Thursday, September 18, 2014



AS ROMA wakiwa kwao kucheza na CSKA Moscow kwenye hatua ya makundi Uefa Champions Ligi ndio walianza kuonesha nia na kiu kwa kuanza kupachika mabao, Wakiifunga bao 4-0 kipindi cha kwanza timu ya CSKA Moscow.Bao la kwanza lilifungwa na Juan Manuel Iturbe dakika ya 6, Bao la pili lilifungwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal Gervinho katika dakika ya 10, Maicon akapachika bao la tatu dakika ya 20 na kisha Gervinho kuongeza bao tena dakika ya 31 na mtanange kumalizika kipindi cha kwanza CSKA Moscow wakiwa nyuma ya bao 4-0.

Kipindi cha pili dakika ya 51 baada ya patashika kutokea mchezaji wa CSKA Moscow Sergey Ignashevich alijifunga bao na kufanya bao kuwa 5-0.
Bao la CSKA Moscow lilifungwa na Ahmed Musa katika dakika ya 82 kipindi chaa pili na mtanange kumalizika AS Roma wakiwa na ushindi wa bao 5-1.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog