Baada ya klabu ya Chelsea kupoteza mchezo wa kwanza wa International Champions Cup dhidi ya New York Red Bulls kwa goli 4-2, kocha wa timu hiyo Jose Mourinho hakaukiwi maneno mdomoni mwake kama alivyozoeleka !!
Mourinho
ambaye anafahamika kwa tabia yake ya kupenda kuongea, kubeza na
kujitamba amefurahisha wengi baada ya kuzungumza kauli nyingine za
kujiamini kabisa!!
“Walikuwa na hamasa na furaha ya kucheza dhidi yetu, walituonesha mchezo bora na tulijifunza”>>>Mourinho
“Tumefanya
mazoezi mara 11 ndani ya siku sita, tunawaamini hawa wachezaji,
tuliwahi kucheza mara 10 na hii timu tumeshinda mara 9 lakini kipindi
cha pili kilikuwa majanga”>>>Mourinho
Mourinho kama ilivyo kawaida yake, hajaishiwa kingine cha kuongea >>>>“Mimi ni kocha wa timu bora Uingereza, tuna wachezaji wa viwango vya juu hivyo hakuna udhaifu”>> Mourinho
Mourinho ni kocha mwenye utamaduni wa kujisifia, kuna wakati aliwahi kumponda mchezaji wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu Cristiano Ronaldo, alisema yeye anamtambua Ronaldo mmoja tu naye ni Ronaldo de Lima na hakuna mwingine.
0 maoni:
Post a Comment