Thursday, July 23, 2015



Straika mpya wa Liverpool amefanya mazoezi yake ya kwanza leo na Wenzake Liverpool tangu ajiunge na Klabu hiyo kwenye Uwanja wa Mazoezi wa Melwood.

Benteke akiteta na  Mario Balotelli kwa furaha wakati wa Mazoezi

Benteke akiwa karibu na mgeni mwenzake  Roberto Firmino

Benteke akipiga kichwa mpira

Benteke akipeana mpira na Philippe Coutinho, aliyecheza  Copa America msimu huu

Benteke na mpira
Kutua kwa Benteke ni habari nyingine  Balotelli na Fabio Borini wana kazi ya ziada

Balotelli, Emre Can, Coutinho, na  Benteke wakati wanapasha kujiandaa na msimu mpya wa 2015/2016

Picha ya Pamoja
Mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli ameambiwa kuwa hatima yake ipo mikononi mwake.
Mchezaji huyo mtukutu raia wa Italia kwa sasa hajasafiri na wenzake wa Liverpool katika ziara kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi baadae mwezi Agosti.
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amenukuliwa akisema hana uhakika iwapo ataendelea kuwa na Balotelli Liverpool moja kwa moja katika msimu huu.

Liverpool imefanya ziara ya kujiandaa na ligi katika nchi za Asia , Australia na Malyasia lakini Balotelli yeye hakuwepo.



Beki wa timu ya LLBA ya Burundi, Hakizimana Issa akijaribu kumzuia mchezaji wa timu ya APR ya Rwanda, Mubumbyi Barnabe katika mchezo wa Kome la Kagame uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijioni Dar es Salaam. APR imeshinda 2-1. (Picha na Francis Dande)

Beki wa LLBA FC ya Burundi, Manirakiza Aruna akioko hatari langoni mwake.

Heka heka katika lango la timuya LLBA FC.

Simbomana Patrick wa APR ya Rwanda (kulia) akichuana na mchezaji wa LLBA FC ya Burundi, Ndaye Chancel.

Uwimana Messo akimiliki mpira uku akizongwa na mchezaji wa APR, Simbomana Patrick.

Beki wa LLBA, Manirakiza Aruna (katikati) kiwania mpira.

Bigirima Issa wa ARP (kushoto) akichuana na Uwimana Messo.

Kocha wa APR ya Rwanda, Dusan Dule akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Manirakiza Aruna akichuana na mchezaji wa LLBA FC ya Burundi.


Danny Ings akiwachomoka wachezaji wawili wa Felda United


Mabingwa wa England Chelsea wanebamizwa Bao 4-2 na New York Red Bulls wakati Kijana wa Miaka 16 akiwatoboa moja ya Bao hizo huko Red Bull Arena, New York katika Mechi yao ya kwanza Ziarani USA.
Bao za Chelsea zilifungwa na Loic Remy na Eden Hazard lakini ni New York Red Bulls waliokwenda mbele 3-1 huku Tyler Adams, Kijana wa Miaka 16, akipiga moja ya Bao hizo.
Bao Nyingine za Red Bull zilifungwa na Franklin Casterllanos na Davis Bao 2.
Mechi ifuatayo kwa Chelsea ni hapo Jumamosi dhidi ya PSG.
Adams akichuana na OscarVictor Moses Wachezaji wa Chelsea wakipongezana bao laoDiego Costa akituliaza mpiraCosta chupuchupu apate bao hapaEden Hazard akiruka juu kumpita aduiRamires akiparanganyika kwenye patashika kuutafuta mpira
YANGA SC wamezinduka katika michuano ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame, baada ya jioni ya leo kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Telecom ya Djibouti, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC iliyoanza vibaya mechi za Kundi A kwa kufungwa 2-1 na Gor Mahia ya Kenya, sasa inaweza kwenda Robo Fainali iwapo itashinda mechi zijazo dhidi ya KMKM na Khartoum N ya Sudan.
Katika mchezo huo, uliochezeshwa na refa Issa Kagabo wa Rwanda aliyesaidiwa na Lee Okello wa Uganda na Yeatyew Belachew wa Ethiopia, hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Malimi Busungu akipongezwa na Msuva na Tambwe baada ya kufunga bao la kwanza

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji mpya kutoka Mgambo JKT ya Tanga, Malimi Busungu dakika ya 26 baada ya kufumua shuti la kitaalamu akiwa katikati ya msitu wa mabeki wa Telecom, kufuatia krosi ya beki wa kulia, Mghana Joseph Tetteh Zuttah.
Yanga SC wangemaliza kipindi cha kwanza wanaongoza kwa mabao zaidi, kama wasingepoteza nafasi tatu za wazi za kufunga na kukosa pia penalti mbili.
Dakika ya 10 Busungu alipewa pasi nzuri na beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali aliyepanda kusaidia mashambulizi, lakini shuti lake likaokolewa na kipa Mrundi, Jeff Nzokira. 
Dakika ya 16, mshambuliaji Amisi Tambwe alipiga juu ya lango akiwa amebaki yeye na Mrundi mwenzake, kipa Nzokira ndani ya 18 baada ya kupasiwa na Busungu. 
Tambwe akapiga nje mkwaju wa penalti dakika ya 39 baada ya winga Simon Msuva kuchezewa rafu kwenye boksi na Warsama Ibrahim Aden.
Warsama Ibrahim Aden akasababisha penalti nyingine, baada ya kuunawa mpira ulioinuliwa na Msuva dakika ya 43, lakini shuti dhaifu la mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania likapanguliwa na kipa Nzokira.
Malimi Busungu akimtoka beki wa Telecom
Beki Hussein Botoyi wa Telecom akimpitia Mrundi mwenzake, Amissi Tambwe wa Yanga


Beki wa Yanga SC, Mwinyi Hajji Mngwali akitafuta njia ya kuwapita wachezaji wa Telecom
Simon Msuva alisababisha penalti mbili, moja akakosa mwenyewe, nyingine akakosa Tambwe


Kipindi cha pili, kocha wa Yanga SC aliwatoa wote wakosa penalti, Msuva na Tambwe na kuwaingiza Godfrey Mwashiuya na Mliberia Kpah Sherman.
Yanga SC ikafanikiwa kupata bao la pili dakika ya 66, mfungaji Yule Yule, Busungu akimalizia krosi nzuri ya Mwashiuya. 
Mwashiuya akafungua akaunti yake mabao Jangwani baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 77 baada ya kufumua shuti kali kutoka umbali wa mita 19 ‘lililomsumbua’ kipa Nzokira kabla ya kudondokea nyavuni.
Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Joseph Zutah, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Salum Tela, Simon Msuva/Godfrey Mwashiuya dk46, Haruna Niyonzima, Amisi Tamwe/Kpah Sherman dk46, Malimi Busungu na Deus Kaseke/Andrey Coutinho dk87.
Telecom FC; Jeff Nzokira, Said Hassan Elmi/ Warsama Hussein Said dk52, Daoud  Wais Ali, Mohamed Kader Daher, Warsama Ibrahim Aden, Moussa Ahmed Hassan, Mohamed Meraneh, Abubakar Dharar Djama, Mohamed Moustafa/ Anwar Sadad Ibrahim dk82, Eninga Freddy na Hussein Butoyi.


YANGA SC itahitaji kuifunga KMKM ya Zanzibar kesho, tena ushindi mzuri ili kujihakikishia nafasi ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, michuano inayoendelea Dar es Salaam.
Na KMKM itahitaji ushindi ili pia kujihakikishia kwenda Robo Fainali ya michuano hiyo kutoka Kundi A.
Timu tatu kati ya tano za kundi hilo zitakwenda Robo Fainali kuungana na washindi wawili wa kila kundi B na C pamoja na mshindi wa tatu bora kutoka makundi hayo.
KMKM na Yanga SC kila moja ina pointi tatu baada ya kila timu kushinda mechi moja hadi sasa, dhidi ya wapinzani wale wale, Telecom ya Djibouti.
Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm akimpa maelekezo mchezaji wake, Simon Msuva wakati ananyooshwa misulu na Jacob Onyango

KMKM imekwishapoteza mechi mbili baada ya kufungwa 2-1 na Khartoum N na 3-1 na Gor Mahia, wakati Yanga SC imepoteza mechi moja tu dhidi ya Gor.
Kama KMKM itafungwa na Yanga SC kesho, ina maana wakitoka Uwanja wa Taifa, watakwenda moja kwa moja kwenye boti za Azam Marine kurejea Zanzibar.
Kocha Ally Bushiri wa KMKM alisema jana bada ya kipigo cha Khartoum kwamba watarudi Uwanja wa Taifa, Ijumaa kupigania ushindi ili kuangalia uwezekano wa kwenda Robo Fainali.
Yanga SC ina mechi nyingine ngumu dhidi ya vinara wa kundi hilo, Khartoum N ya Sudan ambayo itakuwa ya mwisho baada ya kucheza na KMKM kesho.
Khartoum ina pointi sita, mabao saba ya kufunga na moja la kufungwa, wakati Gor Mahia walio nafasi ya pili wana ponti sita, mabao matano ya kufunga na mawili ya kufungwa.
Yanga SC inashika nafasi ya tatu kwa pointi zake tatu, mabao manne ya kufunga na mawili ya kufungwa, wakati KMKM ina pointi tatu, mabao matatu ya kufunga na matano ya kufungwa.
Telecom ya Djibouti ambayo itacheza mechi ya mwisho na Gor Mahia kabla ya kuelekea Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kupanda ndege ya kurejea Djibouti haijashinda mchezo hata mmoja hadi sasa baada ya kufungwa mechi zote tatu.
Ilifungwa 1-0 na KMKM, ikafungwa 5-0 na Khartoum na jana imefungwa 3-0 na Yanga SC. 
Hadi sasa unaweza kusema Khartoum na Gor Mahia tayari zipo Robo Fainali, lakini nafasi ya tatu inagombewa na Yanga SC na KMKM-maana yake mechi ya kesho ni ya ‘kukata na shoka’.
Na kihistoria timu za Zanzibar zinapokutana na vigogo wa Bara katika michuano hii ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) huwa ni ‘patashika nguo kuchanika’ basi Yanga kazi wanayo kesho.  
KMKM watahitaji ushindi dhidi ya Yanga SC ili kwenda Robo Fainali

Wachezaji wa Simba SC wakiwa mazoezini kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kujiandaa na mechi dhidi ya AFC Leopards mwezi ujao katika tamasha la Simba Day litakalofanyika na baadaye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Kulia ni kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili, Mserbia DuÅ¡an Momcilovic.



brezzy3
Chris Brown anaziandika headlines kwa mara nyingine tena, siku chache zilizopita staa huyu alikuwa Ufilipino kwa ajili ya kufanya show, lakini akazuiliwa kuondoka nchini humo jana kutokana na mzozo wa mkataba wake wa nyuma.
Chris Brown alizuiliwa Airport siku ya Jumatano asubuhi akiwa anajiandaa kuondoka na ndege yake binafsi kutoka Manila International Airport kwenda Hong Kong kwa ajili ya concert nyingine.
brezzy2
Chombo cha Sheria na Haki Ufilipino ilitoa amri siku ya Jumanne usiku kumzuia Chris Brown kuondoka nchini humo mpaka atakapolipa hela za Promoters walioandaa show kipindi cha mwaka mpya, show ambayo Chris hakutokea.
breezy
Kwa sasa Chris Brown ameambiwa kama atahitaji kuondoka nchini humo kwa sababu za msingi basi itambidi aombe ruhusa kwa Ofisi ya Uhamiaji ambao kama wakikubali basi watampatia cheti kinachoonyesha sababu hizo ni za mzingi na kuwa atarudi.



all-of-zlatan-ibrahimovics-26-league-goals-for-psg-this-season-video
Mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden anayekipiga katika klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa amezidisha uvumi wa kuwa huenda akahama timu hiyo kufuatia majibu ya swali aliloulizwa na jibu alilotoa.
Zlatan-ibrahimovic (1)
Zlatan amekuwa akihusishwa kuhama PSG msimu huu kwa muda mrefu licha ya yeye kutotoa jibu la kukanusha wala kukubali kuhusiana na uvumi huo..Zlatan ambaye amejiunga PSG toka mwaka 2012 akitokea katika klabu ya AC Milan ya Italia amekuwa akihusishwa kurudi AC Milan ambayo imedhamiria kurejesha makali yake kwani msimu uliopita haikufanya vizuri na ilimaliza katika nafasi ya 10 katika msimamo wa Seriea A.
zlatan-ibrahimovic
Baada ya mechi ya michuano ya International Champions Cup ambapo PSG ilishinda kwa goli 4-2 dhidi ya klabu ya Fiorentina ya Italia Zlatan aliulizwa swali kuhusu hatma yake.
TOPSHOTS Paris Saint-Germain's Swedish forward Zlatan Ibrahimovic celebrates after scoring during the French L1 football match Paris Saint-Germain (PSG) vs Caen (SMC) at the Parc des Princes stadium in Paris on February 14, 2015. The match ended in a 2-2 draw. AFP PHOTO / KENZO TRIBOUILLARDKENZO TRIBOUILLARD/AFP/Getty Images
“Nitabakia Paris? Maamuzi yote yapo mikononi mwa Mino Raiola”>>>> Zlatan
Mino Raiola ni wakala wa Zlatan Ibrahimovic ambaye anashughulikia masuala yake yote ya uhamisho kutoka klabu mmoja kwenda nyingine au wakata anaposaini mkataba mpya.
Tetesi za usajili wa kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Angel Di Maria kuondoka Old Trafford na kujiunga na Paris Saint Germain leo zimechukua sura mpya.
 Kwa siku kadhaa baadhi ya vyombo vya habari nchini Ufaransa vimekuwa vikiripoti kwamba mchezaji huyo angeuzwa kwa ada ya zaidi ya Euro Millioni 60 na angetambulishwa rasmi na PSG Ijumaa hii, lakini kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha BeIN Sports kinachomilikiwa na bwana Nasser Ghanim Al-Khelaifi, ambaye mmiliki wa klabu ya PSG – ni kwamba klabu hiyo imeghairi kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo baina ya United na PSG yameisha rasmi. 
Akiwa na miaka 27, Manchester United walivunja rekodi ya usajili ya Uingereza kwa kulipa kiasi cha £59.7m kumsajili Angel Di Maria lakini muargentina huyo ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu ya EPL na inaaminika anavutiwa na wazo la kwenda PSG.
Hata hivyo, inaonekana vilabu hivyo vimeshindwa kuafikiana juu, huku CEO wa United akiripotiwa kutaka kurudisha fedha zote walizotumia kumpata winga huyo.

waliotembelea blog