Mwanasoka raia wa
Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea
ndani ya bara la Afrika.
Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika
imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika
klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani.Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.
Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.
Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon
Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Ivory Coast, tuzo ambayo ameishinda kwa mwaka wa pili mfululizo.
Klabu bora ya soka barani Afrika ni TP Mazembe, kutoka DR Congo
Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon
Mwamuzi bora wa mwaka ni Bakary Gassama kutoka nchini Gambia
Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.