Friday, January 3, 2014


Uongozi wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi (Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.

Charles Boniface Mkwasa 'Master' aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha msaidizi Fred Felix "Minziro" ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa mwaka 2013.

Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80's kwa kiwango cha hali juu pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya aiwe mgeni katika mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kocha wa makipa wa timu ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" Juma Pondamali "Mensah" anachukua nafasi ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa ambaye pia alistishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.


Pondamali golikipa aliyeichezea Yanga miaka ya 80's kwa kwa kiwango cha hali ya juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika timu ya Young Africans kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi kwa vipindi tofauti.

Dr Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi.

Mara baada ya kuwapata viongozi hao watatu wa Benchi la Ufundi kikosi cha Young Africans kesho kitaanza mazoezi jioni katika Uwanja wa Bora Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya Kimataifa huku kocha Mkwasa akiongoza benchi hilo la Ufundi mpaka atakapopatikana kocha mkuu ambaye watafanya watafanya kazi kwa pamoja.
Mitanage raundi ya tatu ya Kombe la zamani kabisa Duniani, FA CUP, zitachezwa Wikiendi hii, Jumamosi na Jumapili, na hii ndio hatua ambayo Klabu za Ligi Kuu England ndio zinaanza Mashindano haya huku BIGI MECHI ni ile Dabi ya London Kaskazini itakayochezwa Jumamosi Uwanjani Emirates kati ya Arsenal na Tottenham.
Mabingwa wa England, Manchester United, Jumapili watakuwa kwao Old Trafford kucheza na Swansea City na Siku hiyo hiyo Chelsea wako Ugenini kuivaa Derby County na Man City wako Ugenini Siku ya Jumamosi kucheza na Blackburn Rovers.
Jumapili, Liverpool watakuwa Anfield kucheza na Mshindi kati ya Oldham.
Awali kulikuwa na Raundi zilizoshirikisha Timu za Madaraja ya chini na hata Timu ambazo hazipo kwenye Ligi rasmi.

Timu ambazo hazimo kwenye Ligi na ambazo zimetinga Raundi ya Tatu ni pamoja na Grimsby Town, Kidderminster Harriers na Macclesfingeld Town.
RATIBA RAUNDI YA TATU
Mapema JUMAMOSI
15:45 Blackburn v Manchester City
Mechi zote zinazofuata ni Saa 18:00
Bournemouth v Burton
Ipswich v Preston
Grimsby v Huddersfield
Brighton v Reading
Everton v QPR
Bolton v Blackpool
Macclesfield v Sheffield Wednesday
Aston Villa v Sheffield United
Norwich v Fulham
Charlton v Oxford United
Wigan v MK Dons
Rochdale v Leeds
Newcastle v Cardiff
Southampton v Burnley
Stoke v Leicester
Doncaster v Stevenage
Kidderminster v Peterborough
West Brom v Crystal Palace
Middlesbrough v Hull
Southend v Millwall
Bristol City v Watford
Liverpool v Oldham
Yeovil v Leyton Orient
Barnsley v Hartlepool au Coventry
2015 Arsenal v Tottenham
Jumapili Januari 5
1500 Nottingham Forest v West Ham
1700 Sunderland v Carlisle
1715 Derby v Chelsea
1800 Liverpool v Oldham
1800 Port Vale v Plymouth
1930 Manchester United v Swansea

waliotembelea blog