Thursday, July 9, 2015



BEKI Matteo Darmian atasaini Manchester United baada ya kukubali Mkataba wa miaka minne.
United imekubai kutoa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 12.7 kwa Torino, ambayo inaweza kuongezeka hadi Pauni Milioni 14.4 iwapoa mchezaji huyo atafanya vizuri. 
Klabu ya kwanza ya Darmian, AC Milan pia inatarajiwa kupata Pauni 287,000 kama sehemu ya asilimia tano yao kwa mauzo ya mchezaji huyo. 
Matteo Darmian akiichezea Italia katika mechi ya kufuzu Euro 2016 dhidi ya Bulgaria Machi, mwaka huu
Taratibu za mwisho zilitarajiwa kukamilishwa jana baina ya wanasheria wa pande zote na mchezaji huyo anatarajiwa kutangazwa rasmi leo.
Bei huyo wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 25, anayeweza kucheza kulia na katikati atakuwa mchezaji wa pili kusajiiwa United kuelekea msimu ujao, baada ya Memphis Depay kutoka PSV Eindhoven. 
Depay atatambulishwa katika Mkutano na Waandishi wa Habari kesho.United inahitaji mchezaji anayeweza kucheza kulia baada ya Louis van Gaal kuona Mbrazili, Rafael hawezi kazi hiyo.


Mbunge wa jimbo la Songea Mjini, Dk. Emmanuel John Nchini (kulia), akimkabidhi basi kwa ajili ya klabu ya Majimaji ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, John John Nchimbi (kushoto) leo asubuhi. Dk Nchimbi amemshukuru rafiki yake, Paul Hinks kwa kufanikisha kupatikana kwa gari hilo. Tayari Nchimbo ambaye amekuwa Mbunge wa Songea Mjini tangu mwaka 2010 amesema hatagombea tena katika jimbo hilo.
Rais JK
Stori kuhusu Siasa zinapewa nafasi kubwa sana sasa hivi, Tanzania inaingia kwenye Uchaguzi Mkuu Mwezi October 2015… Tayari wapo waliotangaza Kugombea nafasi mbalimbali lakini macho ya wengi yako kwenye nafasi ya Urais, mpaka sasa kuna majina zaidi ya 35 ya watu waliotangaza Kugombea nafasi ya Urais kupitia CCM.
Rais Kikwete yuko Dodoma, imenifikia hii Ripoti ya kilichoendelea jana wakati wa Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili cha CCM.


KLABU ya BidVest Wits ya Afrika Kusini ambayo hivi karibuni iliwaalika Simon Msuva wa Yanga SC na Jonas Mkude wa Simba SC kwa majaribio, imemsajili winga wa kimataifa wa Msumbiji, Elias Pelembe (pichani) kutoka Mamelodi Sundowns.
Pelembe amemaliza mkataba wake na 'Wabrazil' mwezi uliopita na baada ya kufanya mazungumzo na klabu kadhaa, akaamua kuungana na Gavin Hunt klabu ya Wits.
Klabu hiyo imetweet leo juu ya kumsajili mchezaji huyo na wazi hilo ni pigo kwa Kaizer Chiefs na Orlando Pirates ambazo nazo zilikuwa zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31.
Pelembe alicheza kwa mara ya kwanza chini ya Hunt wakati alipojiunga na SuperSport United msimu wa 2007/2008 akitokea Desportivo Maputo ya Msumbiji.
Alishinda mataji mfululizo na Matsatsantsa kabla ya kuhamia Sundowns mwaka 2009, akiripotiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa zaidi Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Baada ya misimu sita ya wawili hao kuwa tofauti, hatimaye Hunt anakutana tena na Pelembe Wits.
Pelembe, anayecheza kulia, anakuwa winga wa pili kununuliwa na klabu hiyo msimu huu baada ya Daine Klate aliyejiunga na timu hiyo Juni. Klabu hiyo pia imemsajili beki mkongwe Nazeer Allie kutoka Ajax Cape Town.

waliotembelea blog