Kocha wa klabu ya Arsenal ya Uingereza Arsene Wenger amedumu na klabu ya Arsenal kwa zaidi ya miaka 15 toka alipojiunga nayo 1996, Wenger anakuwa kocha wa pili katika historia ya Ligi Kuu Uingereza kudumu na timu kwa muda mrefu baada ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye amestaafu mwaka 2013.
Kufuatia kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwaka 2013 kumekuwa na maswali mengi kuhusiana na Wenger lini atastaafu, wengi wanaamini Wenger alikuwa na uwezo wa kuifundisha Arsenal kutokana na rekodi alioweka ndani ya miaka tisa ya mwanzo klabuni hapo, Wenger alishinda mataji 7 lakini miaka kumi baadae Wenger ameishia kutwaa mataji mawili pekee rekodi inayotia mashaka kuhusu uwezo wake kwa sasa.
Wengi walitazamia kuwa kuna uwezekekano wa Wenger
kustaafu kwa miaka ya hivi karibuni lakini alichojibu kuhusu suala la
yeye kustaafu bado linawaacha watu njia panda ya lini atastaafu.
“Kustaafu? ndio wakati mwingine huwa inanijia akilini lakini sio zaidi ya sekunde 5 kwa sababu huwa nahofia…Nataka nifanye vizuri na klabu ili siku nitakapoondoka niiache klabu katika nafasi nzuri ili iweze kuendelea poa”>>>Wenger
0 maoni:
Post a Comment