Tuesday, June 9, 2015


Slaven Bilic ameteuliwa kuwa Meneja mpya wa West Ham kwa Mkataba wa Miaka Mitatu.
Bilic, Raia wa Croatia mwenye Miaka 46, anachukua nafasi ya Sam Allardyce alieachia ngazi mwishoni mwa Msimu ulioisha Mei baada ya kuifikisha Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England.
Bilic aliwahi kuichezea West Ham Mechi 54 kati ya Mwaka 1996 na 1997 na kisha kuwa Kocha wa Croatia kwa Miaka 6.

Pia Bilic alizifundisha Klabu za Lokomotiv Moscow ya Urusi na Besiktas ya Uturuki ambayo aliachana nayo Mwezi Mei.
Lakini katika Klabu zote hizo mbili hakuna mafanikio makubwa aliyoyaleta ingawa mwenyewe ameonyesha matumaini makubwa kwa kujiunga na West Ham moja ya Klabu kongwe za Jiji la London.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog