Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney, siku kadhaa nyuma alifikia rekodi ya mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Uingereza Sir Bobby Charlton, usiku wa September 8 alivunja rekodi ya Sir Bobby Charlton kwa kufunga goli la 50.
Wayne Rooney alifunga goli la 50 kwa mkwaju wa penati akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza wakati wa mchezo dhidi ya Switzerland wa kuwania kufuzu kucheza EURO 2016, mechi ilimalizika kwa Uingereza kuibuka na ushindi wa jumla wa goli 2-0.
Baada ya mechi hiyo Rooney
aliingia katika chumba cha kubadilishia nguo huku akipigiwa makofi na
wachezaji wenzake pamoja na kocha na kukabidhiwa jezi namba 50 ambayo ni
jumla ya magoli aliyofunga katika timu ya taifa ya Uingereza.
Hii video ya Rooney na wachezaji wenzie wakiwa dressing room.