Thursday, September 18, 2014


http://i3.mirror.co.uk/incoming/article3064065.ece/alternates/s1227b/Wayne-Rooney.jpgWayne RooneySTAA wa Manchester United Wayne Rooney amemmwagia sifa Meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson kwa kumwita ni ‘Mtu wa hodari’.
Rooney, amabe aliripotiwa kugombana na Sir Alex Ferguson Mwaka mmoja uliopita hasa baada ya kutua kwa Robin van Persie Klabuni hapo, sasa ametimiza Miaka 10 akiwa na Man United na amesheherekea kwa kumpongeza Ferguson kwa kumpa nafasi kucheza Old Trafford ikiwa ni dalili ya wazi ulio uhusiano wao ‘uliopoa’ sasa umerudi tena.

Rooney aliiambia MUTV, Kituo cha TV cha Man United: “Yeye ni Mtu muhimu sana. Ninamshukuru kwa kuniamini na kunichukua kutoka Everton. Sir Alex ndie Meneja bora kupita yeyote na kwa yeye kutambua kipaji changu na kutaka kujiunga nae ni heshima kubwa!”
Aliongeza: “Hakika alinisaidia sana mimi na wote. Alitukusanya Vijana na kutuingiza kwenye Kikosi na kutufanya tuwe Klabu Bingwa Duniani. Nashukuru kwa kila kitu alichotufanyia.”
Rooney, ambae alisaini Mkataba wa Miaka Mitano na Nusu Mwezi Februari, amesema yeye atamaliza Mkataba huo akiwa hapo hapo Man United.

Amesema: “Nategemea hilo. Nimesaini Mkataba wa muda mrefu na nategemea baada ya Miaka Mitano


LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Septemba 20
14:45 QPR v Stoke
17:00 Aston Villa v Arsenal
17:00 Burnley v Sunderland
17:00 Newcastle v Hull
17:00 Swansea v Southampton
19:30 West Ham v Liverpool
Jumapili Septemba 21
15:30 Leicester v Man United
15:30 Tottenham v West Brom
18:00 Everton v Crystal Palace
18:00 Man City v Chelsea
Jumamosi Septemba 27
14:45 Liverpool v Everton
17:00 Chelsea v Aston Villa
17:00 Crystal Palace v Leicester
17:00 Hull v Man City
17:00 Man United v West Ham
17:00 Southampton v QPR
17:00 Sunderland v Swansea
19:30 Arsenal v Tottenham
Jumapili Septemba 28
18:00 West Brom v Burnley
Jumatatu Septemba 29
22:00 Stoke v Newcastle


Warembo 30 wanaoshiriki shindano la Redd's Miss Tanzania 2014 jana walitembelea hifadhi ya taifa ya Mikumi mkoani Morogoro kujionea vivutio mbalimbali vya utalii viliovyopo katika hifadhi hiyo ambapo waliweza kujionea wanyama wa aina mbalimbali wakiwepo, Tembo, Twiga, Swala, Viboko na Simba.
Klaas Jan Huntelaar akifanya yake kusawazisha baoWachezaji wa Chelsea wakiwa hoi baada ya Schalke 04 kusawazisha bao kupitia kwa Klaas Jan Huntelaar katika kipindi cha pili dakika ya 62. Cesc Fàbregas akiachia shuti kali na kufunga1-0Dakika ya 11 Cesc Fàbregas anaipachikia bao la kwanza Chelsea dhidi ya Schalke 04. Bao hilo lilipatikana baada ya ushirikiano safi kutoka kwa Eden Hazard.Cesc Fàbregas akishangilia baoDrogba akiruka juu kwenye eneo hatari la box Eden Hazard akiendesha...Mzoefu ...Drogba nae jana alikuwemo.



AS ROMA wakiwa kwao kucheza na CSKA Moscow kwenye hatua ya makundi Uefa Champions Ligi ndio walianza kuonesha nia na kiu kwa kuanza kupachika mabao, Wakiifunga bao 4-0 kipindi cha kwanza timu ya CSKA Moscow.Bao la kwanza lilifungwa na Juan Manuel Iturbe dakika ya 6, Bao la pili lilifungwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal Gervinho katika dakika ya 10, Maicon akapachika bao la tatu dakika ya 20 na kisha Gervinho kuongeza bao tena dakika ya 31 na mtanange kumalizika kipindi cha kwanza CSKA Moscow wakiwa nyuma ya bao 4-0.

Kipindi cha pili dakika ya 51 baada ya patashika kutokea mchezaji wa CSKA Moscow Sergey Ignashevich alijifunga bao na kufanya bao kuwa 5-0.
Bao la CSKA Moscow lilifungwa na Ahmed Musa katika dakika ya 82 kipindi chaa pili na mtanange kumalizika AS Roma wakiwa na ushindi wa bao 5-1.


Gerard Piqué akishangilia bao lake kipindi cha kwanza dakika ya 28. bao lililodumu mpaka dakika 90 kumalizika na Barcelona kujichukulia alama 3 muhimu wakiwa nyumbani kwao kwenye mchezo wa Uefa Champions League hatua ya makundi.Lionel Messi akifukuziwa na Bonge la msitu...Dakika ya 28 Gerard Piqué aliifungia bao la kichwa Barcelona na kuitanguliza 1-0 dhidi ya timu ya APOEL Nicosia.




Kikosi cha timu ya Kipanga kilichotoa upinzani na Timu ya Miembeni kuilazimisha kutoka sare ya bao 1--1, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar. Ikiwa imepanda daraja msimu huo baada ya kudima kwa muda katika daraja la kwanza na hatimai kufanikiwa kurudi ligi kuu na kutowa upinzani kwa timu ya miembeni katika uwanja wa amaan.

Kikosi cha timu ya Miembeni kilicholazimisha sare na timu ya Kipanga katika dakika za lalasama kupitia mshambuliaji wake Othm,an Omar, kuweza kuisawazishia timu yake katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Mshambuliaji wa timu ya Kipanga Matteo Antoni mwenye mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Miembeni Othman Omar katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Grand Malt inayofanyika katika uwanja wa Amaan.

Beki wa Timu ya Miembeni Mohammed Du Bakari akiokoa moja ya hatari golini kwake na huku wachezaji wa timu ya Kipanga wakijaribu kumzuiya kushoto Hassan Saleh na Amour Suleiman.

Shabiki wa timu ya Kipanga akipeperusha bendera ya timu yake kwa wapenzi wa timu ya Miembeni wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Grand Malt iliofanyika uwanja wa Amaan

waliotembelea blog