Tuesday, June 9, 2015



Wananchi wa kijii cha Rukoma kata ya Rukoma wakiwa wamekusanyika wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo Bukoba vijijini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.

Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa katika uwanja wa Katoro,kwenye mkutano wa hadhara Bukoba vijijini mkoani Kagera jioni ya leo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongela akizungumza na wananchi na kuwaleza kuwa wasitishwe na mtu yeyote katika suala zima la kujiandikisa," asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini na wala msiogope",alisema Mh.Mongella.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog