Stori kuhusu bondia wa kitanzania Francis Cheka kusafiri kwenda Manchester Uingereza kupambana na bondia wa kiingereza zimezidi kuchukua headlines kutokana na safari yake kutoeleweka. Cheka aliripotiwa kusafiri kwenda Uingereza kwa zaidi ya wiki kadhaa nyuma lakini safari yake imekuwa ikihairishwa mara kwa mara.
Siku kadhaa nyuma meneja wa bondia huyo Juma Ndambile alifanya mahojiano na gazeti la The Citizen na kuthibitisha bondia huyo, kuwa yupo katika mpango wa kwenda Uingereza kupambana katika pambano lisilo la Ubingwa na bondia wa kiingereza licha ya kuwa hakuwa amewekwa wazi ila Juma alikiri kuwa bondia wake yupo tayari kupambana na bondia yoyote.
November 4 pambano hilo limeingia katika headlines kwa mara nyingine baada ya Francis Cheka kushindwa kusafiri kutokana na sababu ambazo hata Cheka hajui kwa nini pambano hilo limekuwa likihairishwa kwa zaidi ya mara tatu na bado hapokea tiketi ya safari hiyo.
“Sifahamu
ni kitu gani kinaendelea, hii mechi imekuwa ikihairishwa kama mara nne
sasa siwezi kujua nini hao waingereza wanakusudia lakini sijui labda
wanahofia kwa sababu mabondia wao wengi nimewahi kupigana nao na
kuwapiga, Labda kuna mtu yupo Tanzania anatoa taarifa kuwa Cheka yuko
vizuri hivyo mechi muhairishe” >>> Cheka