Wednesday, August 5, 2015


barca
Kiungo raia wa Argentina Javier Mascherano ameteuliwa kuwa nahodha wa nne kwenye klabu ya Barcelona akiongeza idadi ya manahodha ambayo ilikuwa imebakia manahodha watatu baada ya kuondoka kwa Xavi Hernandez.
Kuondoka kwa Xavi Hernandez kumefungua nafasi moja ya unahodha baada ya kupandishwa kwa Andres Iniesta ambaye amekuwa nahodha wa kikosi cha kwanza huku Lionel Messi akiwa nahodha wa pili na Sergio Busquets akiwa nahodha wa tatu.
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amemzungumzia Mascherano kama mchezaji ambaye ana sifa ya uongozi hata kama sio nahodha rasmi kwenye timu na kwa sababu hii ana kila sifa ya kuwemo kwenye orodha ya manahodha wa klabu.
Enrique ameongeza kuwa Mascherano ni mchezaji ambaye timu nzima inamheshimu na hivyo ni uchaguzi ambao haukuwa na pingamizi toka kwa wachezaji wengine.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog