Monday, July 20, 2015

Vipindi vya Bongo Star search vimeanza kwenda hewani, na siku ya jana imeruka episode ya kwanza kuonyesha mchujo jinsi ulivyoenda mpaka kubakiwa na Top 6 (pichani) ya washiriki kutoka Mwanza ambayo itajumuika na washindi wa mikoa iliyosalia. Kipindi kitakuwa kinaruka kila siku ya Jumapili, saa tatu kamili kwenye vituo vya televisheni vya Clouds Tv na Star Tv na marudio yake; Kwa Clouds Tv ni Jumanne saa tano kamili asubuhi pamja na Alhamisi saa nane kamili mchana; Kwa StarTV ni Alhamisi saa tisa na nusu mchana.



David de Gea Manchester United

Usajili wa kipa Mhispania David De Gea kuelekea klabu ya Real Madrid kwa sasa inaonekana kama huenda usitokee tena hivi karibuni baada ya klabu hii ya Hispania na wenzao wa Manchester United kushindwa kufikia makubaliano .
Manchester United imegoma kabisa kufanya mazungumzo na Real kuhusiana na De Gea kutokana na Wahispania hao kushindwa kutimiza masharti ambayo United imeyaweka katika mazungumzo hayo .
United imewaambia Real kuwa endapo wanamtaka De Gea basi wakubali kumruhusu beki Mkongwe Sergio Ramos ajiunge na United au Gareth Bale jambo ambalo vijana hawa wa Florentino Perez amelikataa katakata.
Tayari Real Madrid imesajili kipa Kiko Castilla ambaye amejiunga tokea Real Sociedad huku Keylor Navas akichukua mikoba ya kipa namba moja baada ya gwiji Iker Casillas kuondoka ambapo amejiunga na Fc Porto .
Real Madrid kwa muda mrefu wamekuwa wakimtaka David De Gea ambaye wamepanga kumfanya mrithi rasmi wa Iker Casillas huku United ikigoma kabisa kuzungumza dili yoyote inayomhusu De Gea.
Vyanzo vingine vya habari vimesema kuwa Real Madrid inajiandaa kusubiri mpaka mwishoni mwa msimu huu mpya wakati ambapo mkataba wa De Gea utakapokuwa unamalizika na kumfanya kipa huyu kuwa mchezaji huru hali itakayowafanya Real wamsajili bure



1280px-Flag_of_FIFA.svg

Ikiwa imepita miezi miwili tangu rais wa Fifa Sepp Blatter alipotangaza kuiacha wazi nafasi yake baada ya  kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Fifa , shirikisho hilo limetangaza tarehe ya uchaguzi wake mkuu utakaofanyika kujaza nafasi ya Blatter.
Uchaguzi huo sasa utafanyika tarehe 26 mwezi Februari mwaka 2016 kwenye makao makuu ya Fifa huko nchini Uswisi na tayari watu kadhaa wameanza kutajwa kama vinara wa mbio za kumrithi kiongozi huyu ambaye amekaa muda mrefu .
Rais wa sasa Sepp Blatter alijiuzulu siku mbili baada ya kuchaguliwa tena kufuatia shinikizo lililotokana na kashfa ya rushwa ndani ya Fifa.
Rais wa sasa Sepp Blatter alijiuzulu siku mbili baada ya kuchaguliwa tena kufuatia shinikizo 
lililotokana na kashfa ya rushwa ndani ya Fifa.
Moja ya majina yanatotajwa kuongoza mbio za kurithi mikoba ya Blatter ni jina la rais wa sasa wa shirikisho la soka barani ulaya UEFA Michel Plattini ambaye amekuwa na azma ya muda mrefu ya kuwania urais wa Fifa na alilazimika kujitoa kwenye uchaguzi wa mwaka huu baada ya kutambua kuwa hana nafasi ya kushinda mbele ya Blatter .
Mgombea amnaye aliingia mpaka kwenye hatua ya mwisho ya uchaguzi wa mwaka huu Prince Ali Bin Hussein naye anatajwa kuwemo kwenye mbio hizi japo hakuna yoyote kati ya wawili hawa ambaye amethibitisha kuwania nafasi ya Urais wa Fifa .
Rais wa sasa Sepp Blatter aliwashtua wengi baada ya kutangaza kujiuzulu wadhifa wake zikiwa zimepita siku mbili tangu alipochaguliwa kwa kura nyingi katika uchaguzi ulihusisha wagombea wawili pekee .
Blatter aliamua kung’atuka kutokana na shinikizo kubwa juu ya Fifa lilitokana na kashfa ya uozo wa matumizi mabaya ya madaraka na ofisi pamoja na kashfa ya rushwa ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikifanyiwa upelelezi unaongoza na FBI toka nchini Marekani .

Makamu wa rais wa Fifa Prince Ali Bin Hussein na rais wa UEFA Michel Plattini wametajwa kuwa vinara wa mbio za kurithi nafasi ya Sepp Blatter.
Makamu wa rais wa Fifa Prince Ali Bin Hussein na rais wa UEFA Michel Plattini wametajwa kuwa vinara wa mbio za kurithi nafasi ya Sepp Blatter.




bayern-munich-team-2015-photo-1024x576

Taarifa za usajili ndio kitu ambacho kimekuwa kikitengeneza headlines nyingi kwenye vyanzo vya taarifa za kimichezo hususan mchezo wa soka barani ulaya na mojawapo kati ya taarifa ambazo leo (alhamis) zimeonekana kuwavuta wengi ni hii hapa .
Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wamefikia makubaliano na klabu ya Juventus juu ya usajili wa kiungo hodari raia wa Chile Arturo Vidal ambapo kiungo huyo sasa anatarajiwa kujiunga na wababe hawa siku chache zijazo .

Kiungo wa Chile Arturo Vidal amesajiliwa na Bayern Munich na atatambulishwa siku chache zijazo.
Kiungo wa Chile Arturo Vidal amesajiliwa na Bayern Munich na atatambulishwa siku chache zijazo.
Ripoti nchini Italia zinasema kuwa Bayern imekubali kulipa paundi milioni 40 kwa ajili ya kiungo huyo tegemeo ambaye ataingia Bayern kuziba pengo la kiungo mkongwe Bastian Shcweisteiger ambaye amesajiliwa na Manchester United .
Arturo Vidal aliwahi kucheza nchini Ujerumani kwenye klabu ya Bayer Leverkusen na aliwahi kuingia makubaliano ya kujiunga na Bayern Munich miaka kadhaa iliyopita lakini makubaliano hayo hayakutimia .


nuhu
Bado kuna hali ya sintofahamu miongoni mwa uhusiano uliopo kati ya Shilole na Nuhu Mziwanda.
Shilole amesema kwa sasa wamegombana na hatarajii kuachia wimbo na mwenzake huyo ambaye walipanga kutoa wimbo..amesema mtu akizungua na yeye anamzingua..
Amesema Nuhu amekua na wivu sana wakati yeye anaangaika kutafuta pesa..ila amesema akijua alipokosea atamsamehe ila akizingua anatafuta mtu mwingine.
Nuhu Mziwanda amesema sio kwamba wanapromote wimbo na sasa hana muda na Shilole…wana siku kama tatu tangu wagombane.



louis-van-gaal-manchester-united_1sjazi885y191peieecz900kg

Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal amezoeleka kuwa aina ya kocha ambaye hapendi masikhara toka kwa wachezaji wake na amekuwa si mzito kufanya maamuzi ya kumuondoa mtu kwenye timu pale ambapo anaona anakwenda kinyume na matarajio yake .
Hilo lilidhihirika siku chache zilizopita wakati ambapo kocha huyo alipotangaza wazi kuwa na mpango wa kumuuza kipa namba mbili Victor Valdez kutokana na kushindwa kuendana na falsafa zake .
Van Gaal alisema wazi kuwa Valdez hana maisha ndani ya United kwa sababu alionyesha kwenda kinyume na maelekezo ya kocha wake wakati alipokataa kucheza mechi za kikosi cha wachezaji wa akiba .
Kipa wa Manchester United Victor Valdez amewekwa kwenye orodha ya wachezaji wanaouzwa kwa kukiuka maagizo ya kocha Louis Van Gaal.
Kipa wa Manchester United Victor Valdez amewekwa kwenye orodha ya wachezaji wanaouzwa kwa kukiuka maagizo ya kocha Louis Van Gaal.
Valdez alijiunga na Manchester United baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda wa zaidi ya miezi sita akiwa anauguza jeraha la goti na Van Gaal alimpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake ndani ya United msimu uliopita .
Waandishi wa habari walimhoji Van Gaal kwanini Valdez hajaambatana na wachezaji wenzie kwenye ziara ya klabu hiyo nchini Marekani na jibu la kocha huyo lilikuwa jepesi , kipa huyo hana nafasi kwa kuwa ameonyesha ukaidi .
Kwa sasa United bado iko kwenye harakati za kusaka kipa namba moja kufuatia mpango uliopo wa kipa wake namba David De Gea kujiunga na Real Madrid
KIPA wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Mwameja Mohamed Mwameja aliyewika Simba SC, amesema kwamba ukipa si ‘lele mama’.
Mwameja aliyewahi pia kudakia Ndovu ya Arusha na Coastal Union ya Tanga, amewataka makipa kujituma na kuzingatia nidhamu kwenye fani hiyo ili kufikia mafanikio.
Mwameja ambaye alipewa jina la Tanzania One kwa umahiri wake wa kusimama imara langoni amekiri kuwa kuna magolikipa wengi wa sasa ambao hawajitumi kama ipasavyo na hivyo kuleta mafanikio kwenye klabu zao na Taifa kwa ujumla.
Mwameja amefanya mahojiano na tovuti ya Simba SC na kusema kwamba nidhamu na kujituma ndio siri ya mafanikio yake alioyapata wakati akiwa Simba.
Pamoja na kustaafu tangu mwaka 2002, lakini Mwameja ameendelea kudakia timu za maveterani ili kulinda utimamu wake wa mwili

“Nafasi hii ya kuwa mlinda mlango inahitaji umakini wa hali ya juu sana, kujituma na nidhamu jambo ambalo mpaka sasa bado walinda mlango wengi wanakosa sifa na tunu hizo muhimu katika soka,”amesema Mwameja aliyewahi pia kudakia Reading ya England.
Kwa upande mwingine Mwameja ambaye anashiriki mafunzo ya Makocha wa makipa ya FIFA yanayofanyika uwanja wa Karume yalioandaliwa na TFF, ameushukuru uongozi wa Simba kwa kutambua umuhimu wake na kumuwezesha kushiriki kozi hiyo ambayo kwa mara ya kwanza inafanyika hapa Tanzania.
“Unajua ujuzi hauozi, mafunzo ninayoyapata hapa kwa hakika yananiongezea uwezo mkubwa sana tofauti na uzoefu wangu na kufanya kazi kwa mazoea. Kwa kweli Simba naishukuru sana kwa maamuzi yake haya ya busara ya kuniwezesha kushiriki mafunzo haya yanayofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania,”. 
“Mimi ni mtu ninayeamini sana kwenye kujenga urithi kwa vijana na naamini kuwa ujuzi nitakaoendelea kuupata hapa, nitautumia kujenga makipa imara wa nchi hii,” alisema Mwameja, aliyezaliwa Desemba 21, mwaka 1964 Mwakidila mkoani Tanga. 

waliotembelea blog