Saturday, January 3, 2015


MABINGWA wa FA CUP, Arsenal, wanaanza utetezi wa Taji lao Wikiendi hii kwa kucheza Nyumbani Emirates na Hull City hilo likiwa pambano moja kati ya Matatu yanayohusisha Timu za Ligi Kuu England pekee kwenye Raundi ya Tatu.
Mengine ya Timu za Ligi Kuu England pekee ni yale ya Tottenham kucheza Ugenini na Burnley na Leicester kukipiga na Newcastle.
Msimu uliopita Arsenal walibeba FA CUP kwa kuitoa Hull City kwenye Fainali.
Vinara wa Ligi Kuu England, Chelsea, wao wako Nyumbani Stamford Bridge kucheza na Watford, Timu ya Daraja la chini, Championship, wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Man City, pia wako kwao Etihad kucheza na Sheffield Wednesday ambayo pia ipo Daraja la chini.
Vigogo Man United wao watakuwa Wageni wa Yeovil Klabu ya Ligi 1 ambalo ni Madaraja mawili chini ya Ligi Kuu England.

Mara ya mwisho kwa Yeovil kukutana na Manchester United ni Mwaka 1949 walipobamizwa Bao 8-0.

FA CUP
RATIBA
Ijumaa Januari 2

22:45 Cardiff v Colchester

Jumamosi Januari 3
Zote Saa 12 Jioni

Barnsley v Middlesbrough
Blyth Spartans v Birmingham City
Bolton v Wigan
Brentford v Brighton
Cambridge v Luton
Charlton v Blackburn
Derby v Southport
Doncaster v Bristol City
Huddersfield v Reading
Fulham v Wolves
Huddersfield v Reading
Leicester v Newcastle
Millwall v Bradford
Preston v Norwich
Rochdale v Nottm Forest
Rotherham v Bournemouth
Tranmere v Swansea
West Brom v Gateshead

Jumamosi Januari 4
Zote Saa 10 Jioni

Dover v Crystal Palace
QPR v Sheff Utd
Sunderland v Leeds

Saa 12 Jioni
Aston Villa v Blackpool
Man City v Sheffield Wednesday
Southampton v Ipswich
Stoke v Wrexham
18:30 Yeovil v Man United
19:00 Chelsea v Watford
20:30 Arsenal v Hull

waliotembelea blog