Tuesday, June 9, 2015



Wananchi wa kijii cha Rukoma kata ya Rukoma wakiwa wamekusanyika wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo Bukoba vijijini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa katika uwanja wa Katoro,kwenye mkutano wa hadhara Bukoba vijijini mkoani Kagera jioni ya leo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongela akizungumza na wananchi na kuwaleza kuwa wasitishwe na mtu yeyote katika suala zima la kujiandikisa," asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini na wala msiogope",alisema Mh.Mongella.


Eugénie Le Sommer akipongezwa na wenzake baada ya kuifungia Timu yake bao katika dakika ya 29 kipindi cha kwanza kwenye Mchezo wa mpira wa Wanawake.Pongezi kwa Eugenie Le SommerKipindi cha kwanza dakika ya 29 Eugénie Le Sommer aliwafungia bao la pekee la Ushindi France kwa kuibuka kidedea dhidi ya Timu ya Taifa ya England kwa bao 1-0. Kipindi cha pili Timu hizo zilitoka bila kufungana.
Mtanange ukiendelea..Eugenie akiendesha mpiraElodie Thomis akichuana na Fara WilliamsKocha wa Timu hiyo ya Taifa ya France Philippe



Slaven Bilic ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa West Ham kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.
Bilic, Raia wa Croatia mwenye Miaka 46, anachukua nafasi ya Sam Allardyce alieachia ngazi mwishoni mwa Msimu ulioisha Mei baada ya kuifikisha Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England.
Bilic aliwahi kuichezea West Ham Mechi 54 kati ya Mwaka 1996 na 1997 na kisha kuwa Kocha wa Croatia kwa Miaka 6.

Pia Bilic alizifundisha Klabu za Lokomotiv Moscow ya Urusi na Besiktas ya Uturuki ambayo aliachana nayo Mwezi Mei.
Lakini katika Klabu zote hizo mbili hakuna mafanikio makubwa aliyoyaleta ingawa mwenyewe ameonyesha matumaini makubwa kwa kujiunga na West Ham moja ya Klabu kongwe za Jiji la London.

leoleo
 Mtandao wa Shirika la tathmini za thamani za wachezaji CIES kwa upande wa soka limetoa orodha mpya ya thamani za wachezaji katika ligi tano kubwa Ulaya.
Katika orodha iliyotolewa inaonyesha mshambuliaji wa Chelsea, Eden Hazard atauzwa kwa bei kubwa zaidi ya mshindi wa Ballon d’OrCristiano Ronaldo msimu huu.
Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ubelgiji ana thamani ya kati ya Pound Milioni 99 hadi Milioni 110.
Mshindi huyo wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa kulipwa England (PFA), ameshika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi, ambaye ana thamani ya Pound Milioni 207, wakati mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anakamilisha tatu bora kwa thamani ya kati ya Pound Mil. 83 hadi Mil. 92.
Wachezaji wenye thamani kubwa zaidi Ulaya
Jina la Mchezaji Muda wa mkataba umri Thamani (Pound)
Lionel Messi (Barcelona) 2018 27 188-207
Eden Hazard (Chelsea) 2020 24 99-110
Cristiano Ronaldo (Real Madrid) 2018 30 83-92
Neymar (Barcelona) 2018 23 66-73
Sergio Aguero (Manchester City) 2019 27 57-63
Raheem Sterling (Liverpool) 2017 20 54-60
Paul Pogba (Juventus) 2019 22 52-57
Diego Costa (Chelsea) 2019 26 52-57
Alexis Sanchez (Arsenal) 2018 26 50-55
James Rodríguez (Real Madrid) 2020 23 46-51
Luis Suarez (Barcelona) 2019 28 44-49
Antoine Griezmann (Atletico Madrid) 2020 24 44-48
Cesc Fàbregas (Chelsea) 2019 28 43-48
Isco (Real Madrid) 2018 23 42-46
Harry Kane (Tottenham) 2020 21 40-44
Gareth Bale (Real Madrid) 2019 25 38-42
Philippe Coutinho (Liverpool) 2020 22 37-41
Thibaut Courtois (Chelsea) 2019 23 37-41
Oscar (Chelsea) 2019 23 35-39
Karim Benzema (Real Madrid) 2019 27 33-37
Mario Gotze (Bayern Munich) 2017 23 32-35
Koke (Atletico Madrid) 2019 23 30-33
Christian Eriksen (Tottenham) 2018 23 30-33
Romelu Lukaku (Everton) 2019 22 29-33
Toni Kroos (Real Madrid) 2020 25 29-32
Willian Borges (Chelsea) 2018 26 29-31
Alvaro Morata (Juventus) 2019 22 28-31
Sergio Busquets (Barcelona) 2019 26 28-31
David Silva (Manchester City) 2019 29 28-31
Edinson Cavani (PSG) 2018 28 28-31
Angel Di María (Manchester United) 2019 27 27-30
Kevin de Bruyne (Wolfsburg) 2019 23 27-30
Wayne Rooney (Manchester United) 2019 29 27-29
Marco Verratti (PSG) 2019 22 26-29
Nemanja Mati? (Chelsea) 2019 26 26-29
Robert Lewandowski (Bayern Munich) 2019 26 26-29
Alexandre Lacazette (Lyon) 2018 24 26-29
Thomas Muller (Bayern Munich) 2019 25 26-29
Manuel Neuer (Bayern Munich) 2019 29 25-28
Mesut Ozil (Arsenal) 2018 26 25-28
Gonzalo Higuaín (Napoli) 2018 27 25-28
Ross Barkley (Everton) 2018 21 25-27
Yaya Toure (Manchester City) 2017 32 25-27
Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal) 2018 21 25-27
Jerome Boateng (Bayern München) 2018 26 24-26
Santi Cazorla (Arsenal) 2017 30 24-26
Danny Welbeck (Arsenal) 2019 24 24-26
Jordan Henderson (Liverpool) 2020 24 24-26
Aaron Ramsey (Arsenal) 2019 24 23-26
Miralem Pjanic (Roma) 2018 25 23-26


Marehemu Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ enzi za uhai wake.
MSANII mkongwe wa filamu nchini, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’ amefariki dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwake Tandale jijini Dar es Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.
Mwili wa Mzee Kankaa amezikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Ali Maua jijini Dar es Salaam.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya miaka mitatu. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tandale-Chama jijini Dar.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!


Liverpool wameafikiana dili ya kunsaini Kijana wa Miaka 22 anaecheza kama Straika wa Burnley iliyoporomoka Daraja kutoka Ligi Kuu England licha ya Klabu hiyo kuigomea ofa ya Liverpool.
Danny Ings, anaechezea Timu ya Taifa ya England ya U-21, anamaliza Mkataba wake na Burnley mwishoni mwa Mwezi huu lakini kutokana na umri wake mdogo Kanuni zinaitaka Liverpool kuilipa fidia Burnley.
Liverpool wanatarajia kulipa fidia ya kati ya Pauni Milioni 5 hadi 6 lakini ikiwa Burnley watagoma basi suala hilo litaenda kwenye Jopo litakaloamua idadi inayofaa.
Wakati Burnley imesema itaendelea maongezi na Liverpool, Vigogo hao wa England wametangaza watamsaini Ings Julai 1 baada ya kukubaliana malupulupu yake binafsi na ikiwa Mchezaji huyo atafuzu upimwaji afya yake.

Msimu uliopita, ukiwa ni Msimu wakevwa kwanza kucheza Ligi Kuu England, Ings alipiga Bao 11 katika Mechi 35 alizoichezea Burnley wakati Mastraika wanaotambulika huko Liverpool, Daniel Sturridge, Rickie Lambert, Mario Balotelli na Fabio Borini, wakifunga jumla ya Bao 8 tu huku Raheem Sterling akipiga 7 na Steven Gerrard kufunga 9.
Ings atakuwa Mchezaji wa pili kusainiwa na Liverpool wakati huu baada ya Wiki iliyopita kumpata Mchezaji Huru kutoka Man City James Milner.



  ILE Filamu kubwa iliyoshirikisha wasanii mahiri kutoka Tanzania movie Talent Top Ten 2014 (TMT) ipo tayari na inatarajia kuonyeshwa katika jumba la sinema la Mlimani City Cinema Tarehe 12.June. 2015 ni siku ya Ijumaa na itarfuka kwa siku tatu Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Sinema hiyo ambayo imeshirikisha wasanii wakali wenye elimu ya uigizaji kutoka kwa wakufunzi kutoka Chuo kikuu cha Dar es Salaam imerekodiwa katika viwango vya kimataifa ndio maana inaanza kurushwa katika majumba ya sinema na kuingia sokoni katika Dvd siku ya Jumatatu tarehe 8.June 2015

www.bukobasports.com





Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Watanzania waishio Uholanzi waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili jijini The Hague, Uholanzi, leo Jumatatu Juni 8, 2015.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo na muhtasari wa ziara yake toka kwa Balozi wa Tanzania nchini Uholani Mhe Wilson Masilingi baada ya kuwasili The Hague leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya mafuta ya Shell Bw. Ben van Beurden jijini the Hague, Uholanzi leo Jumatatu Juni 8, 2015.


Manchester United ndio Nambari Wani kwa kuwa ndio bidhaa yenye thamani kubwa zaidi miongoni mwa Klabu za Soka Duniani.
Licha ya kutotwaa Taji lolote Msimu uliopita, Man United imeiengua Bayern Munich na kukamata Nafasi ya Kwanza kwa kuwa ndio Bidhaa ya Biashara yenye thamani kubwa ikikadiriwa kuwa ni Dola Bilioni 1.2 na hii ni kwa mujibu wa takwimu za Washauri mahsusi wa Bidhaa na Fedha, Brand Finance.
Katika Listi iliyotolewa na Washauri hao wa Bidhaa na Fedha, Klabu 6 katika 10 Bora Duniani ni za England.
Barcelona, ambao Juzi Jumamosi walitwaa Kombe la UEFA CHAMPIONS LIGI, wameporomoka Nafasi 2 na sasa wapo Nafasi ya 6.
Msimu 2014/2015 Klabu ya Barcelona imetwaa makombe matatu(Treble) na hapa ni jana wakati wanatembeza makombe hayo Mtaani!Ingawa Magazeti ya Spain yamekuwa yakivutia upande wa Klabu zao na kudai Man United, kwa kukosa Mataji, imepoteza Mashabiki wengi Duniani, Ripoti ya Brand Finance imesema: "Hata kama ripoti hizo za kupoteza Mashabiki itaaminika, Man United bado ina Maelfu ya Washabiki huko India, Kusini Mashariki ya Asia na China, ikijumuisha zaidi ya Nusu Bilioni ya Watu na habari hizo hazijawakimbiza Wadhamini."
Brand Finance imesema kuwa kwa kusaini Dili na Wadhamini kama Chevrolet na Adidas, ambao walisaini nao 2014 kwa Dau la Pauni Milioni 750 kwa Miaka 10, ni vitu tosha kuthibitisha thamani ya Klabu hiyo na kwamba thamini yao itapanda zaidi kama ilivyopanda kwa Asilimia 63 tangu 2014.

KLABU 20 BORANA THAMANI YAKE!
1. Manchester United (England): $1206 Milioni
2. Bayern Munich (Germany): $933 M
3. Real Madrid (Spain): $873 M
4. Manchester City (England): $800 M
5. Chelsea (England): $795 M
6. Barcelona (Spain): $773 M
7. Arsenal (England): $703 M
8. Liverpool (England): $577 M
9. Paris Saint-Germain (France): $541 M
10. Tottenham Hotspur (England): $360 M


Hofu imetanda Russia na Qatar huenda zikapokonywa uwenyeji wa kombe la dunia 2018 na 2022 iwapo ushahidi wa ufisadi utapatikana dhidi yao.
Afisa wa FIFA Domenico Scala ameiambia jarida moja la Uswisi, Sonntagszeitung, kuwa haki ya kuandaa mashindano hayo ya dunia itakuwa katika hatari kubwa iwapo kutaibuka ushahidi wa kutosha kuwa mataifa hayo mawili yalitoa rushwa.
Hata hivyo Scala amekanusha kuwa hadi sasa amepata wala kuona ushahidi wa aina yeyote dhidi ya mataifa hayo mawili.
Scala ambaye anahudumu kama kiongozi wa kamati ya uhasibu na uchunguzi
''iwapo ushahidi utatokea kuwa uteuzi wa mataifa hayo mawili haukuwa wa kweli na haki bila shaka watapokonywa uwenyeji wa mashindano hayo''
"hadi kufikia leo hakuna ushahidi wa kutosha wa kulazimisha hatua kuchukuliwa.''
Hii si mara ya kwanza kwa Scala kutoa onyo hilo

waliotembelea blog