Saturday, September 28, 2013


HUU wimbo hatari tupu.Inaelezea maisha ya Diamond kabla hajatoka kimuziki.Dogo aloimba anadai Diamond ni ndugu yake wa damu na hakumbuki alipotoka.Duuh kaongea mambo mengi sana.Sina mbavu kwa kweli.Isikilize hapa Chini.Ni balaa tupu.Ni bonge moja la Ngoma,AUDIO HII HAPA CHINI

Friday, September 27, 2013

HIVI NDIO HALI YA JENGO LA WESTGATE BAADA LA SHAMBULIO LA AL-SHABAAB...!!




Picha za nje ya jengo la Westgate hazioneshi uhalisia wa hali iliyoko ndani ya jengo baada ya shambulio la kigaidi Jumamosi iliyopita jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70.
a7
Picha hizi zinatoa picha halisi ya jinsi jengo hilo lilivyoharibika vibaya kwa ndani baada ya ghorofa tatu za jengo hilo kudondoka baada ya kupigwa mabomu katika mchakato wa kukabiliana na magaidi.
a6 Hivi ndivyo jengo la West gate linavyoonekana kwa nje

Picha hizi pia zinaonesha jinsi magari yaliokuwepo eneo la maegesho ya magari katika jengo hilo yakiwa yameharibiwa kiasi kwamba kuna mengine ambayo huenda hata wamiliki wanaweza kushindwa kuyatambua.
a1
a2
a3
a4
a5
a8
a9 Picha: Nairobi Wire, Mail Online

Wednesday, September 25, 2013

UDAKU WA USAJILI
article-2424444-1BE2CFB3000005DC-104_634x970
Winga wa nchi ya Wales Gareth Bale, 24, 
alipanda ndege kurudi toka Hispania na kuzungumza na
  Manchester United kabla ya kukamilisha uhamisho 
wake wa kuvunja rekodi wenye thamani ya £86m kwenda Real Madrid.
 431174_526661757361058_2029326973_n
Manchester United, Chelsea, Arsenal na 
Tottenham wanaweza kuhusishwa na wasiwasi wa
 hatma ya Andrea Pirlo akiwa Juventus
. Kiungo huyo Muitaliano, 34, anaweza kuruhusiwa
 kuondoka mwezi januari endapo Klabu
 hiyo yaya jijini Turin haitamwongezea mkataba.
 Valais Cup 2013 - OM-FC Porto - 20130713 - Eliaquim Mangala
Chelsea wanataka kumsajili Beki 
wa Porto Eliaquim Mangala, 22, katika dirisha
 la usajili la mwezi Januari. Klabu ya Monaco
 pia wameonyesha nia ya kutaka
 kumsajili Beki huyo wa kati wa Kifaransa.
 rafael
Beki wa Manchester United Rafael,23, 
anafikiria kurudi Brazil, akiwa na  Corinthians
 klabu ambayo Beki huyo wa kulia anaweza kuhamia.
 César_Azpilicueta_Chelsea_vs_AS-Roma_10AUG2013
Athletic Bilbao wameonyesha nia ya kutaka 
kumsajili beki wa Chelsea Cesar Azpilicueta
 mwezi Januari. Beki huyo wa Kihispania, 24,
 amecheza mechi moja tu akitokea benchi msimu huu.
 hinteregger060312apa726
Arsenal na Juventus wameonyesha kuvutiwa na
 Beki wa Red Bull Salzburg mwenye
 asili ya Austria Martin Hinteregger, 21.
UDAKU MWINGINE
article-0-07418B06000005DC-80_306x395
Meneja wa zamani wa  Brighton Gus Poyet amefanya
 mazungumzo na Mmiliki wa Sunderland Ellis 
Short kuhusu kuwa mbadala wa
 Paolo Di Canio ndani ya dimba la Stadium of Light. Steve McClaren na 
Tony Pulis pia wako katika mbio za kugombania hiyo kazi.
 Manchester City v Liverpool - Premier League-1572822
 Kocha wa zamani wa Manchester City  
Roberto Mancini yupo kayika nafasi nzuri kuwa
 mbadala wa Fatih Terim ndani ya Galatasaray.
 Chris-Hughton-Norwich-2012
Meneja wa Norwich Chris Hughton anaweza
 kufukuzwa kazi ikiwa timu yake itafungwa na Stoke Jumapili.
 FBL-FRA-LIGUE1-PSG-BREST
Mshambuliaji wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 31
, atakuwa anapata mshahara wa jumla ya kitita cha
 £12.6m kwa mwaka, badala ya mshahara wa £11.6m,
 baada ya kuongeza mkataba na Paris St-Germain.
luis-suarez-celebrates-at-anfield-620-987991160
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers amesema hatasita
 kumtumia Mshambuliaji Luis Suarez dhidi ya
 Manchester United ndani ya  Old Trafford siku ya
 Jumatano baada ya kufungiwa mechi kumi.
 Cristiano-Ronaldo-celebrates-a-goal-with-team-mate-Gareth-Bale-2281212
Gareth Bale amepanga kwenye nyumba ya Kaka nchini 
Hispainia. Real Madrid walimpatia Bale mkataba wa
 makubaliano na Kiungo huyo wakibrazili, 31, ambaye amerudi AC Milan.
 
MCHUNGAJI Ambilikile Mwaisapila wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) amesema Mungu ameendelea kujifunua kwake na kumuonyesha kuwa Tanzania itakuwa kioo cha Afrika na baadaye kioo cha dunia.

Ametoa kauli hiyo jana asubuhi (Jumanne, Septemba 24, 2013) mbele ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Samunge, wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakati msafara wa Waziri Mkuu uliposimama nyumbani kwake ili kumsalimia akiwa njiani kurejea mjini Arusha.

Mchungaji Mstaafu Mwaisapila maarufu kama Babu wa Samunge alisema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa kwenye Biblia lakini hayakutokea Israeli na sasa yatafanyika hapa Samunge. “Mungu ametupenda sana, yanakuja mambo makubwa na wala hayako mbali. Kama mimi ni mzee na nitayaona, kwa hiyo mtarajie kuwa hayako mbali kutokea,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema katika mafunuo aliyopewa na Mungu ameonyeshwa kwamba watu wengi zaidi watafurika kijijini Samunge kuliko ilivyokuwa hapo awali. Alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa misaada iliyotoa wakati wa ‘kugawa kikombe’ ikiwemo mahema, maji na ulinzi.

Waziri Mkuu ambaye yuko mkoani Arusha kwa ziara maalum ya kusikiliza matatizo ya ardhi yanayowakabili wakazi wa wilaya ya Ngorongoro, katika tarafa za Ngorongoro, Loliondo na Sale alisema anakubaliana na utabiri wa Mch. Mwaisapila kwani Tanzania imejaliwa gesi nyingi na mafuta mengi ambavyo vitabadili sura ya Taifa hili.

“Mungu ametupa gesi nyingi sana, katika miaka miwili tutakuwa na umeme kila mahali. Tuna makaa ya mawe ambayo ni nishati kubwa na sasa tuna fursa ya kupata nishati ya umeme kutoka ardhini (geo-thermal) katika Ziwa Natron,” alisema.

Alisema Tanzania imekuwa kimbilio la kila mwekezaji na sababu kubwa ni amani na utulivu uliopo nchini.

Aliwaeleza wakazi wa Samunge kwamba mapema mwakani mkandarasi wa barabara atakuwa katika eneo lao kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya lami ambapo awamu ya kwanza itaanzia Wasso hadi Mto wa Mbu kupitia Samunge.

Akitoa ombi maalum kwa niaba ya vijana mbele ya Waziri Mkuu, Bw. Elias Kalumbwa alisema wanaomba kuchimbiwa bwawa ili waweze kujiajiri kupitia kilimo cha mbogamboga na matunda.

Bw. Kalumbwa ambaye amesomea masuala ya wanyamapori alisema eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wa msimu unaopita kijijini hapo. “Eneo la kuchimba bwawa lipo katika mto wetu, vijana tunaweza kujiajiri endapo tutapata bwawa ili tufanye kilimo cha umwagiliaji maji,” alisema huku akishangiliwa.

Naye Bibi Martha Sereri (70) alimweleza Waziri Mkuu kwamba wanaomba jimbo la Ngorongoro ligawanywe kwa sababu ni kubwa sana kiasi kwamba inamuwia vigumu mbunge wao kufika maeneo yote. Aliomba pia wapatiwe walimu wa sayansi na hisabati kwa ajili ya shule 10 za sekondari zilizopo kwenye tarafa yao.

Aliomba wapatiwe mikopo ya matreka ili waweze kuongeza ukubwa wa mashamba yao. “Tunaomba mikopo ya matrekta na plau, haya mashamba umeyaona njiani yamelimwa na Wakenya. Ukikodisha trekta kila ekari unatozwa sh. 100,000/-. Je tutafika wapi? Mkitukopesha matrekta mtakuwa mmetusaidia zaidi,” alisema.

Akijibu hoja hizo, Waziri Mkuu alisema hoja zao ni za msingi na kwamba suala la vijana kupatiwa bwawa ni jambo linalowezekana kupitia mipangpo ya maendeleo ya kilimo ya wilaya (DADPS).

“Andaeni andiko lenu, inabidi litoke kwa wananchi na siyo Serikalini. Mkituletea ni jambo linalowezekana kwani liko ndani ya mipango ya wilaya.”

Akijibu hoja kuhusu ukubwa wa jimbo, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao kwamba inawezekana kuongeza jimbo isiwe suluhisho la matatizo yao kwa sababu ya jiografia ya eneo lao.

Kuongeza jimbo inaweza isiwe jibu la kila kitu kwani matatizo mnayopata yanatokana na jiografia ya eneo lenu, kutoka Ngorongoro, Loliondo hadi huku Sale. Mimi nadhani tuangalie pia uwezekano wa kuwapa Halmashauri ili kusogeza huduma kwa wananchi. Tutaangalia njia zote mbili na kuona ipi italeta majibu ya haraka kwenu,” alisema.

Tuesday, September 24, 2013




 

                                               Mwonekano wa  kanisa la ROMANI kahama
                                                              mjini jimbo la NYASUBI







             Hapa waumini wakichoma mailizi


                                         Padri akizungusha SAKARAMENT kwa waumini

                                                                SAKRAMENT








                                                         waumini wakiomba











                                                    sehemu walipochomea ilizi








waliotembelea blog