Kikosi cha timu ya Kipanga kilichotoa upinzani na Timu ya Miembeni kuilazimisha kutoka sare ya bao 1--1, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar. Ikiwa imepanda daraja msimu huo baada ya kudima kwa muda katika daraja la kwanza na hatimai kufanikiwa kurudi ligi kuu na kutowa upinzani kwa timu ya miembeni katika uwanja wa amaan.
Kikosi cha timu ya Miembeni kilicholazimisha sare na timu ya Kipanga katika dakika za lalasama kupitia mshambuliaji wake Othm,an Omar, kuweza kuisawazishia timu yake katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
Mshambuliaji wa timu ya Kipanga Matteo Antoni mwenye mpira akijiandaa kumpita beki wa timu ya Miembeni Othman Omar katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Grand Malt inayofanyika katika uwanja wa Amaan.
Beki wa Timu ya Miembeni Mohammed Du Bakari akiokoa moja ya hatari golini kwake na huku wachezaji wa timu ya Kipanga wakijaribu kumzuiya kushoto Hassan Saleh na Amour Suleiman.
Shabiki wa timu ya Kipanga akipeperusha bendera ya timu yake kwa wapenzi wa timu ya Miembeni wakati wa mchezo huo wa Ligi Kuu ya Grand Malt iliofanyika uwanja wa Amaan
0 maoni:
Post a Comment