Saturday, October 24, 2015



 Leo ni Leo Mwanza... maana wakazi wa jiji La Mwanza na vitongoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumpokea mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli. Huku Maelfu ya watu wamejitokeza kwenda CCM Kirumba jijini Mwanza kuhudhuria mkutano wa kufunga kampeni leo Oktoba 24, 2015.
 Kila mmoja akijikaza kujongea CCM Kirumba, Mwanza.

 Akina mama nao wamo.....
 Vijana wamehamasika kweli kweli....
 Leo hapakaliki...
 Mwenyekiti wa CCM,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akisalimiana na Mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Pombe Magufuli,mara baada ya kuwasili katika uwanja wa CCM Kirumba kuhitimisha shughuli za kampeni nchini kote,ambapo hapo kesho wananchi wanatarajia kupiga kura ya kuwachagua viongozi wawatakao.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli wakielekea jukwaani kwa pamoja mara baada ya kupokelewa katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo umati mkubwa watu umejitokeza kushuhudia tukio hilo adhimu.
 Mara baada ya kuwasalimia Wananchi kwa pamoja wakirejea meza kuu.

 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitoa chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba huku akilakiwa na melfu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika hivi sasa kwenye hitimisho la mikutano ya kampeni.
 Wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia wakati Mgombea Urais wa CCM alipokuwa akiwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba hivi punde kuhitimisha mikutano ya kampeni,ambapo kesho Wananchi nchini watapiga kura kuwachagua viongozi wawatako kuwatumikia katika awamu ya tano.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasili ndani ya uwanja wa CCM Kirumba huku akilakiwa na melfu ya wakazi wa jiji la Mwanza waliofurika hivi sasa kwenye hitimisho la mikutano ya kampeni.

Jose Mourinho amemponda Marc Wilmots kuhusu madai yake kwamba Eden Hazard ataondoka Chelsea na kuhamia Real Madrid
Msimu uliopita Hazard, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Belgium, alitunukiwa Tuzo ya PFA pamoja na ile ya Wanahabari ya kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka huko England lakini Msimu huu uchezaji wake umeporomoka.
Wiki iliyopita Mourinho alimpiga Benchi Hazard wakati Chelsea inaifunga Aston Villa 2-0 kwenye Ligi kwa madai kuwa anataka kuzuia Timu yake isiruhusu Mabao.
Magazeti kadhaa huko England yalimnukuu Marc Wilmots, ambae ni Kocha wa Timu ya Taifa ya Belgium, akisema Hazard, mwenye Miaka 24, anapaswa kuhamia Real Madrid ilia pate uhuru zaidi wa kucheza na pia kukwepa sulubu nzito ya Soka la England.
Maneno hayo yamemkasirisha Mourinho ambae amesema: "Kocha wa Timu ya Taifa ni wa Taifa. Hazard akiwa Timu ya Taifa mimi sisemi lolote. Lakini Watu wengine hawana maadili na wanazungumzia Wachezaji wakiwa Klabuni kwao!”

Alipoulizwa kama Hazard atacheza hii Leo dhidi ya West Ham, Mourinho alijibu: “Sijui. Kuna Watu wengi wanatoa maoni yao kuhusu uchezaji wa Hazard Msimu huu. Mimi sipendi kuzungumzia Mtu binafsi.”


NAHODHA wa England na Manchester United Wayne Rooney Leo ametimiza Miaka 30 ya kuzaliwa kwake.
Rooney alitinga na kujitambulisha katika Dunia ya Soka Miaka 13 iliyopita alipocheza Mechi wakati Timu yake Everton inaifunga Arsenal Bao 2-1 Mwaka 2002 na yeye kufunga Bao safi mno na kumaliza mbio za Arsenal za kutofungwa katika Mechi 30.
Miaka Miwili baadae Rooney alihamia Manchester United na pia kujikita kama Mchezaji wa kuaminika wa Timu ya Taifa ya England.
Kwa sasa Rooney ndie anaeshikilia Rekodi ya Ufungaji Bao nyingi katika Historia ya England huku pia akiikimbiza Rekodi ya Ufungaji ya Man United.
Licha ya kulaumiwa kuwa hana mafanikio makubwa katika anga za Kimataifa lakini Rekodi yake ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 5 na UEFA CHAMPIONS Ligi pamoja na Medali nyingine nyingi ni kielelezo tosha cha mafanikio yake katika Soka.


WAYNE ROONEY NA MAISHA YAKE YA SOKA

303 – Jumla ya Mabao aliyofunga katika Mechi 673 alizochezea Klabu na England.
50 - Rooney alikuwa Mchezaji wa kwanza kufikisha Bao 50 kwa England alipofunga Penati dhidi ya Switzerland Septemba 2015.
107 – Mara Rooney alizochezea England akifungana na Ashley Cole kuwa Nambari 5 kwa Mechi nyingi za kuichezea England.
236 – Mabao aliyofunga Rooney katika 489 za Manchester United. Anahitaji bao 14 zaidi kuiipita Rekodi ya Mabao mengi ya Sir Bobby Charlton.
187 – Mabao ambayo Rooney amefunga kwenye Ligi Kuu England na kumfanya ashike Nambari Mbili pamoja na Andy Cole wakiwa nyuma ya Mfungaji Bora Alan Shearer mwenye Mabao 260.
3 - Rooney alipiga Bao 3 katika Mechi yake ya kwanza tu kuichezea Man United walipoitandika Fenerbahce 6-2 katika UEFA CHAMPIONS LIGI.



LA LIGA
RATIBA
Jumamosi Oktoba 24

17:00 Celta de Vigo v Real Madrid CF
19:15 Granada CF v Real Betis
21:30 Sevilla FC v Getafe CF
23:05 Malaga CF v Deportivo La Coruna

Jumapili Oktoba 25
14:00 Levante v Real Sociedad
18:00 Las Palmas v Villarreal CF
20:15 FC Barcelona v SD Eibar
22:30 Atletico de Madrid v Valencia C.F

Jumatatu Oktoba 26
22:30 Athletic de Bilbao v Sporting Gijon

waliotembelea blog