Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim
Lipumba akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafuasi wa chama
hicho waliojitokeza katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar
es salaam,na kuwaambia kuwa CUF ni Taasisi,hivyo wanachama wote wanatakiwa
kukijenga chama hicho wawe na vyeo ama wasiwe na vyeo kazi kubwa ni
kukijenga chama cha CUF,Pro Lipumba aliyasema maneno hayo bila kutoa ufafanuzi wa kina.
Profesa Lipumba
alitakiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama
hicho,lakini mpaka dakika za mwisho hakufanya mkutano huo badala yake
alikuwa
na kikao na wazee wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa dini na
wanachama,aidha wakati akiondoka katika ofisi hizo ndipo akazungumza
maneno hayo hakuyafafanua zaidi.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim
Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari
katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam
Baadhi ya wanachama wa chama cha
CUF wakiwa katika makao makuu ya chama hicho wakipiga kelele kuashiria
kumuunga mkono mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba.
Wana CUF wakiwa wamejitokeza kwa
wingi katika makao makuu ya chama hicho Buguruni kumsikiliza Mwenyekiti
wao Profesa Ibrahim Lipumba
Mpiga Picha wa Gazeti la
Uhuru Emmanuel Ndege akisaidiwa na waandishi wenzake mara baada ya
kujeruhiwa na feni wakati waandishi hao wakisubiri Mwenyekiti wa CUF
Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza nao katika makao makuu ya chama hicho
Buguruni.PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jami.
MWENYEKITI wa Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),amewataka wanachama
wa chama hicho kukijenga kwa nafasi
walizonazo iwe kiongozi au mwanachama wa kawaida.
Lipumba ameyasema hayo wakati
akizungumza na wanachama waliofika katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho
wakitaka kauli ya yake juu ya chama na taarifa zilizopo katika mitandao juu ya
kutaka kuachia nafasi yake uenyekiti wa chama hicho.
Lipumba amesema kuwa chama ni taasisi sio chama mtu
mmoja anaweza kufanya kila kitu hivyo wanachama tambueni hivyo.
Aidha amewataka wanachama waisome katiba
ya chama hicho kwa sababu zipo ili kuweza kujua chama jinsi kinavyoendeshwa
kutokana na katiba ambayo inapitishwa na wanachama.
Wakati huo huo mkutano ulitishwa na chama hicho kwa lengo la
Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa,Ibrahim Lipumba umearishwa kutokana na wazee
wa chama hicho kuvamia Ofisi hiyo na kwenda kuzungumza na mwenyekiti wa chama
hicho.
Akizungumza wakati kuarisha Mkutano
huo Mwenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu Bara,Magdalena Sakaya amesema kuwa mkutano
huo ulikuwa wa mwenyekiti Lipumba lakini wazee wa chama wamevamia hivyo hawezi
kuzungumza tena.
Sakaya amesema kitu ambacho alikuwa
anataka kuzungumza anajua mwenyewe hivyo haiwezekani mtu mwingine azungumze
kitu cha mwenyekiti.
“Jamani tunaahirisha mkutano wetu
ambao ulitakiwa kuzungumzwa na mwenyekiti lakini wazee wa chama wamevamia ofisi
na kuwa na mazungumzo na mwenyekiti”amesema Sakaya Naibu Katibu Mkuu Bara.