Tuesday, August 25, 2015

Klabu ya Juventus ya Italia bado inaongeza nguvu katika kikosi chake kwa kusajili wachezaji kadhaa ili kuweza kuendana na kasi ya michuano mbalimbali itakayoshiriki msimu huu. Juventus ambayo imeondokewa na nyota kadhaa kikosini mwake ikiwemo Carlos Tevez na Andre Pirlo imeongeza nguvu katika kikosi chake.
2BA4773D00000578-3209576-image-a-1_1440491596620
Juventus August 25 wamekamilisha usajili wa mkopo kwa muda wa msimu mmoja wa aliyekuwa winga wa klabu ya Chelsea Juan Cuadrado ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2015 akitokea katika klabu ya Fiorentina ya Italia.
Pichaz Juan Cuadrado alivyowasili Italia August 24 kabla ya August 25 kutangazwa kusajiliwa

2BA2EA5500000578-0-image-a-83_1440458491736

Mshambuliaji Pape Abdoulaye N'Daw mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kutua leo usiku kutoka Dinamo Bucuresti ya Romania kufanya majaribio Simba SC 

SIMBA SC imeachana na Msenegali, Papa Niang baada ya kumjaribu kwa dakika 45 tu jana katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Hawajachoka, Simba SC leo wanatarajia kupokea wachezaji wawili wengine wa kigeni kuwafanyia majaribio, ambao ni Msenegali Pape Abdoulaye N'Daw na Mmali.
N'Daw mwenye umri wa miaka 21, kwa sasa anachezea klabu ya Liga I ya Romania, Dinamo BucureÈ™ti, wakati wa Mali bado jina lake halijapatikana na haijulikani anatoka timu gani. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba wachezaji hao watafanyiwa majaribio na atakayevutia zaidi, ndiye atapewa Mkataba. 
Niang alikuja SImba SC baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Kevin Ndayisenga juu ya dau la usajili.
Niang kutoka klabu ya Alianza F.C. ya El Salvador ambaye ni mdogo wa mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Senegal, Mamadou Niang jana alishindwa kabisa kuwashawishi wana Simba kwa soka yake.
Papa Niang amerejea kwao baada ya 'kuchemsha' jana katika mchezo wa kiraiki na Mwadui

Mchezaji huyo wa zamani wa CF Mounana ya Gabon, Al Shabab SC ya Kuwait, FC Vostok ya Kazakhstan, FF Jaro, AC Oulu na FC OPA za Finland alitarajiwa kuondoka usiku wa jana kurejea kwao, ikiwa ni baada ya siku tatu za kuwa Dar es Salaam.
Awali Simba SC pi ilishindwa kumsajili mshambuliaji mwingine hatari wa Vital’O, Laudit Mavugo kufuatia klabu mbili za nchini humo kupandisha thamani ya mchezaji huyo na kuwa Sh. Milioni 200, badala 110 walizokubaliana awali.
Aidha, kuibuka pia kwa mzozo mpya kati ya klabu ya Vital’O FC na Solidarity FC, inayodai kumlea Mavugo na kudai ina hakimiliki ya mchezaji huyo nako kuliishitua Simba.
Vital’O ikaikoroga zaidi Simba SC baada ya kudai kiwepo kipengele cha wao kupata asilimia 50 kama mchezaji huyo atauzwa na Wekundu hao wa Msimbazi kwenda klabu nyingine.   


Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
ALIYEKUWA kipa wa Simba SC kwa misimu mmoja nusu uliopita, Ivo Philip Mapunda (pichani kushoto) amesema anarejea Kenya, baada ya kuachwa na klabu hiyo mapema mwezi huu.
Ivo aliyewahi kudakia pia Yanga SC, amesema hana kinyongo na Simba SC na anaondoka nafsi yake ikiwa safi kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine.
“Nawashukuru mashabiki wa mpira haswa wa Simba kwa kuwa nami kipindi chote, nilipofanya vibaya na nilipowaudhi mlikuwa nami na ndiyo soka ipo hivyo,”amesema.
Ivo Ameongeza; “Maisha yana changamoto na ndiyo nimezipata kwa sasa Simba baada ya watu fulani kufanya hivyo, ila naamini maisha ni popote na Mungu ndiye kila kitu,”.
Ivo amesema kwamba anarudi Kenya ambako bado anakubalika na anaamini atapata timu.
Ivo alijiunga na Simba SC Desemba 2013 akitokea Gor Mahia ya Kenya katika cha mwaka mmoja na nusu wa klabu hiyo ya Msimbazi, ameidakia jumla ya mechi 39 na kufungwa mabao 25, akiiwezesha timu hiyo kutwaa taji moja, Kombe la Mapinduzi.
Ivo Mapunda akipongezwa na wenzake Januari mwaka huu baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa Kombe la Mapinduzi Uwanja wa Amaan, Zanzibar

Zaidi Ivo aliwafurahisha mno wana Simba kwa kulinda vyema lango kwenye mechi dhidi ya mahasimu, Yanga SC na kwa kipindi chake chote Wekundu wa Msimbazi hawajapoteza mechi dhidi ya watani wao hao.
Alianza na mechi ya Nani Mtani Jembe mwaka juzi, Simba ikishinda 3-1, akadaka mechi ya Ligi Kuu, timu hizo zikitoka sare ya 1-1 kabla ya Desemba mwaka jana kuiongoza tena timu hiyo kushinda mechi ya Nani Jembe 2 mabao 2-0 na mechi yake ya mwisho ya watani kudaka, Wekundu wa Msimbazi walishinda 1-0 katika Ligi Kuu.
Ivo Mapunda ameondoka Simba SC baada ya mechi 39, akifungwa mabao 25

REKODI YA IVO MAPUNDA SIMBA SC

Simba 3-1 Yanga (Nani Mtani Jembe, alifungwa moja Dar)
Simba SC 1-0 AFC Leopard (Mapinduzi, hakufungwa Zbar)
Simba SC 0-0 KCC  (Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 Chuoni (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-0 URA (Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 0-1 KCC (Fainali Kombe la Mapinduzi, alifungwa moja)
Simba SC 1-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu Bara hakufungwa)
Simba SC 4-0 JKT Oljoro (Ligi Kuu Bara, hakufungwa)
Simba SC 1-1 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Mgambo JKT (Ligi Kuu Bara, alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Coastal Union (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 1-2 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
Simba SC 1-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Ashanti United (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 1-1 Yanga SC (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 0-3 ZESCO United (Simba Day, alifungwa mbili Dar)
Simba SC 2-1 Kilimani City (kirafiki Zanzibar, hakufungwa)
Simba SC 2-0 Mafunzo (kirafiki Zanzibar, hakufungwa )
Simba SC 5-0 KMKM (Kirarfiki, Zanziabr hakufungwa)
Simba SC 3-0 Gor Mahia (Kirafiki, Dar es Salaam, hakufungwa)
Simba SC 0-1 URA (Kirafiki, Dar es Salaam alifungwa moja) 
Simba SC 2-2 Coastal Union (Ligi Kuu, alifungwa mbili)
Simba SC 1-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-4 Mtibwa Sugar (Kirafiki Chamazi, alifungwa nne)
Simba SC 2-0 Yanga SC (Nani Mtani Jembe, hakufungwa)
Simba SC 3-1 Mwaduni FC (Kirafiki, Taifa alifungwa moja)
Simba SC 0-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu Taifa, alifungwa moja)
Simba SC 0-0  Mtibwa Sugar (aliingia dakika ya 90 Simba ikashinda penalti 4-3 Fainali Kombe la Mapinduzi)
Simba SC 2-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu, alifungwa moja)
Simba SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-0 Polisi Moro (Ligi Kuu, alidaka kipindi cha kwanza akaumia na kutoka bila kufungwa) 
Simba SC 0-1 Stand United (alifungwa moja)
Simba SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 1-0 Yanga SC (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 1-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 0-2 Mgambo Shooting (Ligi Kuu, alifungwa moja akatolewa kwa kadi nyekundu kipindi cha pili)
Simba SC 4-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 3-0 Ndanda FC (Ligi Kuu, hakufungwa)
Simba SC 2-1 Azam FC (Ligi Kuu, alifungwa moja).
Ivo Mapunda wakati anasaini Simba SC Desemba mwaka juzi mjini Nairobi

aiyolacoverfinal (1)
Diamond Platnumz ameamua kumtambulisha msanii wake wa kwanza mtu wangu kutoka kwenye lebo yake ya WCB,msanii huyu anaitwa Harmonize na hii ni singo yake ya kwanza inaitwa Aiyola,ukiisikiliza unaweza kuandika comment hapo chini.
Klabu ya soka ya Simba mwishoni mwa wiki iliyopita ilimleta mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papa Niang ambaye ni ndugu wa damu na Mamadou Niang mchezji aliyetamba katika vilabu kadhaa barani Ulaya ikiwemo timu ya taifa ya Senegal.
DSC_9335
August 24 Papa Niang alijaribiwa na wekundu hao wa msimbazi katika mechi ya kirafiki ya Simba dhidi ya Mwadui FC ya Shinyanga inayofundishwa na kocha Jamhuri Kiwelo, taarifa zilizotoka ni  kuwa Niang hajafanya vizuri majaribio ya Simba hivyo August 25 inaleta msenegal mwingine kuja kumfanyia majaribio.
Taarifa zinaeleza Simba inamleta Abdulah Ndow kutoka Senegal ila analetwa na wakala aliyemleta kocha wa Simba Dylan Kerr, msenegal huyo anayekuja Simba inadaiwa ameshawahi kucheza Ulaya katika klabu ya Bucharest ila alivunja mkataba baada ya kutolipwa fedha anazodai.

EL 1Mgombea Urais wa UKAWA 2015 Edward Lowassa alianza ziara ya kuingia mitaani Dar es salaam Aug 24 2015 ili kukutana na Wananchi uso kwa uso na kusikiliza matatizo yao.
 Lowassa amesema atatusaidia, tuna furaha sana leo ametutembelea, hatukutarajia,” alisema mwanafunzi wa Shule ya Nyegulu, Dorcus Wilson baada ya kuzungumza na Lowassa.

Mwanafunzi mwingine wa Shule ya Msingi Maarifa, Grey Issa alisema amefurahi kumuona Lowassa kwa sababu amekuwa akimwona kwenye televisheni. Alisema kero yao kubwa ni unyanyasaji wanaoupata kutoka kwa makondakta wa daladala.

Baadhi ya wananchi walisema Lowassa ndiye rais wao mtarajiwa kwa sababu haijawahi kutokea kwa kiongozi yeyote mkubwa kufika kwenye makazi yao na kuzungumza nao... 

“Lowassa ndiye rais wetu. Ni mtu muhimu sana, amefika kwetu na kuzungumza na sisi. Angekuwa ni kiongozi mwingine angefika hapa na walinzi wengi,” alisema Augustino Nyembo, mkazi wa Gongo la Mboto.

Ilipotimu saa 2.35 asubuhi, waziri mkuu huyo wa zamani, aliingia kwenye daladala lililofika kituoni hapo kupakia abiria na kusafiri nalo kwenda Chanika. Baadhi ya abiria walistaajabu kumuona akiingia kwenye daladala hilo na baadhi yao waliteremka kwa mshangao.

Ndani ya daladala hilo, Lowassa aliketi kiti kimoja na mwanafunzi na muda wa kulipa nauli ulipofika, kondakta alisema; “Kwa kuwa wewe ni rais mtarajiwa sitakutoza nauli, utapanda bure”, ombi ambalo mgombea huyo alilikataa.

Lowassa alitoa noti ya Sh2,000 na kumtaka konda achukue nauli yake, pia akate ya mwanafunzi aliyekaa naye. Kondakta alichukua fedha hizo na hakurejesha chenji ya Sh1,400 wala kudaiwa. Watu wengine waliokuwa wameongozana naye katika daladala hilo walijilipia nauli ya Sh400 kila mmoja kutoka Gongo la Mboto mpaka Chanika.

Kondakta huyo, alimweleza Lowassa kuwa tatizo kubwa wanalolipata katika kazi yao ni kutokuwa na mikataba ya kazi na kwamba wanaweza kufukuzwa muda wowote bila kuwa na utetezi wa namna yoyote.

Mgombea huyo wa urais, pia alizungumza na wananchi eneo la Chanika na kuwasikiliza kisha kuendelea na ziara yake kuelekea Mbagala kwa kutumia gari lake.

Bodaboda wajiunga na msafara
Wakati msafara wa Lowassa ukielekea Mbagala, baadhi ya waendesha bodaboda waliufuata hadi uliposimama kwa ajili ya kujaza mafuta eneo la Kajiungeni.

Mmoja wa vijana hao, Zawadi Mrutu alisema wanampenda mgombea huyo kwa sababu ni mchapakazi na anaweza kuleta mabadiliko. Alisema hawajapewa fedha kujiunga na msafara wa Lowassa, bali ni mapenzi yao.

Alisema kiongozi wa wajasiriamali hao aliyezungumza juzi kwenye mkutano wa CCM hajui shida wanazozipata barabarani kwani kama angezifahamu... “asingezungumza vile. Hatumtaki tena kwenye chama chetu.”

Kijana mwingine, Ali Kasembo alisema wanachotaka ni mazingira mazuri ya kufanya kazi yao ya kusafirisha abiria. Alisema wamekuwa wakinyanyaswa na askari polisi katika kazi yao kwa madai kwamba wanakiuka taratibu.

“Lowassa ni jembe, namkubali sana. Tunataka atusaidie kupata mazingira mazuri ya kazi ili na sisi tuliojiajiri kwa kazi hii tujisikie huru, siyo kila siku tunakimbizana na polisi,” alisema Kasembo, anayefanya shughuli zake za bodaboda Chanika.

Akiwa Mbagala
Msafara wa Lowassa ulipofika eneo la Rangitatu, Mbagala na wananchi kumbaini, walianza kufuata gari lake huku wakiimba; “pisha, pisha, Rais apite…, pisha, pisha, Lowassa apite…”

Ilipotimu saa 4.05 asubuhi, msafara huo uliingia kwenye Kituo cha Daladala Mbagala Rangi Tatu huku watu wakisukumana kutaka kumuona.

Hata hivyo, Lowassa alipojaribu kuzungumza nao hakusikika kutokana na kelele zilizotawala kituoni hapo.

Baada ya spika kufungwa kwenye gari, mgombea mwenza, Juma Duni Haji alisimama na kusema wamepita kuwasalimia wale ambao wameitwa malofa. Alisema hatazungumza zaidi kwa sababu wataambiwa walifanya mkutano usiotambulika rasmi.

“Leo tumepita kuwasalimia maskini wanaoambiwa ni vibaka, malofa, wapumbavu. Tunaomba mtuache tuendelee na safari, tutakutana Jumamosi,” alisema Duni na kurejea kwenye gari na kuendelea na safari yao.

Mwenyekiti Monduli ahamia Chadema
Wakati huohuo; Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli, Arusha, Reuben Ole Kuney ametangaza kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema.

Ole Kuney ambaye aliwahi kuwa mkuu wa wilaya mbalimbali kabla ya kustaafu, alisema amejiondoa CCM kutokana na kubaini chama hicho kimeshindwa kusimamia taratibu na kanuni zake.

“Mimi kama mwenyekiti wa wilaya anayotoka Lowassa, waziri mkuu wa zamani na mbunge wetu, siwezi kubaki CCM kwani chama kilishindwa kutenda haki katika mambo mengi ikiwamo mchakato wa urais,” alisema.

Katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Elisante Kimaro alisema kamati ya siasa ya chama hicho itakutana Jumatatu kujadili mwenendo wake na kupanga ratiba ya kampeni.


Mshambuliaji mtukutu ambaye amewahi kuvichezea vilabu kadhaa Mario Balotelli ameondoka Liverpool na kurejea katika klabu yake ya zamani ya AC Milan, Balotelli anarudi AC Milan ikiwa ni msimu mmoja umepita toka ajiunge na Liverpool akitokea AC Milan ya Italia kwa dau la pound milioni 16.
2BA42FE500000578-3209049-image-a-14_1440489938281
akiwasili kwa kufanya vipimo vya afya Milan
Balotelli anarudi Italia katika klabu ya AC Milan kwa mkopo wa muda mrefu na tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya na yupo tayari kukitumikia kikosi hicho.
Mshambuliaji huyo wa kiitaliano mwenye asili ya Ghana amerejea AC Milan akiwa na rekodi ya kucheza mechi 16 akiwa na Liverpool na kuifungia goli moja pekee.
2BA4315400000578-3209049-image-m-18_1440489981510
” Nipo fiti nasubiri kufanya mazoezi na timu nina hamasa kubwa ninachotaka ni kufanya kazi na sio kuongea, nilifikiri nitarudi Milan siku moja? ndio siku zote Milan ipo katika moyo wangu na nilikuwa na matumaini kuwa nitarudi siku moja”>>> Balotelli
2BA4B25800000578-3209049-image-a-1_1440496287259
Baada ya kumaliza kufanyiwa vipimo vya afya
45
Rekodi ya Balotelli katika vilabu alivyochezea


Giroud (left) was replaced by Theo Walcott but the England man also failed to hit the back of the net
Henry would also like to see a new midfielder at Arsenal, to help the likes of Aaron Ramsey 
Jamie Carragher believes that Arsenal boss Arsene Wenger has had three years to address these issues


Omar Wayne (aliyeruka juu) amepelekwa kwa mkopo Majimaji ya Songea
MAJIMAJI ya Songea mkoani Ruvuma imesajili wachezaji wawili wa Azam FC kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu- beki Ismail Gambo ‘Kussi’ na kiungo Omary Wayne.
Wawili hao matunda ya akademi ya mabingwa hao wa Afrika Mashariki na kati tayari wamesafiri kwenda Songea kujiunga na Majimaji iliyorejea Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu.
Wawili hao wanafanya idadi ya wachezaji watatu ndani ya wiki moja kutolewa kwa mkopo Azam FC, baada ya winga Joseph Kimwaga kupelekwa Simba SC jana.


KIPA anayeonekana kuwa bora zaidi kwa sasa, Aishi Manula (pichani kushoto) wa Azam FC ameachwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichopo kambini Uturuki. 
Taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto, imesema kwamba Aishi Manula hakuweza kusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga SC Jumamosi.
Yanga SC ilishinda kwa penalti 8-7 mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya sare ya 0-0 na Aishi alimaliza mechi yote.
Wachezaji 21 wapo kambini Uturuki chini ya kocha Mkuu Charles Boniface Mkwasa, Msaidizi wake, Hemed Morocco, kocha wa makipa Manyika Peter na Mshauri wa Ufundi, Abdallah Kibadeni.
Wachezaji wa Taifa Stars wakifanya mazoezi leo mjini Kartepe, Uturuki

Hao ni makipa Ally Mustafa ‘Barthez’, Said Mohamed, mabeki Juma Abdul, Shomari Kapombe, Mwinyi Haji Mngwali, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka, Abdi Banda, Kelvin Yondani na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Viungo ni Frank Domayo, Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Telela, Said Ndemla na washambuliaji ni Simon Msuva, Deus Kaseke, John Bocco, Rashid Mandawa, Farid Musa na Ibrahim Hajibu. 
Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na Libya usiku wa ijumaa kwenye moja ya viwanja vilivyopo hoteli ya Green Park mjini Kartepe, Uturuki.
Taifa Stars na Libya zote zimeweka kambi katika hoteli hiyo kujiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika na usiku wa Ijumaa zitamenyana katika mchezo wa kirafiki.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa anatarajiwa kuutumia mchezo huo kukipima kikosi chake kwa mara ya kwanza humo, baada ya mazoezi ya siku nne.
Mkwasa amesema huduma na vifaa vilivyopo katika hoteli waliyofikia (viwanja, gym) wanavyotumia kwa ajili ya mazoezi ni vizuri, hivyo ratiba yake ya mazoezi inakwenda kama alivyopanga katika maandalizi ya wiki moja ya kuajiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.



Manchester United wameripotiwa kutoa Ofa inayokaribia Pauni Milioni 140 kumnunua Straika wa Barcelona ambae ni Kepteni wa Brazil, Neymar, kwa mujibu wa Chombo cha Habari cha huko Brazil Globo Esporte.
Inaaminika Mkataba wa Barcelona na Neymar, mwenye Miaka 23, una kipengele kinachotaka Mabingwa hao wa Spain walipwe Dau la Pauni Milioni 140 ikiwa atataka kuhama kabla Mkataba kumalizika.

Globo Esporte ndicho Chombo cha Habari cha kwanza kutoboa Mwezi uliopita kwamba Mbrazil Roberto Firmino yupo njiani kujiunga na Liverpool na kitu hicho kikatokea kweli.
Habari hizo kutoka Brazil pia zimedai Neymar yeye hana kipingamizi chochote cha kucheza England na hasa Man United ambayo anaiona ni Klabu kubwa Duniani na yenye historia iliyotukuka.

Hapo Jana, mara baada ya Barcelona kuifunga Athletic Bilbao Bao 1-0 katika Mechi yao ya kwanza kabisa ya La Liga katika Msimu huu mpya, Kocha wao Luis Enrique alikataa kuongea lolote kuhusu uvumi huu.
Hiyo Jana Neymar hakucheza Mechi hiyo kwani alikuwa mgonjwa na alianza tena mazoezi hivi Juzi tu.
Mapema kwenye Dirisha la Uhamisho hili, Meneja wa Man United Louis van Gaal aliwahi kudokeza wao wanaweza kuleta maajabu katika Soko la Uhamisho.
Mwezi Julai, wakiwa Ziarani huko USA, Van Gaal aliwahi kusema kuhusu Straika ambae watamnunua: “Si Straika ambae Vyombo vya Habari vinamzunguzia. Itabidi mkae na kusubiri.”

FULL TIME: ARSENAL 0 vs 0 LIVERPOOL, HAKUNA MBABE EMIRATES!

Kipa Petr Cech ndie aliyeilinda Arsenal usiku huu kutofungwa Alexis Sanchez akijituma
Wakati Liverpool hawajapoteza hata Mechi moja kwenye Ligi Msimu huu baada ya kushinda Mechi 2 na hii Sare na sasa wako Nafasi ya 3 wakifungana na Man United, Arsenal wao wako Nafasi ya 9 wakiwa wamefungwa Mechi 1, Ushindi 1 na Sare 1.
Arsenal walianza Ligi Msimu huu mpya kwa kufungwa Mechi yao ya kwanza 2-0 na West Ham wakiwa hapo Emirates na Wikiendi iliyopita kushinda 2-1 Ugenini walipocheza na Crystal Palace wakati Liverpool wameshinda Mechi zao mbili, kwa Bao 1-0 kila Mechi, walipocheza Ugenini na Stoke City na kisha Nyumbani Anfield na Bournemouth.
Cech akiokoa shuti langoni mwake lililopigwa na Benteke katika kipindi cha kwanza ambapo Arsenal na Liverpool zilibanana na kwenda mapumziko zikiwa 0-0.Ramsey akifanya yake, alifunga bao lakini mwamuzi alidai si bao kwani Ramsey alikuwa Ofsaidi



Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro tayari imewasili salama nchini Uturuki katika mji wa Kartepe - Kocael leo mchana, tayari kwa kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika mwaka 2017.
Msafara wa Taifa Stars uliopoa nchini Uturuki unaongozwa na mjumbe wa kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed Mgoyi ukijumuisha benchi la ufundi 7 na wachezaji 21 umefikia katika hoteli ya Green Park Kartepe, ambapo leo jioni timu inatarajiwa kuanza mazoezi.

Kocha Mkuuu wa Taifa Stars Charles Mkwasa mara baada ya kufika katika eneo la kambi, amesema mazingira ya kambi ni mazuri na sasa vijana watapata nafasi nzuri ya kufanya mazoezi na kujiandaa vizuri kwa mchezo dhidi ya Nigeria.

Mkwasa amesema ana imani yeye na benchi lake la ufundi, wataandaa vijana kufanya vizuri kwa mchezo huo wa Septemba 5, 2015 na kuomba watanzania kuwaspoti katika maandalizi hayo kuelekea kwenye mchezo wenyewe.
Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa, timu itakua ikifanya mazoezi kutwa mara mbili kila siku uwanjani, na kutumia vifaa vya mazoezi viliyopo katika hoteli waliyofikia kuhakikisha timu ikirejea inakuwa katika hali nzuri ya kufanya vizuri zaidi.
Stars inatarajia kucheza michezo miwiliya kirafiki katika wiki moja ya kambi nchini Uturuki, kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kupamabana na Nigeria.


TFF KUMPELEKA MAADILI MWENYEKITI WA UCHAGUZI DRFA

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatarajia kumpeleka katika kamati ya maadili ya TFF Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya DRFA Ndg. Rashid Saadallah siku ya Alhamisi tarehe 27/08/2015 saa 9:00 alasili kwa kosa la kudharahu na kupingana na maagizo ya mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF.

Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya TFF alimwagiza asimamishe uchaguzi wa chama cha mpira wa wilaya ya Temeke (TEFA), ili kuitisha fomu zote za waomba uongozi pamoja na maamuzi ya kamati za TEFA na DRFA ili kujiridhisha kama taratibu zilifuatwa katika mchakato huo kutokana na malalamiko ya baadhi ya wagombea kwamba hawakutendewa haki.

Pamoja na kupata barua hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya TFF aliandika barua ya kukataa kutii maagizo hayo. TFF imechukua hatua hiyo kulinda nidhamu kwa vyombo vilivyo chini ya TFF.

U-15 YAINGIA KAMBINI

Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kimeingia kambini katika hosteli za TFF zilizopo Karume kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya Morogoro (U-15) mwishoni mwa wiki hii.U15 inayonolewa na kocha wake Bakari Shime, ianatarajiwa kucheza michezo miwili na timu ya kombaoni ya Morogoro (U15) siku ya jumamosi na jumapili mjini Morogoro, ambapo kocha huyo amekua akitumia nafasi hiyo kupima uwezo wa vijana wake na kuboresha kikosi kwa kuongeza vijana wengine anaowaona wanafaa katika timu hiyo.TFF imekua na program ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 15 kukutana kila mwisho wa mwezi kwa kambi, kabla ya kusafiri mikoani kucheza michezo ya kirafiki. Mpaka sasa timu hiyo imeshacheza na timuza kombaini za mikoa ya Mbeya na Zanzibar.

Timu hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, inajandaa na kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Madagascar mwaka 2017. IMETOLEWA NA TFF

waliotembelea blog