Wednesday, August 5, 2015

LIP1
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wafuasi wa chama hicho waliojitokeza katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni jijini Dar es salaam,na kuwaambia kuwa CUF ni Taasisi,hivyo wanachama wote wanatakiwa kukijenga chama hicho wawe na vyeo ama wasiwe na vyeo kazi kubwa ni kukijenga chama cha CUF,Pro Lipumba aliyasema maneno hayo bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Profesa Lipumba alitakiwa kuzungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho,lakini mpaka dakika za mwisho hakufanya mkutano huo badala yake alikuwa na kikao na wazee wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa dini na wanachama,aidha wakati akiondoka katika ofisi hizo ndipo akazungumza maneno hayo hakuyafafanua zaidi.
LIP2
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akisisitiza jambo wakati akizungumza na baadhi ya wanahabari katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es salaam
LIP3
Baadhi ya wanachama wa chama cha CUF wakiwa katika makao makuu ya chama hicho wakipiga kelele kuashiria kumuunga mkono mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba.
LIP4
Wana CUF wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika makao makuu ya chama hicho Buguruni kumsikiliza Mwenyekiti wao Profesa Ibrahim Lipumba 
LIP5
Mpiga Picha wa Gazeti la Uhuru Emmanuel Ndege akisaidiwa na waandishi wenzake mara baada ya kujeruhiwa na feni wakati waandishi hao wakisubiri Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza nao katika makao makuu ya chama hicho Buguruni.PICHA KWA HISANI YA FULLSHANGWE BLOG.
 
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jami.
 
MWENYEKITI wa Taifa wa  Chama Cha Wananchi (CUF),amewataka wanachama wa  chama hicho kukijenga kwa nafasi walizonazo iwe kiongozi au mwanachama wa kawaida.
 
Lipumba ameyasema hayo wakati akizungumza na wanachama waliofika katika ofisi ya makao makuu ya chama hicho wakitaka kauli ya yake juu ya chama na taarifa zilizopo katika mitandao juu ya kutaka kuachia nafasi yake uenyekiti wa chama hicho.
 
Lipumba  amesema kuwa chama ni taasisi sio chama mtu mmoja anaweza kufanya kila kitu hivyo wanachama tambueni hivyo.
 
Aidha amewataka wanachama waisome katiba ya chama hicho kwa sababu zipo ili kuweza kujua chama jinsi kinavyoendeshwa kutokana na katiba ambayo inapitishwa na wanachama.
 
Wakati huo huo  mkutano ulitishwa na chama hicho kwa lengo la Mwenyekiti wa Chama hicho Profesa,Ibrahim Lipumba umearishwa kutokana na wazee wa chama hicho kuvamia Ofisi hiyo na kwenda kuzungumza na mwenyekiti wa chama hicho.
 
Akizungumza wakati kuarisha Mkutano huo Mwenyekiti wa Naibu Katibu Mkuu Bara,Magdalena Sakaya amesema kuwa mkutano huo ulikuwa wa mwenyekiti Lipumba lakini wazee wa chama wamevamia hivyo hawezi kuzungumza tena.
 
Sakaya amesema kitu ambacho alikuwa anataka kuzungumza anajua mwenyewe hivyo haiwezekani mtu mwingine azungumze kitu cha mwenyekiti.
 
“Jamani tunaahirisha mkutano wetu ambao ulitakiwa kuzungumzwa na mwenyekiti lakini wazee wa chama wamevamia ofisi na kuwa na mazungumzo na mwenyekiti”amesema Sakaya Naibu Katibu Mkuu Bara.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog