Friday, September 18, 2015



Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akishuka kutoka kwenye Helkopta anayoitumia kwa ziara zake za Kampeni, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Muleba, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muleba Kusini kupitia CHADEMA, Kashasira Alistides, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, Mjini Muleba, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015. Katikati ni Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye.

Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza, Mh. Ezeckiel Wenje akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni zake za kuwania nafasi hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muleba Kusini kupitia CHADEMA, Kashasira Alistides, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, Mjini Muleba, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.



LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Septemba 19

14:45 Chelsea vs Arsenal
17:00 Aston Villa vs West Brom
17:00 Bournemouth vs Sunderland
17:00 Newcastle vs Watford
17:00 Stoke vs Leicester
17:00 Swansea vs Everton
19:30 Man City vs West Ham
Jumapili Septemba 20
15:30 Tottenham vs Crystal Palace
18:00 Southampton vs Man United
18:00 Liverpool vs Norwich
Jose Mourinho v Arsene Wenger


FIFA imetangaza kuwa ile Hafla ya kumtangaza Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2015 ambae hutunukiwa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or itafanyika Jumatatu Januari 11, 2016 huko Zurich Nchini Uswisi.
Siku hiyo pia hutangazwa Mchezaji Bora kwa upande wa Kinamama pamoja na Kocha Bora kwa pande zote mbili za Wanaume na Wanawake.
Pia, Goli Bora la Mwaka, ambalo hutunukiwa Tuzo ya Puskas, litajulikana baada ya Kura kutoka kwa Wadau wote inayofanyika Mtandaoni.
Tuzo nyingine ambazo zitatolewa Siku hiyo ni ile ya Uchezaji wa Haki na pia, kwa kushirikiana na FIFPro, Chama cha Wachezaji wa Soka la Kulipwa, kitatangazwa Kikosi Bora cha Mwaka kijulikanacho kama FIFA FIFPro World XI.
Tuzo ya mwisho itakayotolewa Siku hiyo ni ile Tuzo ya Rais wa FIFA ambayo humwendea Mtu au Taasisi iliyotoa mchango bora katika Soka.

FIFA Ballon d’Or
WASHINDI WALIOPITA:

2014 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2013 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2012 Lionel Messi [Argentina]
2011 Lionel Messi [Argentina]
2010 Lionel Messi [Argentina]
2009 Lionel Messi [Argentina]
2008 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2007 Kaká [Brazil]



Kufuatia safari ya vijana watano wa U15 Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias, Athumani Maulid waliokwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando Pirates kufuatia mwaliko uliotolewa na TFF na klabu hiyo, safari hiyo ilikamilika na vijana wamerejea nyumbani.
Vijana hawa waliongozana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi wakiwa Afrika Kusini walifanya mazoezi ya wiki moja kuanzia Septemba Mosi mpaka tarehe 7 Septemba, 2015 chini ya uangalizi wa Augusto Placious ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Orlando Pirates.
Idara ya ufundi ya Orlando Pirates imejiridhisha na kiwango kilichoonyeshwa na vijana hao.



Mchezaji wa timu ya Ilala Rukia Annaph (kushoto) akichuana vikali na mchezaji wa timu ya Temeke Christina Daudi katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1

Mchezaji wa timu ya Ilala Tumaini Michael (Kulia) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17). Temeke iliibukana na ushindi wa magoli 2-1.

Mchezaji wa timu ya Ilala Jackline Albert (Kushoto) akimtoka mchezaji wa timu ya Temeke Shamimu Hamis katika mchezo wa nusu fainali ya Airtel Rising Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi September 17. Temeke ilishinda 2-1.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akisalimian na ndugu wa Marehemu Cornel Pastory,alipowasili kwenye kijiji cha Nyakantutu,wilayani Biharamulo.Dkt Magufuli amemaliza mikutano yake ya kampeni mkoani Kigoma na kuelekea nyumbani kwake wilayani Chato kwa mapumziko ya siku mbili,ambapo siku ya jumapili atawahutubia Wananchi mjini humo na kisha kuanza ziara yake mkoani Kagera.
 Marehemu Cornel Pastory enzi za uhai wake
  Dk Magufuli akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza shule ya Msingi Chato, marehemu, Cornel Pastory. 
  Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.
  Dk Magufuli akiomba alipozuru kaburi la aliyekuwa mwalimu wake wa darasa la kwanza marehemu Pastory wilayani Biharamulo, Kagera.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyakanazi waliokuwa wamefunga barabara wakitaka wamuone na kumsalimia sambamba na kumueleza matatizo yao ili aweze kuyatatua iwapo atapewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika awamu ya tano 
 Wananchi wa Nyakanazi wakimsikiliza Dkt Magufuli kwa makini 
  Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akijinadi  kwa  wananchi huku akishangiliwa aliposimama kusalimia katika Mji wa Nyakanazi, wilayani Biharamulo, Mkoa wa Kagera leo.

 Baadhi ya wafuasi wa chama cha CCM wakifuatilia mkutano wa kampeni wa Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Biharamulo mjini mkoani Kagera.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akijinadi kwa wananchi mjini Biharamulo ili wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka hu.
 Wananchi wa Biharamulo wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia mjini humo jioni ya leo
 Wakazi wa Biharamulo wakishangilia mara baada ya kusikiliza sera za Dkt Magufuli mapema leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa CCM mjini humo .


KASEJA...

Kipa Juma Kaseja, kesho anatarajia kuweka rekodi iwapo ataichezea Mbeya City.


Mbeya City inatarajia kuchuka dimbani kwa “Mbeya derby” dhidi ya wapinzani wao wakubwa Prisons.

Mechi hiyo inachezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya na kama Kaseja atakuwa langoni, atakuwa kwa mara nyingine anajumuika kwenye mechi ya watani nje ya Dar es Salaam.

Kaseja ni kati ya wachezaji waliocheza mechi nyingi zaidi za watani lakini ni akiwa Simba mara nyingi zaidi na akiwa Yanga pia wakati wakiivaa Simba.

Lakini safari hii, Kaseja anacheza derby ambayo itakuwa haihusishi timu za Dar es Salaam au timu kongwe za Yanga na Simba.


Kocha Juma Mwambusi amesema ana imani na kiwango cha Kaseja na akiamka salama, yuko tayari kumtumia hiyo kesho.

Rais wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Florentino Perez ambaye amezoeleka kuingia katika headlines kwa masuala yake ya kufanya usajili mkubwa kwa wachezaji ambao klabu yake inawahitaji, huenda umezoea kumsikia katika suala hilo, safari hii kafanya hili kwa wakimbizi kutokea Syria.
real-madrid-syria-_3444522b (1)
Florentino Perez ameingia katika headlines baada ya kuwapa nafasi wakimbizi kutoka Syria kutembelea uwanja wa klabu ya Real Madrid Santiago Bernabeu pamoja na kuwapa mualiko wa kuhudhuria mechi yao dhidi ya Granada.
syrian-refugee-rea_3444524b
Usama Alabed Almohsen na watoto wake Zied na Mohammed ndio waliyopata mualiko huo kutoka kwa Perez. Usama na familia yake waliwasili Hispania kwa usafiri wa treni usiku wa Jumatano ya September 16, hata hivyo Usama ambaye alikuwa kocha wa mpira wa miguu wakati yupo Syria amepewa nafasi ya kuongeza taaluma yake ya ukocha katika chuo cha Madrid.
Syrian-Refugees-Visit-the-Santiago-Bernabeu-Stadium


Teknolojia ya sasa inazidi kukua siku hadi siku, wataalamu wamekuwa wakibuni vitu mbalimbali duniani kwa lengo la kuleta ushindani.
Katika piti pita zangu nimekutana na hizi hoteli ambazo zimeingia kwenye maajabu ya duniani kutokana na ubunifu wake…
hot17
1 – Montaña Mágica Lodge (Magic Mountain Lodge) – Chile

hot16
2 – The Dog Bark Park Inn – USA

hot15
3– Can Sleep Hotel – Denmark

hot14
4 – The Bird’s Nest – TreeHotel – Sweden

hot13
5. Gagudju Crocodile Holiday Inn –Australia

hot12
6 -The Mirrorcube – TreeHotel – Sweden

hot11
7. Das Park Hotel – Austria

hot10
8– Glass Igloos – Kakslauttanen Hotel and Igloo Village – Finland

hot8
9- V-House Jungle Hotel – Mexico

hot7
10- Zhangzhou Wei Qun Lou Inn – China

hot5
11. Mira Mira Fantasy Accommodation – Australia

hot2
12. Hang Nga Guesthouse and Art Gallery – Vietnam

hot3
13- La Balade des Gnomes Hotel – Belgium

tem
14- Elephant Villa – Kumbuk River Resort – Sri Lanka

cot
15- Costa Verde Hotel – Costa Rica

waliotembelea blog