Monday, November 2, 2015


MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho atabakia kwenye kibarua chake kwa sasa licha ya Jana kutandikwa 3-1 Uwanjani kwao Stamford Bridge na Liverpool kwenye Mechi ya Ligi Kuu England ikiwa ni ni kipigo chao cha 6 katika Mechi 11 za Ligi hiyo Msimu huu.
Chelsea, ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, wapo Nafasi ya 15 kwenye Msimamo wa Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Man City.
Akihojiwa mara baada ya kipigo cha Jana kama anadhani hiyo ndio Mechi yake ya mwisho kama Meneja, Mourinho alijibu: “Hapana. Sifikirii hilo!”

Mourinho, ambae hajawahi kufungwa zaidi ya Mechi 6 za Ligi katika Msimu mmoja akiwa kama Meneja wa Chelsea, aliongeza: “Mapambano yanaendelea lakini wakati mwingine mapambano haya ni magumu kushinda. Unaingia kwenye mapigano na silaha nyingine!”
Jose Mourinho na wasaidizi wake na viongozi wengin wakiteta jambo
Mourinho wakijiuliza jambo

Maswali yaliyobaki bila Majibu!!!

#3-1 walinyukwa na Liverpool wakiwa nyumbani Stamford Bridge


Jose Mourinho

waliotembelea blog