa uzinduzi wa kampeni hiyo akiwa na mtoto aliyeashangaza
umati wa vijana waliofurika kwenye uzinduzi huo baada ya kujibu swali
ambalo hawakutegemea angelijibu kutokana na umri wake.
Meza
Kuu, Kutoka kulia ni Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt.
Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kamishna wa
TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja
K. Nyalandu pamoja na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose
Haji Mwalimu.
Baadhi
ya Mameneja wa Redio 10 za Jamii zitakazokuwa zikirusha vipindi vya
SHUGA Redio vitakavyoanza kurushwa rasmi tarehe 2 Agosti mwaka huu
wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jana kwenye viwanja
vya Samora mjini Iringa.
Kikundi
cha Wazalendo a.k.a Makhirikhiri wa Bongo kutoka Mtwivila Iringa
wakitoa burudani kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio uliofanyika
jana kwenye viwanja vya Samora mjini Iringa.
Mohamed
Omari kwa jina la usanii Sam wa Wazalendo Group kutoka mjini Iringa
akito burudani za nyimbo za Makhirikhiri kwa staili ya aina yake huku
akiwa na Nyoka mdomo kwenye sherehe za uzinduzi huo.
Mwanafunzi
Calist Hermet wa kidato cha Sita kutoka shule ya Sekondari Tosamaganga
akiimba wimbo wenye kuhamasisha matumizi ya Kondomu na upimaji wa Virusi
vya Ukimwi kwa vijana huku akipewa sapoti na baadhi ya wanafunzi
wenzake katika sherehe za uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
Kutoka
kushoto B Dozen a.k.a B12, Shadee pamoja na Stella Shubi wakiwakilisha
Clouds FM Redio ikiwa ni miongoni mwa Redio zitakazokuwa zikirusha
vipindi vya kampeni ya SHUGA Redio kupitia kipindi cha Bongo Fleva
kinachopendwa kusikilizwa na vijana wengi katika Redio hiyo.
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu
(kushoto) na Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison
Jenkins wakifuatilia burudani mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye
uzinduzi huo.
Afisa
Programu kutoka UNESCO, Courtney Ivins (kushoto) na Mratibu na Mkufunzi
wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu wakiwa kwenye
jukwaa kuu ndani ya viwanja vya Samora mjini Iringa.
Mwanadada Shadee kutoka CLOUDS Media akipata picha ya kumbukumbu na Mwanafunzi Calist Hermet wa shule ya Sekondari Tosamaganga.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi na mashirika mbalimbali walijumuika kwenye uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
Pichani
juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari
mkoani Iringa waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio.
Mgeni
rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni
Mkuu wa Wilaya ya Iringa akizindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio ambapo
amewaasa Vijana kuzingatia matumizi sahihi ya Kondomu na upimaji wa VVU
ili kuzitambua afya zao mapema na kuepukana na maambukizi mapya ya VVU.
Mkuu
wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins
akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amesema Lengo kuu la kampeni ni
kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU
miongoni mwa vijana wa umri wa kubalehe kupitia vyombo vya habari na
kuwafikia kwa ujumbe mahususi kuhusu upimaji wa hiari na ushauri nasaha
na ngono salama. Kampeni inakusudiwa kuchochea vijana walioko kwenye
hatari kubwa ya kupata maambukizi waweze kutafuta na kuziendea huduma
zilizopo.
Bi.
Jenkins aliongeza kuwa kutakuwa na mfululizo wa vipindi 12 vya kuigiza
wenye muda wa dakika nane umeelezea maisha ya vijana wanne (Sofia,
Fally, Amina na Kavis) kuwakilisha vijana wa umri wa miaka 15 – 24.
Simulizi iliyopo inahusu ndoto, chaguzi, marafiki, mapambano ya
changamoto za kimaisha katika Dunia, ambayo UKIMWI ni tishio
kubwa.Simulizi hizi kwa ujumla wake zinajikita kwenye somo la mbinu za
upimaji wa VVU na ushauri nasaha, matumizi ya kondomu katika mahusiano
ya muda mrefu , Kinga, unyanyasaji wa kijinsia na kingono, unywaji pombe
na athari za kuwa na wapenzi wengi zinazopelekea kupata maambukizi ya
UKIMWI.
Mgeni rasmi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Leticia Warioba ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa akimpongeza Mkuu wa kitengo cha watoto na Ukimwi kutoka UNICEF, Alison Jenkins (kulia) kwa risala nzuri wakati wa uzinduzi huo. Kushoto ni Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu.
Mratibu
wa TACAIDS Mkoa wa Iringa, Bw. Owen Wimbo miongoni mwa wadhamini wa
kampeni hiyo akizungumza machache na wakazi wa Iringa, Vijana na wageni
waalikwa waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio
iliyozinduliwa rasmi jana kwenye viwanja vya Samora mkoani Iringa.
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu,
akizungumza na vijana waliohudhuria uzinduzi huo ambapo aliwaasa
kutouza mechi kusubiri muda muafaka na kuzingatia zaidi masomo sanjari
na kuepuka kufanya ngono zembe.
Kamishna wa TACAIDS na Balozi wa Vijana (UNICEF) na Kampeni ya SHUGA Redio, Faraja K. Nyalandu akisikiliza
majibu kuhusu elimu ya afya ya uzazi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule za
sekondari mkoani Iirnga waliopata nafasi ya kuhudhuria uzinduzi huo.
Mgeni rasmi akiwa ameungana na wasanii wa Bongo Flava pamoja na meza kuu kwa ajili ya kuzindua rasmi kampeni ya SHUGA Redio.
Sasa imezinduliwa rasmi…..!
Baadhi
ya wanafunzi wa shule mbalimbali za Sekondari mkoani Iringa wakitumia
mbio kutoka kwenye majukwaa yao kusogea uwanja kushuhudia burudani za
wasanii wa Bongo Flava Izo Business na Ben Paul waliopamba uzinduzi wa
mradi huo jana mkoani Iringa.
Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva nchini Ben Paul akitoa burudani ya aina yake
iliyoambatana na ujumbe mahususi wa kuhamasisha vijana kupima afya zao
wakati wa uzinduzi wa kampeni ya SHUGA Redio ulioanyika jana mkoani
Iringa kwenye viwanja vya Samora.
Umati
wa vijana na wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari Iringa
wakishuhudia burudani za wasanii maarufu wa Bongo Flava waliosinfdikiza
uzinduzi huo.
Pichani
juu na chini ni msanii wa muziki wa Hip Hop nchini anayejulikana kama
Izo Business akitoa burudani kwa Vijana na wageni mbalimbali
waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni ya SHUGA Redio iliyozinduliwa rasmi
jana mkoani Iringa kwenye viwanja vya Samora.
George
Magesa kutoka UNICEF (katikati) akipata ukodak na Msanii wa Bongo Fleva
nchini Ben Paul pamoja na Mtangazaji wa Clouds FM Redio B Dozen a.k.a B
12.
Baadhi
ya wanafunzi wa Kituo cha Upendo mjini Iringa wakiwa kwenye foleni ya
kuingia kwenye chumba maalum kwa ajili kupima Virusi vya Ukimwi bure
wakati wa sherehe za uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Radio uliofanyika kwenye
viwanja vya Samora mjini Iringa.
Mtaalamu
kutoka AMREF akichukua vipimo vya damu kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa
kituo cha Upendo mjini Iringa aliyejitolea kupima kwa hiari Virusi vya
Ukimwi wakati wa uzinduzi wa Mradi wa SHUGA Redio unaotekelezwa kwa
ushirikiano wa Mashirika ya Kimataifa moja linaloshughulikia Huduma za
Watoto (UNICEF), Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) sambamba na Redio
Jamii 10 nchini Tanzania wenye lengo la kuendeleza kampeni za hamasa kwa
vijana kupunguza maambukizi mapya ya VVU.
Vijana wa kiume nao walihamasika kupima afya zao bure bila malipo.
0 maoni:
Post a Comment