Thursday, July 23, 2015



brezzy3
Chris Brown anaziandika headlines kwa mara nyingine tena, siku chache zilizopita staa huyu alikuwa Ufilipino kwa ajili ya kufanya show, lakini akazuiliwa kuondoka nchini humo jana kutokana na mzozo wa mkataba wake wa nyuma.
Chris Brown alizuiliwa Airport siku ya Jumatano asubuhi akiwa anajiandaa kuondoka na ndege yake binafsi kutoka Manila International Airport kwenda Hong Kong kwa ajili ya concert nyingine.
brezzy2
Chombo cha Sheria na Haki Ufilipino ilitoa amri siku ya Jumanne usiku kumzuia Chris Brown kuondoka nchini humo mpaka atakapolipa hela za Promoters walioandaa show kipindi cha mwaka mpya, show ambayo Chris hakutokea.
breezy
Kwa sasa Chris Brown ameambiwa kama atahitaji kuondoka nchini humo kwa sababu za msingi basi itambidi aombe ruhusa kwa Ofisi ya Uhamiaji ambao kama wakikubali basi watampatia cheti kinachoonyesha sababu hizo ni za mzingi na kuwa atarudi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog