Monday, November 23, 2015


Jumanne Usiku Chelsea wako Ugenini kucheza Mechi ya Kundi G la UEFA CHAMPIONS, Dhidi ya Maccabi Tel Aviv wakiwa na matumaini ya kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu wakiwa na Mechi 1 mkononi.
Hapo kesho, Chelsea wanaweza kufuzu wakiishinda Maccabi ambayo ishatupwa nje ikiwa Dynamo Kiev haishindi Mechi yao na FC Porto huko Ureno.
Na hata Sare kwa Chelsea inaweza kuwasaidia ikiwa FC Porto itaifunga Dynamo Kiev.
Chelsea wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa kwenye morali nzuri baada ya Jumamosi kushinda Mechi yao ya kwanza ya kutoshinda Mechi 3 kwa kuifunga Norwich City 1-0 katika Ligi Kuu England.
Pia Chelsea wanarudiana na Maccabi ambayo waliitwanga 4-0 katika Mechi yao ya kwanza huko Stamford Bridge.
Lakini Maccabi, chini ya Kocha kutoka Serbia, Slavisa Jokanovic, ambae aliwahi kuichezea Chelsea na pia wanae Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Tal Ben Haim, wameahidi kutia ngumu licha ya kuwa tayari wapo nje ya Mashindano haya.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA 

Mechi  kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku.
Jumanne Novemba 24

KUNDI E
20:00 BATE Borislov v Bayer Leverkusen
Barcelona v AS Roma
KUNDI F
Arsenal v Dinamo Zagreb
Bayern Munich v Olympiakos
KUNDI G
FC Porto v Dynamo Kiev
Maccabi Tel Aviv v Chelsea
KUNDI H
2000 Zenit Saint Petersburg v Valencia
Lyon v KAA Gent
Jumatano Novemba 25
KUNDI A
Malmö FF v Paris St Germaine
Shakhtar Donetsk v Real Madrid
KUNDI B
20:00 CSKA v VfL Wolfsburg
Man United v PSV Eindhoven
KUNDI C
18:00 FC Astana v Benfica
Atletico Madrid v Galatasaray
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach v Sevilla
Juventus v Man City


RAIS wa Real Madrid Florentino Perez ameitisha Mkutano na Wanahabari utakaofanyika Leo Saa 3 na Nusu Usiku kwa Saa za Bongo na hili limekuja mara baada ya Jumamosi kutandikwa 4-0 na Barcelona kwenye El Clasico iliyochezwa Nyumbani kwao Santiago Bernabeu.
Wakati Real inacharangwa na Barca Juzi Jumamosi, Mashabiki wa Real waliokuwepo Uwanjani Bernabeu walimtaka Perez ajiuzulu lakini hili Leo halitegemewi na hata kutimuliwa Kocha Rafa Benitez nako hakutarajiwa.
Wadau wengi wa Real wanamlaumu Perez kwa kuingilia upangaji Timu na kung’ang’ania kuchezeshwa Wachezaji wakubwa hata kama wamedorora na kuachwa Wachezaji ambao wako kwenye fomu.
Mwaka 2006, Mashabiki walimgeukia na kumsakama Perez ambae ghafla alibwaga manyanga na kuachia wadhifa wake wa Urais.
Mkutano huo wa Leo na Wanahabari umekuja baada ya mapema Leo Bodi ya Real kuketi kutafakari kipigo chao kutoka kwa Barca. 
Ushindi wa Barca wa Jumamosi umewafanya wawe Pointi 6 kileleni mbele ya Real ambapo wameporomoka hadi Nafasi ya 3 baada ya Atletico Madrid Jana kuifunga Real Betis 1-0 na kushika Nafasi ya Pili.
Benitez, aliewahi kuzifundisha Valencia, Liverpool, Inter Milan, Chelsea na Napoli, ni Meneja wa 10 chini ya himaya ya Perez na alitwaa wadhifa huo mwishoni mwa Msimu uliopita kutoka kwa Carlo Ancelotti. Ikiwa Benitez atatimuliwa, Wadau wengi wanahisi Gwiji la France Zinedine Zidane, ambae sasa anaifundisha Timu B ya Real, ndie atakaepewa Timu.Mechi inayofuata kwa Real ni hapo Jumatano Ugenini huko Ukraine wakicheza na Shakhtar Donetsk katika Mechi ya Kundi A la UEFA CHAMPIONS LIGI ambao wao washafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi 2 mkononi.
Ikiwa Real wataifunga Shakhtar basi watajihakikishia kufuzu toka Kundi A wakiwa ndio Vinara.


MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger ametamka kuwa Kiungo wao Francis Coquelin atakuwa nje kwa kipindi kisichopungua Miezi Miwili baada ya kuumia Goti Timu yao ilipochapwa 2-1 huko The Hawthorns na West Bromwich Albion.Kipigo hicho cha Jumamosi toka kwa WBA kiliwakosesha Arsenal kukwea kilele cha Ligi Kuu England na kujikuta wametupwa Nafasi ya 4.
Pia kuumia kwa Coquelin na pigo kubwa kuelekea Mwezi Desemba ambao una Mechi mfululizo hadi Mwaka mpya.
Msimu huu, Coquelin, mwenye Miaka 24, ameikamata Namba katika Kikosi cha Kwanza cha Arsenal.

Alipoulizwa ikiwa Kiungo huyo wa Kimataifa wa France ameumia sana, Wenger alijibu: “Siku zote nakuwa mwangalifu lakini nadhani yupo nje si chini ya Miezi Miwili na tunasubiri uchunguzi zaidi.”


Adam Lallana akifurahia Ushindi kwenye Uwanja wa Etihad baada ya Eliaquim Mangala (katikati) kujifunga.
Philippe Coutinho akishangilia bao lake

Firmino alifanya 3-0

Straika wa Man City  Sergio Aguero ndie aliyewapa bao la kufutia machozi Etihad

Manchester City walipata bao lao kupitia kwa Sergio Agüero dakika ya 44 na bao kuwa 3-1.
Liverpool walipata bao kupitia kwa Eliaquim Mangala aliyejifunga bao mapema dakika ya 7 na bao la pili lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 23 na lile la Roberto Firmino dakika ya 32. 


Dakika ya 81 Martin Skrtel alipiga bao la 4 na kufanya matokeo kuwa 4-1 dhidi ya Timu ya Manchester City.


Jamie Vardy akishangilia bao lake la 10 na kwenye mechi 10 leo hii.
Bao za Jamie Vardy, Leonardo Ulloa na Okazaki zimewapa Leicester City ushindi wa 3-0 walipocheza Ugenini huko Saint James Park na Newcastle na kuwapaisha hadi kileleni mwa Ligi Kuu England ambako wanaweza kubaki ikiwa baadae Leo Man City hawatashinda Mechi yao na Liverpool.
Bao la Leo la Jamie Vardy limemfanya afikishe Bao 10 mfululizo kwenye Ligi na kumafanya aishike Rekodi ya Straika wa zamani wa Manchester United Ruud van Nistelrooy aliefanya hivyo hapo hapo Saint James Park.

Mambo yamekwenda kombo leo kwa Meneja Steve McClaren

waliotembelea blog