Friday, September 18, 2015


FIFA imetangaza kuwa ile Hafla ya kumtangaza Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2015 ambae hutunukiwa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or itafanyika Jumatatu Januari 11, 2016 huko Zurich Nchini Uswisi.
Siku hiyo pia hutangazwa Mchezaji Bora kwa upande wa Kinamama pamoja na Kocha Bora kwa pande zote mbili za Wanaume na Wanawake.
Pia, Goli Bora la Mwaka, ambalo hutunukiwa Tuzo ya Puskas, litajulikana baada ya Kura kutoka kwa Wadau wote inayofanyika Mtandaoni.
Tuzo nyingine ambazo zitatolewa Siku hiyo ni ile ya Uchezaji wa Haki na pia, kwa kushirikiana na FIFPro, Chama cha Wachezaji wa Soka la Kulipwa, kitatangazwa Kikosi Bora cha Mwaka kijulikanacho kama FIFA FIFPro World XI.
Tuzo ya mwisho itakayotolewa Siku hiyo ni ile Tuzo ya Rais wa FIFA ambayo humwendea Mtu au Taasisi iliyotoa mchango bora katika Soka.

FIFA Ballon d’Or
WASHINDI WALIOPITA:

2014 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2013 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2012 Lionel Messi [Argentina]
2011 Lionel Messi [Argentina]
2010 Lionel Messi [Argentina]
2009 Lionel Messi [Argentina]
2008 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2007 Kaká [Brazil]

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog