Wednesday, September 9, 2015



.
.
Unakumbuka ile ishu ya bondia wa ngumi Francis Cheka ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?
Sasa good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba bondia huyo wa mchezo wa masumbwi akiwa anatumikia kifungo cha nje kwa sasa anatarajia kwenda nchini Uingereza tarehe 15 mwezi huu kwenye mchezo wa masumbwi.
Leo sept 8 alikuta na ripota wa millardayo.com na kuzungumza machache kuhusiana na taratibu za safari yake pamoja na kifungo anachotumikia nje…’Kwanza namshukuru mwenyezi mungu niko katika hali ya salama kesi yangu katika ustawi wa jamii inaendelea vizuri na ustawi wa jamii niko nao katika hali ya kawaida sababu wao wanajua umuhimu wangu na kuweza kujua mimi Francis Cheka nahitaji nini kwa mashabiki wangu, mimi ni mtanzania ambaye ninawajenga umma wa watanzania kwenye michezo ya boxer’ – Francis Cheka
‘Ustawi wa jamii wamenipa ruksa ya kwenda kupigana kwenye pambano hilo nchini Uingereza nategemea kwenda tarehe 15 mwezi huu na mkurugenzi wa ustawi wa jamii ameweza kuniambia mawili matatu kuhusiana na taratibu au kitu gani ninachotakiwa kukifanya ili niweze kufanikisha safari yangu ya Uingereza’ – Francis Cheka

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog