Saturday, October 24, 2015


NAHODHA wa England na Manchester United Wayne Rooney Leo ametimiza Miaka 30 ya kuzaliwa kwake.
Rooney alitinga na kujitambulisha katika Dunia ya Soka Miaka 13 iliyopita alipocheza Mechi wakati Timu yake Everton inaifunga Arsenal Bao 2-1 Mwaka 2002 na yeye kufunga Bao safi mno na kumaliza mbio za Arsenal za kutofungwa katika Mechi 30.
Miaka Miwili baadae Rooney alihamia Manchester United na pia kujikita kama Mchezaji wa kuaminika wa Timu ya Taifa ya England.
Kwa sasa Rooney ndie anaeshikilia Rekodi ya Ufungaji Bao nyingi katika Historia ya England huku pia akiikimbiza Rekodi ya Ufungaji ya Man United.
Licha ya kulaumiwa kuwa hana mafanikio makubwa katika anga za Kimataifa lakini Rekodi yake ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 5 na UEFA CHAMPIONS Ligi pamoja na Medali nyingine nyingi ni kielelezo tosha cha mafanikio yake katika Soka.


WAYNE ROONEY NA MAISHA YAKE YA SOKA

303 – Jumla ya Mabao aliyofunga katika Mechi 673 alizochezea Klabu na England.
50 - Rooney alikuwa Mchezaji wa kwanza kufikisha Bao 50 kwa England alipofunga Penati dhidi ya Switzerland Septemba 2015.
107 – Mara Rooney alizochezea England akifungana na Ashley Cole kuwa Nambari 5 kwa Mechi nyingi za kuichezea England.
236 – Mabao aliyofunga Rooney katika 489 za Manchester United. Anahitaji bao 14 zaidi kuiipita Rekodi ya Mabao mengi ya Sir Bobby Charlton.
187 – Mabao ambayo Rooney amefunga kwenye Ligi Kuu England na kumfanya ashike Nambari Mbili pamoja na Andy Cole wakiwa nyuma ya Mfungaji Bora Alan Shearer mwenye Mabao 260.
3 - Rooney alipiga Bao 3 katika Mechi yake ya kwanza tu kuichezea Man United walipoitandika Fenerbahce 6-2 katika UEFA CHAMPIONS LIGI.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog