Tuesday, September 30, 2014


Paris St-Germain watatinga Mechi hii ya Nyumbani kwao ya Kundi F dhidi ya FC Barcelona bila ya Straika wao mahiri Zlatan Ibrahimovic ambae ameumia kifundo cha Mguu.
Katika Mechi za kwanza za Kundi lao, PSG ilitoka Sare na Ajax na Barcelona kuichapa Apoel Nicosia Bao 1-0.

Wakati PSG hawajafungwa hata Mechi moja katika Mechi 9 Msimu huu, ingawa 6 kati yake ni suluhu, Barcelona wamekuwa hatari mno huku Mastraika wao Messi na Neymar wakicheka na nyavu kila mara na Juzi waliibamiza Granada 6-0 huku Neymar akipiga Hetitriki na Messi Bao 2.

Mechi hii inawakutanisha Mameneja wa Timu hizi mbili, Laurent Blanc wa PSG na Luis Enrique wa Barca, ambao waliwahi kucheza pamoja wakiwa Barcelona katika Msimu wa 1996/97 na kuiwezesha kutwaa Kombe la Washindi wa Ulaya, Copa del Rey na Spanish Super Cup.



RATIBA MECHI ZA LEO JUMANNE
Mechi zote kuanza Saa 21:45

Jumanne Septemba 30
KUNDI E
19:00 CSKA Moscow vs Bayern Munich
Manchester City vs Roma

KUNDI F
APOEL Nicosia vs Ajax
Paris St-Germain vs Barcelona

KUNDI G
FC Schalke 04 vs NK Maribor
Sporting Lisbon vs Chelsea

KUNDI H
BATE Borisovs vs Athletic Bilbao
Shakhtar Donetsk vs FC Porto


Dakika ya 15 Peter Crouch aliifungia bao la kwanza la kichwa na kuifanya Stoke City kuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Newcastle baada ya Victor Moses kutoa krosi safi kwa Crouch ambaye ameunga kwa kichwa hadi langoni mwa Newcastle.Kibarua mashakani kwa kocha Pardew! 
Mpaka mapumziko Stoke ndio ilikuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Newcastle United.Ushindi wa kwanza wa Nyumbani kwa Stoke City msimu huu wakimtungua Newcastle, bao likifunhgwa na Peter Crouch kipindi cha kwanza dakika ya 15 kwa kichwa.
Kocha wa Newcastle Pardew akiwa kwenye Mawazo mazito kipindi cha pili na hapa akiwa nyuma ya bao 1-0 kwenye Uwanja wa Stoke City Britannia.VIKOSI:
Newcastle XI: Krul, Janmaat, Coloccini, Williamson, Dummett, Tiote, Colback, Sissoko, Cabella, Gouffran, Riviere
Stoke XI: Begovic, Bardsley, Shawcross, Wilson, Muniesa, Whelan, Nzonzi, Diouf, Adam, Moses, Crouch



Wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Kema Mabango, Abdallah Gunda na Jackson Mmbando wakishiriki katika shindano la kukuna nazi wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Washindi wa shindano la kukuna nazi wakishow love. Kutoka
(kushoto), Mshindi wa Kwanza, Abdallah Gunda, Mshindi wa Pili, Jackson
Mmbando na Mshindi wa Tatu, Kema Mabango.

Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakiogelea wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakishiriki katika michezo wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Wafanyakazi wa Airtel na familia zao wakijisevia maakuli.

Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akiwahudumia chakula wafanyakazi wa Airtel na familia zao.
Airtel Family day yalenga kuongeza hamasa kwa wafanyakazi kujituma katika kazi zao Imeelezwa kuwa ufanisi wa watumishi katika ngazi mbali mbali za kiutendaji unaweza ukaongezeka pindi wafanyakazi wanapokutana pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi wao katika hali ya kiurafiki.

Wednesday, September 24, 2014

Edu Albácar ndie aliyeanza kuifunga Real bao dakika ya 15 bao la mkwaju wa penati.
Gareth Bale hakuchukua muda dakikia 20 alisawazisha bao la hilo kwa kichwa na kufanya 1-1.
Cristiano Ronaldo alifunga bao la pili dakika ya 28 na kufanya 2-1 na baadae dakika ya 32 akaifungia bao tatu na kufanya 3-1 dhidi ya Elche kwenye Uwanja wa Nyumbani Bernabeu na ukishuhudiwa na Mashabiki 65,000.
Bao zote tatu zikifungwa katika kipindi cha kwanza cha dakika 45.
Kipindi cha pili dakika ya 80 Cristiano Ronaldo alifunga hat-rick kwa kufunga bao la nne na kufanya bao kuwa 4-1 dhidi ya Elche.

Ronaldo tena katika dakika za majeruhi alitupia bao lingine la tano na kuhitimisha mpira huo Real wakiwa na bao 5-1 dhidi ya Elche baada ya Ronaldo kupata pasi kutoka kwa Gareth Bale.


Fowadi wa Elce  Edu Albscar akishangilia bao lake la mkwaju wa penati

Bale aliweka sawa mambo kwa kufanya 1-1 nyumbani Bernabeu

Ronaldo akaipachikia bao la pili na kufanya 2-1

Ronaldo akishangilia bao lake la kuhitimisha Hat-trick yake leo hii usiku 
Ronaldo akifunga moja ya bao lake leo hii kwa kichwa

Ronaldo akishangilia bao lake

Sergio Ramos kwenye patashika!

Baadhi ya Wachezaji wa Real wakimpongeza mwenzao Staa Ronaldo


Wachezaji wa Southampton wakipongezana baada ya kuifunga bao la pili Arsenal kwenye Uwanja wao wa Emirates, Bao lililofungwa na Nathaniel Clyne dakika ya 40 kipindi cha kwanza.Nathaniel Clyne akifunga bao la pili.2-1Kipindi cha Kwanza dakika ya 14 Alexis Sánchez aliwapatia bao la kwanza Arsenal kwa frii kiki na kufanya bao kuwa1-0 dhidi ya Southampton.

Dakika ya 20 Dusan Tadic aliisawazishia bao Southampton kwa mkwaju wa penati na kufanya 1-1. Dakika ya 40 Nathaniel Clyne aliongeza bao la pili kwa shuti kali na kufanya 2-1 dhidi ya wenyeji Arsenal.Southampton wameenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 2-1 dhidi ya Arsenal.

MATOKEO TIMU NYINGINE:
Arsenal 1 v 2 Southampton
Cardiff 0 v 3 Bournemouth
Derby 2 v 0 Reading
Leyton Orient 0 v 1 Sheffield United
Liverpool 2 v 1 Middlesbrough
MK Dons 2 v 0 Bradford
Shrewsbury 1 v 0 Norwich
Sunderland 1 v 2 Stoke
Swansea 3 v 0 Everton 

Fulham 2 v 1 Doncaster

Tuesday, September 23, 2014



Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini.


Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.

Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo



Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani...

Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.

wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.

Msanii wa Bongo Fleva Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.


Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.

Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MBEYA City fc imepata pigo baada ya wachezaji wake watatu kuumia katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu  iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana, uwanja wa Sokoine, Mbeya, na watakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili.
Afisa habari wa klabu hiyo, Dismas Ten ameiambia MPENJA BLOG mchana huo kuwa baada ya mechi iliyopita, wachezaji watano walipata majeruhi, lakini wawili kati yao watarejea uwanjani jumamosi ya septemba 27 kuchuana na Coastal Union.
“Kwanza nianze na majeruhi; baada ya mechi kumalizika jumamosi iliyopita, kuna wachezaji wetu watano walipata majeraha, lakini wawili kati yao watarejea jumamosi  ijayo kucheza dhidi ya Coastal Union kwasababu maumivu yao hayakuwa makubwa sana. Wachezaji hao ni beki Deogratius Julius ‘Musafwa wa Kweli’ na kiungo mahiri, Steven Mazanda.” Alisema Dismas.
“Wachezaji wengine watatu kwa maana ya John Kabanda, Alex Seth na Eric Mawala, hawataweza kucheza kabisa siku ya jumamosi kwasababu watakaa nje kwa majuma mawili, kwa mujibu wa daktari wetu.”
Dismas aliongeza kuwa maandalizi ya mechi ya pili nyumbani yanakwenda vizuri na wachezaji wana morali ya kutafuta ushindi na kuendeleza rekodi yao ya msimu uliopita ambapo walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na mabingwa Azam fc.
“Hali ya kambi ni nzuri, tunajiandaa vizuri na tunaamini tutaibuka na ushindi. Tulicheza mpira mkubwa sana dhidi ya JKT Ruvu, sema wakati mwingine demokrasia ya mpira wa miguu inabidi tukubaliane nayo”
“Kuna kushinda, kushindwa na kutoa sare, lakini mwisho wa siku tulicheza mpira mzuri na watu waliokuwepo uwanjani waliridhika na kiwango cha timu”

“Tunataka kulipa kisasi, Coastal walitufunga na kutuharibia rekodi yetu. Tunataka kuonesha kwamba kutufunga kwao sio kwamba tulikuwa chini ya kiwango bali walitubahatisha tu”


Na Baraka Mpenja, Dar esl salaam
IMEELEZWA kuwa mshambuliaji wa Simba sc, Mkenya Paul Kiongera Mungai leo amefanyiwa vipimo hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia kuumia goti katika sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union, jumapili iliyopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika vipimo vya awali, Kiongera amebainika kuwa na majeruhi sugu ya goti kama ilivyowahi kuelezwa na mtandao huu siku za nyuma.
Kiongera anayekonga nyoyo za mashabiki wa Simba alitokea benchi katika dakika ya 67 dhidi ya Wagosi wa Kaya, lakini dakika mbili kabla ya mechi kuisha alitonesha goti lake kwa kugongana na kipa Shaaban Hassan Kado, hivyo kulazimika kumpisha Amri Kiemba.
Baada ya kuumia, Kiongera alionekana kubadilika katika lugha yake ya mwili ‘Body Language’ akionesha kuwa ameumia sana na hataweza kurudi uwanjani kirahisi.
Kabla ya kusajiliwa majira ya kiangazi mwaka huu, ripoti zilifafanua kuwa Kiongera ana majeruhi ya muda mrefu aliyopata wakati anacheza Kenya, lakini kutokana na Simba kukosa mfumo wa kupima afya za wachezaji kabla ya kuwasajili walijikuta wakimsainisha mkataba akiwa na ‘pancha’.
Imefahamika kuwa Kiongera anaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki sita au miezi miwili na litakuwa pigo kwa Wanamsimbazi wanaovutiwa na uchezaji wa Mkenya huyo.
Kwa maana hiyo Oktoba 12 mwaka huu kuna uwezekano mkubwa nyota huyo akautazama mpambano wa watani wa jadi, Simba na Yanga akiwa jukwaani na kuwaacha mashabiki wa Simba wakisikitika.
Mbali na Kiongera, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ ni majeruhi pia, wakati Haruna Chanongo aliyeumia kwenye mechi dhidi ya Coastal Union anaweza kurudi uwanjani muda wowote.
Wakati huo huo, Kiungo wa ulinzi aliyekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu sasa, Jonas Mkude ameimarika kiasi cha kusubiri maamuzi ya kocha Patrick Phiri kumpanga katika mechi ijayo dhidi Polisi Morogoro, Septemba 27 mwaka huu uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Mkude hajawahi kucheza chini ya kocha Phiri wala kufanya mazoezi, kwahiyo Mzambia huyo ndiye mwenye maamuzi ya kumpanga au kumpa mazoezi maalumu ili kuimarika zaidi.
Mechi iliyopita, Piere Kwizera alicheza nafasi ya Mkude, lakini alionekana kutoimudu kwa asilimia kubwa na alikosa maamuzi sahihi hasa katika upigaji wa pasi.

Alikuwa anachelewa kuanzisha ‘Movement’ pale inapobidi na alikuwa anapiga pasi vizuri bila kukosea -kukosea, lakini nyingi hazikuwa na madhara kwa Coastal Union.


Aliyekuwa Rais wa TFF, Leodigar Chila Tenga alikuwa mchezaji muhimu wa Taifa Stars miaka ya 1980
HISTORIA inaonesha kuwa zamani mpira wa miguu ulikuwa unachezwa kutoka ngazi ya chini mpaka juu na walipatikana wachezaji wengi wa kulisaidia taifa.
Taifa Stars iliyoshiriki michuano ya mataifa ya Afrika nchini Nigeria miaka ya 1980, ni ushahidi tosha juu ya suala hilo.
Katika kipindi hicho kisichosahaulika miongoni mwa wadau wengi wa soka nchini, wachezaji waliounda Taifa  Stars walitoka timu mbalimbali za chini na za juu. Klabu kubwa za Simba na Yanga hazikutoa wachezaji wake kwa asilimia kubwa.
Leo hii klabu moja inakuwa na wachezaji 6, 8 mpaka 10 katika kikosi cha Taifa Stars. Zamani haikuwa hivi, Simba na Yanga miaka ya 80 wakati Stars ikiifunga Kenya, Harambee Stars 5-0 zilitoa wachezaji wanne tu (kila timu wawili).
Hii ilitokana na kuwepo wachezaji wengi sana. Makocha wa Stars walikuwa na wigo mpana wa kuteua wachezaji kutoka klabu mbalimbali hadi za daraja la pili. Mashindano yalikuwa mengi mno kuanzia chini na mpira ulipigwa kila kona ya nchi.
Leo hii mambo ni tofauti kabisa, mpira hauchezwi kwa misingi mizuri. Hakuna mashindano  mengi maalumu. Taifa Stars inategemea wachezaji kutoka Yanga, Simba na Azam fc.
Kutokana na mazingira hayo, wachezaji wamebaki walewale kila siku. Leo hii kocha wa Stars, Mart Nooij akimuacha Mrisho Ngassa, unadhani ni mchezaji gani mwenye kiwango cha juu atabadili nafasi yake?
Nani anaweza kurithi vizuri nafasi ya Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbwana Samatta au Thomas Ulimwengu? Makocha wamejikuta hawana machaguo kwasababu ndio wachezaji waliopo katika kiwango cha juu kwasasa.
Taifa Stars enzi hizo ilikuwa moto wa kuotea mbali

Kocha amekosa wigo mpana wa kuchagua wachezaji wa Stars, lakini zamani kocha alikuwa anaamua mwenyewe amchukue mchezaji wa aina gani na haikuwa lazima kuzifikiria Simba na Yanga .
Ukweli ni kwamba wachezaji wengi ambao waliibuka na kuwa  nyota wa Tanzania walitoka ligi za mchangani.
Ligi hizi zilikuwa na ushindani na hamasa kubwa, kwahiyo Dr Mwaka Sports Xtra Ndondo Cup inajaribu kurudisha hali hiyo na kutoa fursa kwa vipaji vingi vilivyopo mtaani na kuvipatia jukwaa la kuonekana.
Haya sio mawazo mpya, tayari yalishafanyika huko nyuma, lakini michuano hii inakuja kwa ‘staili’ nyingine ya kileo na itatangazwa.
Wachezaji bora wa mashindano watapatikana na kutafutiwa njia ya kuweza kuwaendeleza.
Pia lengo ni kuzitengenezea klabu kubwa sehemu ya kutafuta wachezaji wapya kuliko kusajili hovyo hovyo. Kwasasa hakuna wigo mpana wa kusajili wachezaji, hivyo michuano hii inataka kuibua vipaji vingi vilivyopo mitaani.
Kwa mfano Mtibwa Sugar kila mwaka inauza wachezaji, lakini bado inaendelea kuwepo na kutafuta vipaji vipya kutoka mchangani. Wachezaji wapo wengi, lakini hakuna mashindano.
Kutokana na mazingira haya, Sports Xtra ya Clouds fm imeamua kuanzisha mashindano yanayokwenda kwa jina la DR MWAKA SPORTS XTRA NDONDO CUP.
Banner Ads Top
Michuano hii itakayoendeshwa kwa mfumo wa kisasa kabisa itashirikisha wachezaji wa mchangani kutoka timu 32.
Kivumbi kinatarajia kuanza  Septemba 27 mwaka huu ambapo mechi ya ufunguzi itawakutanisha  Friend’s Rangers na Kiluvya United katika uwanja wa Makulumla, Magomeni, Dar es salaam, majira ya saa 10:00 jioni.
Mbali na dimba la Makulumla, viwanja vingine vitakavyotumika katika mashindano hayo ni Kinesi (Shekilango), Benjamini Mkapa (Ilala) na Mizinga (Kigamboni).
Timu 32 zitakazoshiriki zimepangwa katika makundi nane yenye timu nne.
Kundi A: Boom fc, Beira Hotspurs, Tabata fc na Tuamoyo
Kund B: Sifa Politani, Vijana Ilala, Kijichi, Micco Villa
Kundi C: Friend’s Rangers, Temeke Market, Kiluvya United na Muheza fc
Kundi D: Ukonga United, Sinza Stars, Congo Shooting na Snow White
Kundi E: Zakhem, Black Six, TP Same na Makumba
Kundi F: Villa Squad, Scud fc, Nyota Afrika na Burudani fc
Kundi H: Stakishari fc, Abajalo, Shelaton na Kimara United

waliotembelea blog