Friday, September 18, 2015


KOCHA wa Brazil Dunga ametangaza Kikosi chake cha Brazil ambacho Oktoba kitaanza safari ya kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2018 huko Russia.
Brazil, ambao ni washika Rekodi kwa kutwaa Ubingwa wa Dunia mara 5, wanacheza Mechi za Mchujo za Kanda ya Marekani ya Kusini na Mechi yao ya kwanza ni huko Santiago Nchini Chile hapo Oktoba 8 dhidi ya Wenyeji Chile ambao ndio Mabingwa wa Copa America.
Tarehe 13 Oktoba, Brazil watakuwa kwao huko Fortaleza kucheza na Venezuela katika Mchujo huo.
Kocha wa Brazil Dunga alimtumia Mkongwe Kaka katika Mechi zao za Kirafiki mapema Mwezi huu huko Marekani walipozifunga Costa Rica na USA lakini safari hii amemtema na kuwabakisha Hulk, anaechezea Klabu ya Urusi Zenit St Petersburg, na Wachezaji Wawili wa Liverpool Philippe Coutinho na Roberto Firmino.
Nae Neymar, Kepteni wa Brazil, ameachwa kwa vile yupo Kifungoni na kutoruhusiwa kucheza Mechi hizo kufuatia kufungiwa kwenye Fainali za Copa America huko Chile Mwezi Julai.


Brazil Squad to Face Chile, Venezuela
Position Players
Goalkeepers Jefferson (Botafogo), Marcelo Grohe (Gremio), Alisson (Internacional).
Defenders David Luiz (PSG), Miranda (Inter Milan), Marquinhos (PSG), Gil (Corinthians), Fabinho (Monaco), Rafinha (Bayern Munich), Filipe Luis (Atletico Madrid), Marcelo (Real Madrid)
Midfielders Luiz Gustavo (Wolfsburg), Fernandinho (Manchester City), Elias (Corinthians), Renato Augusto (Corinthians), Douglas Costa (Bayern Munich), Lucas Lima (Santos), Lucas Moura (PSG), Willian (Chelsea), Philippe Coutinho (Liverpool), Oscar (Chelsea)
Attackers Roberto Firmino (Liverpool), Hulk (Zenit)

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog