Thursday, September 4, 2014


New boy: Loic Remy has decided to take the No 18 shirt after signing for Chelsea on Sunday
Kijana mpya: Loic Remy ameamua kuchukua jezi namba 18 baada ya kujiunga na Chelsea jumapili iliyopita.

MSIMU ujao, Loic Remy hatavaa jezi namba 9 inayosemekana kuwa na gundu katika klabu ya Chelsea. 
Kuondoka kwa Fernando Torres kumeifanya jezi hiyo ambayo kwa utamaduni anavaa mshambuliaji wa kati ibaki bila mtu.
Lakini Remy ambaye amejiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 10.5 akitokea Queens Park Rangers, amechagua kuvaa jezi namba 18 na ilithibitishwa jana usiku wakati klabu hiyo ya ligi kuu ikitangaza orodha ya wachezaji 25 wa timu hiyo sambamba na namba za jezi zao.
Jezi namba 9 itabaki bila mtu mpaka mwezi januari na hii inawezekana ikawa moja ya historia nzuri ya karibuni.
Cursed? The Chelsea players seem to have avoided Fernando Torres' No 9 shirt 
Gundu? Wachezaji wa Chelsea wameonekana kuiogopa jezi namba 9 aliyokuwa anavaa Ferando Torres.
Change: Didier Drogba asked for Oscar's No 11 shirt after originally being handed the No 15
Mabadiliko: Didier Drogba aliomba jezi namba 11 kwa Oscar baada ya awali kupewa jezi namba 15

Torres alifunga mabao 20 katika mechi za ligi kuu kwa miaka mitatu na nusu aliyokaa Stamford Bridge.
Mchezaji aliyemtangulia kuvaa jezi hiyo Franco Di Santo,alishindwa kufunga bao lolote na Steve Sidwell na Khalid Boulahrouz hawakufurahia maisha yao Chelsea wakivalia jezi hiyo.
Kabla ya hapo, mshambuliaji wa Argentina, Hernan Crespo, katika msimu wake mmoja akivalia jezi hiyo alifunga mabao 10 tu.
 Mateja Kezman aliwasili Chelsea akitokea PSG alikofunga mabao 78 katika misimu miwili nchini Uholanzi, lakini akivalia jezi namba 9 katika klabu ya Chelsea alifunga mabao 7 tu.
Petr Cech ameendelea kuvalia jezi namba 1 licha ya Thibaut Courtois kuanza msimu huu kama kipa chaguo namba moja kwa kocha Jose Mourinho.


Novak Djokovic amefanikiwa kumtupa nje ya michuano ya wazi ya Marekani " Us Open " mchezaji wa Uingereza Andy Murray na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Djokovic sasa atacheza na Kei Nishikori wa Japan kwenye hatua hiyo ya nusu fainali.

Andy Murray akijaribu kuurudisha mpira uliopigwa na Novac Djokovic
Novac Djokovic akishangilia kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.


Wayne Rooney akifunga bao lake kwa mkwaju wa penati kipindi cha pili baada ya kwenda 0-0 kipindi cha kwanza.
Rooney akishangilia baada ya kuitanguliza England mbele ya bao 1-0Rooney akishangilia bao lake la penati dakika ya 68 na Jordan Henderson akipongeza pia..
Wayne Rooney akimiliki mpira dhidi ya mchezaji wa  Norway Mats Daehli.
BAO la England lilifungwa na Wayne Rooney kipindi cha pili kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 68 baada ya mchezaji wa England Sterling kuangushwa ndani ya box na Omar Elabdellaoui wa Norway.
Wayne Rooney nafasi yake ilichukuliwa na Danny Welbeck katika dakika ya 79 kipindi cha pili.
Taswira ya mchezo wa  England na Norway kwenye Uwanja wa  Wembley mbele ya mashabiki. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa 0-0 England ni dhidi Norway


Di MariaÁngel Di María akishangilia bao lake kwa aina yake!!
Sergio Agüero aliifungia bao la kwanza katika dakika 20, Bao la pili lilifungwa na Erik Lamela dakika ya 40 na kufanya kwenda mapumziko bao 2-0 dhidi ya Germany. Kipindi cha pili Argentina hawakuishia hapo dakika ya 47 Federico Fernández aliongeza bao la tatu. Bao la nne lilifungwa na Mchezaji mpya wa Man United Ángel Di María aliyewachomoka kwa kiufundi mapeki wa Germany na kujifungia bao hilo dakika y 50.
Germany walipata bao lao kupitia kwa André Schürrle 52 na dakika ya 78 kipindi cha pili M. Götze alifunga bao la pili na kufanya 4-2.
MECHI ZA KIMATAIFA ZA KIRAFIKI:
RATIBA/MATOKEO
Jumatano Septemba 3

Denmark 1 vs 2 Turkey
Russia 4 vs 0 Azerbaijan
Ukraine vs Moldova
 Czech Rep.0  vs 1 USA
Germany 2 vs 4 Argentina
R. of Ireland 2 vs 0 Oman
England 1 vs 0 Norway
Alhamisi Septemba 4
19:20 Slovakia v Malta
20:45 Sweden v Estonia
21:00 Bos-Herce v Liechtenstein
21:00 Croatia v Cyprus
21:45 Belgium v Australia
21:45 Italy v Netherlands
22:00 France v Spain
Ijumaa Septemba 5
13:45 Japan v Uruguay
Jumamosi Septemba 6
04:00 Brazil v Colombia
Jumapili Septemba 7
05:00 Chile v Mexico
21:45 Serbia v France
Jumatatu Septemba 8
14:00 South Korea v Uruguay
23:00 Saudi Arabia v Australia
Jumatano Septemba 10
03:00 Chile v Haiti
05:00 Brazil v Ecuador
05:00 Mexico v Bolivia

waliotembelea blog