Friday, December 25, 2015


MENEJA wa Manchester United Louis van Gaal hana njia ya mkato ili kuokoa kibarua chake bali kuifunga Stoke City huko Britannia Stadium hapo Jumamosi, Boksing Dei.
Man United hawajashinda katika Mechi 4 za Ligi Kuu England na Mechi hii na Stoke imechukua umuhimu mkubwa.
Hilo linajulikana na Van Gaal mwenyewe ambae amesema Mechi na Stoke ni lazima washinde.
Van Gaal ameeleza: “Ndio, kama ukipoteza Mechi 3 mfululizo unahitaji ushindi. Tumetilia mkazo kupata ushindi lakini ni kazi ngumu. Stoke City ni wagumu waliifunga hata Man City.”
Mdachi huyo amekiri Stoka ina Wachezaji wazuri hasa Mafowadi wao, Bojan na Xherdan Shaqiri, ambao waliwahi kuzichezea Klabu kubwa za Barcelona na Bayern Munich.
Katika Mechi 15 zilizopita, Man United wamepoteza Mechi 1 tu kwa Stoke.

Hali za Wachezaji
Kwenye Mechi hii, Man United itawakosa Majeruhi Jesse Lingard, Matteo Darmian, Marcos Rojo, Antonio Valencia na Luke Shaw.
Pia, Kiungo Bastian Schweinsteiger hatacheza akiwa anamaliza Kifungo chake cha Mechi 3.
Stoke itawakosa Majeruhi Peter Odemwingie, Marc Muniesa, Stephen Ireland na Shay Given huku Peter Crouch na Geoff Cameron wakiwa na hati hati.

Juan Mata na Ander HerreraPereira na RomeoMatteo DarmianDepay na Jesse

Wayne RooneyCarrick Picha ya pamojaMorgan na MartialJuan Mata na Ander HerreraMartial na Morgan


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Desemba 26

15:45 Stoke vs Man United
18:00 Aston Villa vs West Ham
18:00 Bournemouth vs Crystal Palace
18:00 Chelsea vs Watford
18:00 Liverpool vs Leicester
18:00 Man City vs Sunderland
18:00 Swansea vs West Brom
18:00 Tottenham vs Norwich
20:30 Newcastle vs Everton 

22:45 Southampton vs Arsenal

www.bukobasports.comSTRAIKA MAHIRI wa Tanzania anaechezea Klabu ya Congo DR, TP Mazembe Mbwana Samatta yuko njiani kwenda Ulaya kujiunga na Klabu kubwa ya Belgium KRC Genk.
Kwa mujibu wa Jarida la kuaminika la France, L’Equipe, TP Mazembe na Genk wamefikia makubaliano kwa Fowadi huyo hatari kuhamia Genk Mwezi Januari Dirisha la Uhamisho likifunguliwa.
Inaaminika Samatta atasaini Mkataba wa Miaka Minne na Nusu na Genk ambayo inacheza Ligi Kuu ya Belgium iitwayo Belgian Jupiler League na wao wapo Nafasi ya 6 baada ya Kushinda Mechi 8, Sare 4 na Kufungwa 8 Msimu huu.
Msimu huu, Samatta amewika mno Afrika akiwa na TP Mazembe kwa kufunga Bao 8 kwenye CAF CHAMPIONS LIGI na kuwapa Ubingwa wao wa 5 wa Afrika.


IMG_7348Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leoIMG_7989Diamond akicheza na mashabiki wake waliofurika Dar Live.
IMG_7359Akicheza na wacheza shoo wake wa kike.IMG_1416Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live wakiendelea kumshangilia Diamond.IMG_7371Wacheza shoo wa kike wa Diamond wakifanya yao.IMG_7324Diamond akiwachombeza mashabiki. IMG_7325Diamond akicheza na wacheza shoo wake wa kiume. IMG_7344Akiongea na mashabiki. IMG_7377
IMG_7379 IMG_7383Diamond akifanya yake na wacheza shoo wake.IMG_7390Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii. IMG_7432Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live. IMG_7455
IMG_7973Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live. IMG_7927Mashabiki baada ya kupagawa na shoo. IMG_7975...Akiongea na mashabiki wake. IMG_7991Akiwasalimia mashabiki.

waliotembelea blog