Saturday, August 15, 2015



Sakata la hatma ya golikipa wa kimataifa wa Hispania David De Gea ndani ya klabu ya Manchester United linazidi kuchukua sura mpya.
 
De Gea ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na Real Madrid, alianza kwa kupigwa benchi kwa mechi mbili za ufunguzi na kocha Louis Van Gaal na taarifa mbalimbali kutoka kwenye vyombo vya habari vya Uingereza zinasema mchezaji huyo aliamuariwa na Van Gaal kufanya mazoezi na timu ya ‘reserves’ na pia alikatazwa kusafiri na United iliyoenda Birmingham kucheza na Aston Villa.
 
David de Gea alifanya mazoezi na timu ya wachezaji wa akiba na kuambiwa kwamba hatokuwa kwenye msafara wa timu ulioenda kupambana na Villa usiku wa leo.
  Sergio Romero aliendelea kukaa langoni mwa United usiku wa leo katika mechi ya ushindi vs Aston Villa.
Siku ya Alhamisi, kocha wa United Van Gaal alikaririwa akisema kwamba De Gea alimwambia kocha wa makipa wa United Frans Hoel Kwamba hataki kucheza mpaka hatma yake itakapojulikana ndani ya klabu hiyo.

Ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga imeanza rasmi leo kwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo FC Bayern Munich kuwakaribisha Hamburg katika dimba la Alianz Arena.

Wakicheza mchezo wa kuvutia na wa kasi FC Bayern wameibuka na ushindi wa magoli 5-0.
 
Beki wa Kimorocco Mehd Benatia alianza kuifungia Bayern goli katika dakika ya 27 ya mchezo kabla ya Robert Lewandoski kuongeza la pili katika dakika ya 53.
 Mshambuliaji wa kijerumani Thomas Muller alifunga mara mbili ndani ya dakika 4 za mchezo huo katika kipindi cha pili dakika ya 69 na 72.
 Kiungo mpya wa timu hiyo Douglas Costa alifunga ukurasa wa magoli matano ya Bayern kwa kufunga goli la kwisho katika dakika ya 87.
  Bayern wanakaa kileleni mwa Bundesliga wakiwa na pointi 3 na magoli ya kufunga 5 huku wakiwa hawajaruhusi wavu wao kuguswa.


Mbele ya Mashabiki 75,000
Bayern Munich wameanza msimu mpya wa Bundesliga 2015/16 vyema baada ya kuwachapa Hamburg SV bao 5-0, Bao za Bayern zilifungwa na Medhi Benatia dakika ya 27 ya kipindi na chanza na kipindi cha pili ndipo walizidi kuishindilia timu hiyo bao nne la pili likifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 53, Thomas Müller alifunga bao mbili dakika ya 69 pamoja na lile la dakika ya Thomas Müller 73 na kufanya 4-0. Bao la tano lilifungwa na Douglas Costa dakika 87 na kufanya 5-0 na mtanange kumalizika kwa dakika 90 Bayern wakiibuka na ushindi mnono wa kufungulia msimu mpya wa Bundesliga 2015/2016.


Januzaji akishangilia bao lake1-0 Man United Mbele!!1-0Furaha kwa Bao la Januzaj dakika ya 29Mpaka ndani ya nyavu!!

Shangwe!Januzaj akipongezwa na baadhi ya wachezaji wenzake wa United baada ya kuipa bao la kuongoza kipindi cha kwanza. Bao hilo pia liliweza kudumu hadi kipindi cha dakika 90 na kufanya United kuibuka kidedea kwa bao hilo la Januzaj kwa ushindi wa bao 1-0 na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu England kwa kufikisha pointi 6.Januzaji dakika ya 29 kipindi cha kwanza anaipa bao la kwanza Man United kwa kufanya 1-0 dhidi ya wenyeji wao Aston Villa. Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha kwanza cha dakika 45 za kipindi cha kwanza United wakiwa mbele ya bao 1-0.Michael Carrick nafasi yake ilichukuliwa na Bastian Jordan Amavi akichuana chini dhidi ya Ander HerreraMeneja  wa Man United Van GaalDepay akipagawa baada ya kukosa bao la wazi kipindi cha piliMkongwe Michael Carrick akiendesha mpira Depay akichuana vikali usiku huu


BAO za Athletic Bilbao zimefungwa na Mikel San Jose mapema kipindi cha kwanza dakika ya 13 na kipindi cha pili dakika ya 53
Aritz Aduriz akaongeza bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya mabingwa Barcelona.

 Aritz Aduriz alifunga tena bao dakika ya 62 na akaongeza bao la tatu(Hat-trick) kwa kufunga penati dakika ya 68 na kufanya 4-0 dhidi ya Barcelona.
Ukuta wa Barca haukuwa imara usiku huu!Lionel Messi hoi!Vijana walipoweka 3-0



































waliotembelea blog