Friday, June 26, 2015


KOCHA mpya wa Simba, Muingereza Dylan Kerr amesema ataendeleza wachezaji chipukizi ili kuwa na timu bora kwa sasa na baadae.
Kerr aliyasema hayo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kulakiwa na wajumbe wa Kamati ya Simba, Collin Frisch na Said Tully.
“Nimefurahi kuja Tanzania na nawaahidi viongozi na mashabiki kuwa nitahakikisha naendeleza wachezaji chipukizi hili Simba iweze kutamba sasa na baadae”, alisema Kerr.
Kocha huyo ambaye amerithi mikoba ya Mserbia Goran Kopunovic amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Simba ambapo atakuwa anasaidiwa na kiungo wa zamani wa timu hiyo Suleman Matola.

Wakati Kerr akiwasili pia alikutana na kocha mpya wa makipa Idd Salim toka Kenya ambaye naye aliwasili tayari kwa kazi yake mpya kwenye klabu ya Simba.
Simba waliamua kuachana na Kopunovic na kusaka kocha huyo mpya baada ya Mserbia huyo kuhitaji Simba imlipe kiasi cha Dola za Marekani 50,000 (sh. Milioni 100) kama ada ya usajili na mshahara wake ambapo kila mwezi atakuwa analipwa dola za Marekani 14,000 9sh. Milioni 28).
Baada ya kushindwana kwenye malipo ndipo uongozi uliamua kumsaka kocha mpya na kumpata Kerr ambaye inasemekana atalipwa mshahara wa dola za marekani 9,000 sawa na milioni 18 kwa mwezi.
Dylan Kerr mwenye umri wa miaka 47, aliwahi kuwa mchezaji, alicheza beki wa kulia kwenye klabu za Leeds United, Reading, Blackpool na nyingine nyingi za Uingereza huku akihudumu kama kocha msaidizi kwenye timu mbalimbali katika nchi za Vietnam ambako ametoka kwenye timu ya Hai Phong F.C. ambako alimaliza mkataba 2014.


Morgan Schneiderlin
Manchester United wanajiandaa kutoa kitita cha £24million kumnasa Mchezaji wa Southampton Morgan Schneiderlin.
Mchezaji huyo alikuwa akiwaniwa na Arsenal na Tottenham lakini vyanzo vinaonesha Man United Pekee ndio yenye nafasi nzuri kumnunua mchezaji huyo na taratibu zitakamilia wiki ijayo.


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.
Akifungua kozi hiyo, Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine amesema ili nchi/Taifa lifanikiwe katika soka ni lazima kuwekeza katika mpira wa watoto na vijana ambao makocha hao ni sehemu ya uwekezaji huo.


“Tumekua na mashindano ya Taifa U-13, kikosi cha timu ya Taifa ya U-15 ambayo inashirikisha vijana wadogo, vijana hao wanapaswa kupata malezi na mafunzo yenu waalimu ili wafikiapo kuchezea timu za Taifa wawe wamekua kwenye msingi bora wa kuujua mpira wa miguu” alisema Mwesigwa.
Naye mkufunzi wa FIFA wa kozi hiyo ya makocha kutoka nchini Ujerumani, Eric Muller amesema hata ujerumani imefanikiwa baada ya kuwekeza katika soka la vijana, mwaka 2000 kwenye fainali za Euro nchi yao ilishika nafasi ya mwisho katika msimamo kundi lao kwa kupata poniti moja, lakini uwekezaji walioufanya kwenye soka la watoto na vijana umewapelekea kutwaa Ubingwa wa Dunia mwaka 2014.


Washiriki wa kozi hiyo ni makocha wa timu za vijana za mikoa yoye Tanzania, ambao watashirki na timu zao za mikoa katika michuano ya Copa Coca Cola mwaka huu.
Kozi hiyo ya makocha wa timu za watoto/vijana inayoendeshwa na wakufunzi wa FIFA, Ulric Mathews kutoka shelisheli na Eric Muller kutoka nchini Ujerumani itamalizika jumatatu tarehe 29 Juni, 2015.

STARS YAANZA MAZOEZI
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.
Stars inayonolewa na makocha wazawa, Charles Mkwasa na msaidizi wake Hemded Morocco, itakua ikifanya mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja huo wa Boko Veterani, huku timu ikiweka kambi yake katika hoteli ya Kiromo mjini Bagamoyo.
Wachezaji wote walioitwa wameripoti kambini tangu jana na leo wamefanya mazoezi asubuhi isipokua Aggrey Morris ambaye ni majeruhi nafasi yake imekuchukuliwa na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar) na Jonas Mkude aliyekwenda kufanya majaribio Afrika Kusini nafasi yake ikizibwa na Mudathir Yahya (Azam FC).


West Ham leo Ijumaa wamemsajili Payet kwa kitita cha £10.7m na hapa akiwa anapimwa Afya

Akisaini mkataba wa miaka 5 leo hii Ijumaa

West Ham tayari wanae Winga ambaye walikuwa wanamfukuzia siku nyingi Dimitri Payet kutoka Klabu ya Marseille ya Ufaransa.


Manchester United imeionya Real Madrid kwamba wanapaswa kulipa zaidi ya ile Ada ya Uhamisho inayoshika Rekodi ya Dunia kwa Kipa ikiwa wanamtaka Kipa wao David De Gea.
Habari zimedai ili kumng'oa Kipa huyo kutoka Spain huko Man United lazima Wanunuzi wavunje Rekodi ya ununuzi wa Kipa wa Italy Gianluigi Buffon iliyowekwa 2001 kwa kulipwa Pauni Milioni 32.6 aliponunuliwa kutoka Parma na kuhamia Juventus.
Man United ilimnunua De Gea, mwenye Miaka 24, Mwaka 2011 kutoka Atletico Madrid kwa Dau la Pauni Milioni 18.9 na kumfanya awe Kipa wa Pili kwa Bei ghali Duniani nyuma ya Gianluigi Buffon.

Inadaiwa msimamo wa Man United hivi sasa ni kutaka De Gea abaki na kumaliza Mkataba wake uliobakiza Miezi 12 na kisha kumpoteza bila kulipwa Fedha yeyote kuliko kumuuza sasa kwa Bei ya kutupwa.
Hata hivyo, zipo kila dalili kuwa Kipa huyo atang'oka Old Trafford kwani hata Nyumba ya kupanga aliyokuwa akiishi huko Cheshire, Kitongoji jirani ya Jiji la Manchester, imetangazwa kuuzwa.
De Gea ndie alietwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Man United kwa Misimu Miwili iliyopita na kukibeba sana Kikosi cha Meneja Louis van Gaal kufuzu 4 bora Msimu uliopita na kurudi tena kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao unaoanza Agosti.



 
Saa zisizopungua 48 baada ya klabu ya Manchester United kuripotiwa kutuma ofa ya kumsajili beki wa kimataifa wa Spain, Sergio Ramos, klabu yake ya Real Madrid imepokea ofa hiyo na imetoa uamuzi.
  Manchester United, juzi walituma ofa ya £35million kwa ajili ya kupata saini ya Ramos na klabu ya Madrid wameipiga chini ofa hiyo.
Madrid walimpa taarifa Ramos juu ya uamuzi wao wakati CEO wa klabu hiyo Jose Angel Sanchez alipokutana na Ramos na wawakilishi wake katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo.
Ramos, 29, aliondoka kwenda mapumzikoni huku akiiambia klabu kwamba anataka kufahamu hatma yake kwenye kikosi cha Madrid kabla timu haijakutana kwa ajili ya kwenda kwenye Pre Season Tour mnamo July 10.
Real, pia, hawataki kumpa mwanzo mgumu kocha wao mpya Rafael Benitez kutokana na mgogoro huu wa Ramos.
Ramos amekasirishwa sana baada ya kuona hapewi thamani anayostahili na ameonyesha kuwa tayari kwenda Old Trafford.
Inafahamika kwamba Ramos anapokea mshahara £4m kwa mwaka ndani ya Bernabeu na anataka kupewa mkataba mpya utakaokuwa na thamani ya £6.5m. United wanatajwa kuwa tayari kumtimizia matakwa yake ya mshahara kwa kumpa ofa ya ya mshahara wa £7.8m ili ahamie Old Trafford.
Baada ya Madrid kukataa ofa hiyo sasa taarifa zinasema klabu hiyo inaandaa ofa mpya na itatumwa hivi karibuni.
Ofa hiyo haitomuhusisha golikipa David De Gea kwa namna yoyote.

waliotembelea blog